Mkulo: Posho za wabunge zinaweza kufutwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkulo: Posho za wabunge zinaweza kufutwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dingswayo, Jun 25, 2011.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Serikali imesema suala la kuondolewa kwa posho za vikao kwa wabunge linawezekana isipokuwa mchakato ni lazima uanzie katika kamati ya uongozi ya Bunge.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  Kauli hiyo ilitolewa juzi jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa magari 15 yaliyotolewa na Uingereza kwa ajili zoezi la Sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwakani.[/FONT]

  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mkulo alisema suala la posho za wabunge limekuwa kubwa na kujikita katika vichwa vya watu katika siku za hivi karibuni na kusema kuwa suluhisho lake ni kamati ya uongozi ya Bunge ambayo kama itaona zinafaa kuondolewa zitaondolewa bila kikwazo chochote.[/FONT]

  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Unajua hizi kanuni na taratibu za Bunge zinasimamiwa na kamati ya uongozi ambayo ina jukumu la kuamua kuzibadilisha ama kuziacha zikiwemo hizi za kuwalipa wabunge posho,” alisema.[/FONT]


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mnafiki huyo, keshasahau mipasho aliyokuwa anatoa Bungeni na kwenye Media majuzi tu. Angesema hivyo awali kungekuwa na tatizo?
   
 3. A

  AlamaZA NYAKATI JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa vile bajeti yake imeshapita ndo anataka kutudanganya sis, unafiki mtuopu
   
 4. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hatudanganyiki mkulo mnafiki sn..alisema haiwezekani leo iweje anasema inawezakana?
   
 5. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  mzee hapo anatupiga changa la macho tu,hakuna lolote watakalo fanya,watu wanalinda na kutetea posho za kulala bungeni[sleeping allawance]
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  Jun 25, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  nilisema lile baraza la mawaziri la Kikwete , ni baraza lililojaa watu wamizaaa , matani na masihara
   
 7. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  hilo ni changa la macho analojipiga mwenyewe. hivi sasa wamejitengenezea maswali yasiyojibika kwa wapiga kura wao, ndio maana hata bashe kapaona, wakifanya ubabe wa kukubaliana na uhalisia wataona impact yake. Nyingine iliyozidi kuwaacha hoi ni ya Mbowe kuwarudishia Shangingi. Hizi ni zama za hoja za ukweli zinazochangia maisha ya mwananchi kuwa duni.
   
Loading...