Mkulo: Posho za wabunge zinaweza kufutwa

lifeofmshaba

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
867
219
25th June 2011

Bpe
Mkullo3(31).jpg

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo
Serikali imesema suala la kuondolewa kwa posho za vikao kwa wabunge linawezekana isipokuwa mchakato ni lazima uanzie katika kamati ya uongozi ya Bunge.
Kauli hiyo ilitolewa juzi jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa magari 15 yaliyotolewa na Uingereza kwa ajili zoezi la Sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwakani.
Mkulo alisema suala la posho za wabunge limekuwa kubwa na kujikita katika vichwa vya watu katika siku za hivi karibuni na kusema kuwa suluhisho lake ni kamati ya uongozi ya Bunge ambayo kama itaona zinafaa kuondolewa zitaondolewa bila kikwazo chochote.
"Unajua hizi kanuni na taratibu za Bunge zinasimamiwa na kamati ya uongozi ambayo ina jukumu la kuamua kuzibadilisha ama kuziacha zikiwemo hizi za kuwalipa wabunge posho," alisema.




CHANZO: NIPASHE
 
Nawashauri waongeze Perdiem toka TShs. 70,000 ya sasa hadi TShs 120,000 na posho zifutwe.
 
sasa kama kamati ya uongozi ndiyo yenye dhamana wanalikuwa waleta ubishi wa nini kumbe hata issue sio ya serikali?
kwa nini hakutoa haya maelekezo toka mapema kuliko kutoa majibu ya kejeri hapo mwanzo
waziri wa hovyo sana huyu, yeye kwa sababu kavimba tumbo kwa hela ya kodi anadhani watu wote wana hali nzuri kimaisha kama yeye
 
Ni faraja kusikia kwamba dhamira ipo. Nashauri hili lifanyiwe kazi mapema maana ni kero iliyogusa wengi.
 
Kwanini kamati ya bunge ambao wote ni wabunge ndio wajadili maslahi yao. Hapo kuna conflict of interest. Ni sawa Seriali Iseme TUCTA ijadili posho za wafanyakazi..

Katika huo mchakato kunatakiwa kuwa watu wa nje ya bunge . La sivyo tume ya maadili ya viongozi ipewe kazi hiyo na sio kamati ya bunge pekee.
 
Mnyasa huyoooo.
sasa kama kamati ya uongozi ndiyo yenye dhamana wanalikuwa waleta ubishi wa nini kumbe hata issue sio ya serikali? kwa nini hakutoa haya maelekezo toka mapema kuliko kutoa majibu ya kejeri hapo mwanzowaziri wa hovyo sana huyu, yeye kwa sababu kavimba tumbo kwa hela ya kodi anadhani watu wote wana hali nzuri kimaisha kama yeye
 
Back
Top Bottom