Mkulo: Uchumi unazidi kukua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkulo: Uchumi unazidi kukua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, May 29, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  SERIKALI imesema kuwa ukuaji wa pato la taifa katika unakadiriwa kuongezeka na kwamba pato halisi litakua kwa asilimia 7 katika mwaka 2010.

  Akiwasilisha taarifa ya mwelekeo wa uchumi kwa mwaka 2009 na mwelekeo katika kipindi cha kuanzia 2010 hadi 2013 mbele ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo alisema kuna matarajio makubwa uchumi kuendelea kukua.


  Huku akiwaomba radhi wabunge kwa kuchelewa kuwapa nakala ya taarifa hiyo, Mkulo alisema maelezo hayo yalipitishwa juzi asubuhi na Baraza la Mawaziri.


  "Naomba radhi waheshimiwa kwa kuchelewa kuwapatia nakala ya taarifa hii kwa kuwa imepitishwa jana asubuhi (juzi) na Baraza la Mawaziri hivyo imechelewa kuchapwa," Mkulo alisema.


  Mkulo alisema kuwa katika mwaka 2011, pato halisi la uchumi litakuwa kwa asilimia 7.1, mwaka 2012 asilimia 7.4 na hadi kufikia mwaka 2013 pato halisi la taifa litafikia asilimia 7.8.


  My take:
  Labda hoja yangu niiweke katika msingi wa swali 'nini maana ya uchumi wa nchi kukua Vs hali halisi ya wananchi wake' inawezekana labda mimi ndiye huwa siielewi serikali inaposema uchumi wetu umeongezeka ukilinganisha na mwaka uliopita wakati mfumko wa bei unazidi kupaa huku pato la wananchi walio wengi likizidi kuwa chini ya dola moja kwa siku.
  Naomba msaada tafadhali.
   
 2. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  ni kweli, uchumi unakua kwenye vitabu..ila wananchi chamoto wanakipata..hahaha.
   
 3. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Kuna topographical error, what he means is:

  Jamani hebu wachumi watueleze wanavyosema uchumi wa nchi unakua wana maana gani? Maisha kwa mtanzania wa Tanzania hivi sasa ni dhoofu bin hali, wanaoweza kunywa chai asubuhi ni wachache ( ona bei ya sukari), watu watashindwa kusafiri ona bei ya diesel na petroli, serikali inkopa benki kwa ajili ya kugharimia semina, warsha, kongamano,shimiwi, chai ya ofisi, maonyesho ya sabasaba, nanenae, wiki ya utumishi wa umma etc. Kweli uchumi unakua?
   
 4. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  kwa wafanyabiashara wasiolipa kodi na mafisadi kwao uchumi unakua sasa tena kwa kupaa. na uko ndo serikali inapochukuia statistic zake na si kwa walalhoi kama mimi ambae kila mwezi panga ninalolimwa kwenye PAYE halielezeki kwa kweli
   
 5. A

  Audax JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2010
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hata mimi c amini-juzi wafadhili wamepunguza mgawo-na leo atwambie pato linakua-c kweli kabisa. C amini kwa mapato yapi? Mapato tunayomengi japo mianya mingi imeachwa wazi na wajanja wananufaika.Mwisho wa cku anayepata au kufeel ugumu wa maisha ni sisi watiu wa chini maana vipato vyetu ni vidogo saana ukilinganisha na hali halisi ya maisha,kwani nusu ya mshahara tunaolipwa unaishia kwenye kodi.
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Nijambo la kujipongeza hasa huyu MKULA kwamba uchumi unakuwa ila mifuko ya vigogo ndo inazidi kutuna na wananchi vijijini wanalia kwa umasikini!
   
 7. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2010
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Hehehe hapa ni patamu. Takwimu hizi za ukuaji wa pato la taifa (GDP) hukokotolewa kwa kutumia bei ya kapu la bidhaa ya mwaka (prevailing year's nominal prices) na ni mara nyingi hutoa taswira kwamba mambo ni mazuri ukilinganisha na mwaka au miaka iliyopita. Mheshimiwa waziri jaribu kwanza kudeflate takwimu zako ili uweze kuadjust figures zako kwa mfumuko wa bei (ambao mwaka jana ulikuwa katika high end na mara kadhaa in double digits) upate real GDP figures kabla ya kuongea haya.

  Utamu mwingine waja pale unapoamua kupata dodoso la kiasi gani wananchi wameneemeka (usambazaji wa keki). Sasa ukichukulia pia na sensa ya mwisho ilionyesha na kukadiria kuwa kutakuwa na ongezeko la watu la kati ya asilimia 1.9 na 2.9, hizi takwimu za mheshimiwa waziri zinakuwa ni kichekesho
   
 8. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #8
  May 29, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Unajua hili swala la kukua kwa uchumi ni very controversial kwasababu the major indicator for uchumi kukua ni GDP growth rate. Sasa hizi figure zinaweza kutengenezwa kwa kuongezwa kwani ni indicator for economic activity na sio kukua kwa uhalisia wa uchumi.

  Mfano unaweza kukuta uchumi umekua simply kwasababu ya uchimbaji holela wa madini na sio uwekezaji katika sekta ya madini. Kwa urahisi GDP inaonyesha just economic activity na sio kupanuka kwa sekta za uchumi. Mfano Tanzania sasa hizi kuna economic bubble ambapo sekta za ujenzi hasa hasa real estate sector unakuta bei za ujenzi, ardhi imepanda mno. Sasa sekta kama hii ni hatari kwa uchumi wa Tanzania kwani while construction costs zikiwa kubwa expectation ni kwamba watu watakodisha kwe bei watakayopanga. Sasa hatari inakuja pale ambapo wapangaji watakuwa hawapatikani na baadhi ya wenye majengo wakafilisika. Na mbaya ni kwamba inakuwapo a spillover kama wenye majengo wamekopa serikalini au katika mabenki.

  Kwangu mie binafsi I think uchumi umeshuka by 4.5% Nitatoa sababu kwani a. Kumeshuka kwa kiwango cha uzalishaji wa ndani tumekuwa tunaongeza wimbi la kuagiza vitu kutoka nje. Vilevile sekta za kutegemewa zimekuwa service sector wakati uzalishaji ilibakia katika vinywaji na madini but kikwazo ni kwamba katika madini mikataba mibovu kwa upande fulani inapunguza kwa kiwango kikubwa pato la taifa. Tukija vinywaji ni bidhaa ambazo sio necessity sasa ikiyumba hali ya kiuchumi na pato layumba sasa sijui inakuwaje? Anyway overall sijui criteria za kukua kwa uchumi wa Tanzania ingelikuwa vema Mkulo atupatie mchakato wa hio hali ya kukua kwa uchumi

  Sijalizungumzia swala la kushuka sarafu kwasababu sarafu inashuka kwasababu nyingi na inaweza isichangie kushuka au kupanda kwa uchumi.
   
 9. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #9
  May 29, 2010
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Mkuu Econ 101, definition ya GDP = The total market value of all final goods and services produced in a country in a given year. Takwimu za overall GDP huwa ni mean aggregates za thamani ya soko ya ukuaji wa sekta mbalimbali na hivyo kwa namna moja au nyingine huonyesha angalau kitakwimu kuwa econ activity in sectors considered imeongezeka, translated ukuwaji wa sekta.

  Mkuu usitupetupe tu namba, wewe hiyo asilimia 4.5 umeipatapataje? Assuming unachosema kuhusiana na uzalishaji wa ndani kushuka kwamba ni kweli, je una takwimu za kuthibitisha hili? Pia unatakwimu na formula ya kutuonyesha ni jinsi gani hii imechangia uchumi kushuka kwa hiyo asilimia "4.5" ? Ukitaka kumchambua bwana Mkulo mchambue kwa takwimu zake alizozitoa siyo za kwako wewe.
   
 10. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #10
  May 30, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mkulo apigwa kombora (Nipashe)

  • Aambiwa kazi imemshinda ajiuzulu
  • Ni ndani ya kamati ya Fedha na Uchumi
  • Wamwambia uchumi wa nchi uko hoi
  Wabunge wameibana serikali kuhusu taarifa yake ya hali ya uchumi wa taifa kwa mwaka 2009 na mwelekeo katika kipindi cha muda wa kati (2010/11-2012/13), kwa madai ya kuwa na mipango mizuri isiyotekelezeka, huku baadhi yao wakitaka Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, kujiuzulu iwapo ameshindwa kusimamia uchumi wa nchi.

  Kauli ya kutaka Waziri Mkulo aachie ngazi na kukaa pembeni, ilitolewa na Mbunge wa Viti Maalum, Devota Likokola (CCM), alipokuwa akichangia hoja katika mjadala kuhusu taarifa hiyo ya serikali.


  Taarifa hiyo ilisomwa na Mkulo katika kikao kati ya viongozi, watendaji na wataalamu wa wizara hiyo na Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, katika ofisi ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam jana.Iligusia malengo ambayo serikali ilijiwekea mwaka jana kwa kuzingatia athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia na maeneo ya vipaumbele kitaifa kwa kuwekeza katika shughuli za kiuchumi na kijamii zinazoweza kuchochea ukuaji endelevu wa uchumi kwa mapana zaidi katika muda wa kati wa mwaka wa fedha wa 2010/2011 hadi 2012/2013.


  Katika mchango wake kuhusu taarifa hiyo ya serikali, Likokola alihoji sababu za kutokuwapo kwa utekelezaji katika mipango mizuri inayowekwa na serikali na kusababisha kubaki kwenye makaratasi.“Kama kuna wataalamu, ambao hawasimamii ipasavyo utekelezaji wa mipango mizuri ya serikali, basi wawajibike, hata kama waziri atakuwa ameshindwa kusimamia uchumi akae pembeni,” alisema Likokola.


  Kauli hiyo ilirejewa na Mbunge wa Morogoro Mjini, Dk. Omari Mzeru (CCM), wakati akichangia hoja kuhusu taarifa hiyo ya serikali, ambaye alisema: “Tatizo la Watanzania, tunaandika vizuri, lakini hakuna utekelezaji.”Likokola alisema kumekuwa na ubaguzi katika umiliki wa uchumi nchini, ambapo wageni, ndio wanaomiliki uchumi peke yao na kuhoji:

  “Inakuwaje Watanzania halisi wasimiliki uchumi, badala yake wamiliki Watanzania weupe peke yao kama Mheshimiwa (Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Harry) Kitillya?”

  Pia, alisema licha ya kuwapo kwa Mpango wa Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi na za Umma (PPP), sekta binafsi na zisizo rasmi, zimekuwa zikitengwa na serikali katika ukuzaji wa uchumi licha ya kuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi.

  “Hivi PPP ni kitu gani? Kiko kwenye makaratasi, lakini kwenye utekelezaji hakipo,” alisema Likokola na kumtaka Waziri Mkulo akamuulize Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ili amweleze namna PPP inavyotekelezeka India.
  Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM), alisema serikali imekuwa ikiweka mipango mizuri ya kukuza uchumi, lakini viwanda vingi vilivyobinafsishwa, ama vimekufa au vinafanya kazi chini ya kiwango.

  “Kwa mfano, Morogoro kulikuwa na viwanda 38, leo havifiki hata saba. Kwanini tumefika hapa? Tatizo miundo tunayo, lakini hatuna mbinu. Sasa lazima tutekeleza wenyewe yale tuliyokubaliana,” alisema Ndassa.Alisema miongoni mwa vikwazo vya kukua uchumi, ni pamoja na kuwapo kwa matumizi makubwa katika ofisi ya waziri. Hata hivyo, hakutaja takwimu za matumizi hayo ya ofisi ya waziri.“Pamoja na hayo, matumizi ya waziri ni makubwa, ni balaa. Unakula fedha za ndani na za wafadhili. Matokeo yake hupeleki fedha kwenye shughuli za maendeleo,” alisema Ndassa.


  Sababu nyingine, alisema ni ukosefu wa umeme wa uhakika viwandani na msongamano wa magari uliokithiri, hususan katika jiji la Dar es Salaam, ambao unatishia kudumaza utendaji makazini.Alisema iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa kudhibiti tatizo la msongamano wa magari, itafika wakati watu watafika makazini saa 5 asubuhi na kufika majumbani baada ya kazi saa 4 za usiku na kwamba, wenye magari watakuwa wanaegesha magari yao barabarani.


  Kutokana na hali hiyo, aliishauri TRA kuongeza kasi ya kukagua magari yanayoingia nchini ili kujua kama yana uhalali au la na kuwekwa utaratibu kwa yeyote anayetaka kuegesha gari katika maeneo ya mjini, kutozwa Sh. 5,000, ikiwa ni njia mbadala ya kudhibiti hali ya msongamano wa magari mijini.


  Mbunge wa Mwibara, Charles Kajege (CCM), alishauri kupigwa marufuku uingizaji wa mafuta ya kula kutoka nchini Malaysia kwa vile wazalishaji wa ndani wanashindwa kushindana katika soko kutokana na mafuta yanayotoka nje ya nchi kuuzwa kwa bei ndogo.


  Naye Dk. Mzeru alilaumu ripoti ya msajili wa viwanda, ambayo ilikitaja kiwanda cha zamani cha mafuta ya kula cha Moproco cha mkoani Morogoro kuwamo katika orodha ya viwanda vinavyofanya kazi wakati hakifanyi kazi tangu mwaka 2004.“Mimi ningekuwa rais wa nchi ningekuwa nimeshamfukuza kazi, kwa sababu hii kama si rushwa ni nini?” alihoji Dk. Mzeru.Kiwanda hicho kinamilikiwa na mfanyabishara na mwanasiasa, Aziz Abood, ambaye anatajwa kuwa katika mkakati wa kuwania jimbo la Morogoro Mjini analoshikilia Dk. Mzeru.

  Dk. Mzeru alisema kumekuwa na madai kwamba Moproco imeshindwa kujiendesha kwa sababu ya kodi kubwa.

  Mwenyekiti wa kikao cha jana, Hamza Mwenegoha, alishauri kuundwa kwa kamati ndogo kupata maelezo kutoka Moproco juu ya madai ya kodi kubwa ambayo imewafanya washindwe kuendelea na uzalishaji.


  Naye Mbunge wa Iringa Mjini, Monica Mbega, alisema serikali imekuwa na tabia ya kutotumia vyanzo vyake vyote vya mapato. Alitoa mfano wa mkoa wa Kilimanjaro ambao una vyanzo 317 lakini ni vitano tu vinatambulika.


  Akijibu hoja hizo, Waziri Mkulo alisema baadhi ya hoja zinagusa sera, hivyo zitafanyiwa kazi na nyingine aliwaruhusu wataalamu wa wizara kuzijibu katika kikao cha jana.

  Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Enos Bukuku, akijibu hoja ya Likokola kuhusu kutoshirikishwa kwa sekta binafsi na zisizo rasmi, alisema ziko kwenye maeneo maalum, hivyo kama kutakuwa na faida au hasara, wanaonufaika ni wale, ambao wako katika eneo husika iliko sekta binafsi.

  Kuhusu mfumko wa bei, Bukuku alisema BoT inafanya kila mbinu kuhakikisha hali hiyo inaondoka; aliainisha baadhi ya hatua kuwa ni kupunguza fedha zilizoko kwenye mzunguko, kwamba ifikapo mwisho wa mwezi ujao mfumuko wa bei utakuwa umerejea chini.Awali Waziri Mkulo alisema maeneo ya kipaumbele ya kitaifa kwa sasa ni pamoja na kilimo na maendeleo ya mifugo na uvuvi; miundombinu; uendelezaji wa ardhi na makazi; vitambulisho vya kitaifa; nishati; viwanda na sekta za fedha.


  Waziri Mkulo alisema sekta ya kijamii (elimu, afya na maji), zitaendelea kupewa umuhimu katika mgawo wa fedha. Alisema kuwa mwaka huu ni wa uchaguzi mkuu hivyo kipaumbele cha kipekee kitazingatiwa ili kuhakikisha kuwa unafanyika kama ulivyopangwa.

  Awali, aliyataja malengo, ambayo serikali ilijiwekea mwaka jana kwa kuzingatia zaidi athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kuwa ni pamoja na pato la taifa kukua kwa asilimia 5.0 mwaka 2009, asilimia 5.7 mwaka 2010 na kuongezeka hadi kufikia asilimia 7.2 mwaka 2011 na 7.5 mwaka 2012.

  Pia, kasi ya mfumuko wa bei kupungua na kufikia chini ya asilimia 10, mwishoni mwa Juni, mwaka huu, kuongezeka kwa mapato ya ndani kufikia uwiano na pato la taifa kwa bei ya mwaka husika kwa asilimia 15.9 mwaka 2008/09; asilimia 16.4 mwaka 2009/10; asilimia 17.2 mwaka 2010/11; na asilimia 18.3 mwaka 2011/12.


  Vilevile, kudhibiti ongezeko la ujazi wa fedha kwa tafsiri pana katika wigo utakaowiana na malengo ya ukuzaji wa uchumi, na kasi ya upandaji bei na kuwa na akiba ya fedha za kigeni itakayoweza kukidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma toka nje kwa kipindi kisichopungua miezi mitano, kuwa na kiwango cha ubadilishaji wa fedha kitakachotokana na mwenendo wa soko la fedha na kuondoa vikwazo vya kimfumo na kimuundo katika sekta ya fedha ili kurahisisha upatikanaji wa mikopo kwa sekta binafsi.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  May 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  HIvi na uchaguzi mkuu huu mlitegemea waseme uchumi haukui? hawajipendi? as a matter of fact amesahau kusema kuwa unakua kwa kasi kuliko nchi yoyote katika bara la Afrika na kuwa kumomonyoka kwa uchumi duniani hakukuathiri kabisa hali ya uchumi wetu.

  More troubling is this in "The Citizen"..
  How can people count infusion of more cash as "growth"?
   
 12. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #12
  May 30, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu asante kwa kuniuliza swali hilo let me explain nimeipata wapi figure hiyo kwanza unakubaliana nami kwamba GDP Growth rate ya Tanzania ilikuwa 7.1% 2008-to 7.3% sasa tukiangalia kwamba mwaka 2008-2009 palikuwapo na economic recession Tanzania tumekuwa affect katika real economy na sio banking sector au financial markets. Likewise the global economic trend ilikuwa katika recession na sio growth but nchi nyingi za afrika trend hiyo tunaanza kuisikilizia sasa na sio kipindi kile kwasababu our economy ni cash economy. Sasa tukichukulia mazingira hayo inabidi tutafute wakati ambapo nchi yetu ilikuwa na constant economic growth rate. Tukiassume kwamba uchumi wetu ulikuwa katika constant na sio kukua.

  Tunakuta kwamba mwaka 1995-1999 Tanzania ilikuwa katika constant economic growth rate ya 4.0 (See IMF archive for this). Kutokana na figure hii tunaitumia kama base rate toa na rate ya mwaka 2009 unakuta kwamba uchumi watanzania unategemewa kushuka by 3.1%. Pia IMF walitoa figure ya kwamba GDP ya Tanzania itakuwa 4.5%.

  Hivyo basi ukiangalia figure yangu na figure ya IMF GDP growth rate is between 4.0-4.5% na hilo ni anguko la uchumi from 3.1-3.6%.

  Upo hapo mkubwa?

  Tunamuomba mkulo atupe figures zake amezitoa wapi?
   
 13. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #13
  May 30, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Asante mkubwa labda figures hizi zimewekwa kuwaonyesha wazawa kuwa Tanzania inakua kiuchumi ili tupige kura but fumbo mfumbie mjinga............
   
 14. K

  KEIKEI Member

  #14
  May 30, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii huitwa "growth without development", ni vipimo vya maendeleo vilivyobununiwa na WB na IMF kwamba maendeleo yaangaliwe kwa percapita income. UNDP utumia human development index kwa kuangalia life expectancy, education, standard of living na hiyo percapita income na ukitumia vipimo hivi ndiyo utapata majibu kamili ya Tanzania iko wapi. Mkulo anatoa hii state of the economy report kwa sababu za kisiasa tu na kuwafurahisha WB na IMF.
   
 15. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #15
  May 30, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Mkullo and his gang are trying to cheat us by using cooked figures!! Ndio zao hizo, mnakumbuka hawa jamaa walimuingiza mkenge Kikwete kwenye figures alizotoa juu ya wage bill ya taifa ingekuwaje kama serikali ingeridhia maombi ya TUCTA!!
  Mkullo , with due respect remember that you can lie with your figures but figures do not lie!!
   
 16. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #16
  May 30, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mkulo mkulo mkulo.
  et all
   
 17. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #17
  May 30, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kama uchumi unakua na pato la Serikali linaongezeka, kwa nini bado tunategemea 40% ya bajeti kutoka kwa wahisani na tumekwenda kopa Stanbic?
   
 18. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #18
  May 30, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  On the other hand, did Mkulo factored that 40% of that growth is tied to donor grants and loan and in reality we do not own and enjoy the whole 7%?
   
 19. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #19
  May 30, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mi natamani kutapika nikimsikia huyu mkulo maana haelewi kitu
   
 20. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #20
  May 30, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hilo ndilo haswa swali ninalojiuliza kama uchumi wetu unaongezeka kwanini serikali isiwaongezee angalau mishahara wafanyakazi wake wanaofanya uchumi ukue au ndio uchumi unaosemwa unakua kwenye makaratasi, kweli bado sijapata jibu sahihi kuna siku itanilazimu niende binafsi ofisini kwa Mkulo kumuuliza hili swali.
   
Loading...