Mkuu,
Asante kwa taarifa yako. Hata hivyo, pia tungependa kujua iwapo amezungumzia chochote kuhusu taarifa ya Task Force iliyokuwa imeundwa kushughulikia suala hili. Kwa kumbukumbu za haraka haraka ni kwamba timu hiyo ilishakabidhi taarifa yake kwa serikali.
Au ndio tudhanie tu kwamba aliyowaeleza mkulo leo ndio executive summary ya riport?
Binafsi, naamini report ya tume iliyoundwa ndiyo itaweza kueleza kinaga ubaga ni wanachama kiasi gani walikuwa wamepanda mbegu zao na bado walikuwa walisubiri 'kuvuna' kwa kipindi chote na si wale tu wa miezi mitatu.
Mbali na hilo, we go east, we go west, nawatupia lawama sana our intelligence forces kwa kushindwa kung'amua mchezo huu mchafu tangu ulipoanza na kuweza kuvushauri vyombo husika juu ya hatua za msingi za kuchukua kabla ya maelfu ya watanzania wenzetu kuingizwa mkenge na wenzao whachache.
Naamini kuna watu wanastahili kuwajibika na kuadhibiwa kule usalama wa Taifa pamoja na kamati ya ulinzi na usalama katika baadhi ya mikoa na wilaya.