Hizi ni zama mpya. Hapo nyuma mbunge wa aina hii angeonywa kwenye vikao vyao vya chama, na akileta jeuri angetimuliwa uanachama wa magamba kitu ambacho magamba walijua hata uchaguzi ukirudiwa wangeshinda. Sasa hivi mambo ni tofauti sana. Nilianza kuona hofu ya magamba pale waliponywea baada ya kumhusisha Dr Kigwangala na ule mgomo wa madaktari. Komaa Kangi, tunataka kujua Mkulo alivuta kiasi gani kwenye uuzwaji haramu wa kile kiwanja (nyumba?) iliyokuwa mali ya serikali, wakileta za kuleta tutakupokea CDM.