Mkullo na Zitto: Mnajiandaaje Na Bajeti? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkullo na Zitto: Mnajiandaaje Na Bajeti?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mchambuzi, Feb 3, 2012.

 1. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Imebakia miezi mine kabla Bajeti ya Mwaka Mpya wa fedha 2012 – 2013 kutangazwa. Ingawa bajeti hizi utangazwa kila Mwezi Juni ya mwaka, maandalizi uanza muda mrefu. Kwa maana hiyo, maandalizi ya bajeti ya mwaka huu wa fedha tayari yameshafikia mbali. Hivyo nimeona nije na mjadala huu ili sisi wananchi huku ‘site’, tupate wasaa wa kujadili matarajio yetu badala ya kusubiri kuja shitukizwa na takwimu mbalimbali ifikapo Mwezi Juni 2012. Nimewataja Mkullo na Zitto kwa sababu Mkullo ni Waziri wetu wa Fedha na Uchumi, na Zitto ni Waziri wetu Kivuli wa Fedha na Uchumi. Na success au failure ya bajeti yetu ijayo, kwa kiasi kikubwa itatokana na kazi ya viongozi hawa wawili.

  Kwa ujumla wake, bajeti ni maelezo kuhusu MAPATO na MATUMIZI. Ukubwa wa bajeti ya nchi utegemea ukubwa au wingi wa mapato yake. Katika hali ya kawaida, serikali inapokusanya mapato kidogo, matumizi kwa ajili ya huduma kama elimu, afya, n.k, huwa ni madogo, hivyo kuchangia Bajeti ya namna hii kutokuwa na manufaa kwa wananchi walio wengi. Lakini serikali inapokusanya mapato mengi, matarajio miongoni mwa wananchi wengi huwa ni ‘maisha bora’.

  Bajeti ya 2011-2012 ilituacha na mambo mengi, lakini sitayadili kwa sasa. Kilicho muhimu ni kwamba, pamoja na jitiada zote za serikali zilizojaa mbwembwe, kauli na ahadi mbalimbali katika bajeti ya mwaka jana, serikali iliishiwa hela ndani ya miezi sita. Na hivi sasa, ili Serikali iweze kufika mwezi Juni 2012, inahitaji bajeti ndogo, kuongezea katika bajeti iliyopita ambayo ilikuwa ni ya jumla ya Sh. Trilioni 13.5. Vyanzo vya Bajeti hii vilikuwa vifuatavyo:
  1. Wahisani walichangia asilimia 29%
  2. Jumla ya mapato ya ndani: 50%
  3. Huku Mapato ya TRA yakiwa ni: 46%
  4. Na Mapato Yasiyo ya TRA yakiwa: 4%
  5. Mikopo yenye masharti ya kibiashara 9.4%
  6. Mikopo ya ndani (isiyo na masharti ya kibiashara) 8.9%
  7. Mapato kutoka kwenye halmashauri zetu nchini 2.59%
  JUMLA 100%


  Wakati anawasilisha Bajeti hii mwezi juni mwaak 2011, Waziri Mkullo ali ahidi Mengi. Lakini muhimu ilikuwa ni pamoja na serikali kupunguza kutegemea wahisani katika bajeti zetu ambalo Mkullo aliahidi kiwango hiki kuzidi kushuka hadi kufikia chini ya 10% ya bajeti, ifikapo mwaka 2015. Katika bajeti iliyopita, mchango wa wahisani ulikuwa ni 29%. Pia Mkullo alitamka kwamba ili kufanikisha hili, itahitaji hatua madhubuti za serikali kuongeza mapato ya ndani, ikiwa ni pamoja na kupanua ‘wigo wa kodi’ (tax base), kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa kodi, kutambua walipa kodi wapya na kudhibiti matumizi ya serikali. Mkullo alisitiza kwamba ifikapo mwaka 2015, juhudu hizi zitasaidia kupunguza utegemezi wa wahisani katika bajeti kufikia kiwango chini ya 10% ya bajeti, na pia ongezeko la mapato ya kodi kufikia 20% ya GDP.

  Kipimo cha ufanisi wa serikali yoyote katika ukusanyaji kodi ni uwiano kati ya mapato ya kodi (Revenue) na pato la Taifa (GDP) i.e. Tax to GDP ratio. Kwa upande mmoja, uwiano huu ukiwa mkubwa, unazaa tafsiri kuu tatu: Moja, nchi inakusanya kodi kwa ufanisi; Pili, ukwepaji kodi upo kiwango cha chini; na Tatu, rushwa katika ukusanyaji kodi ipo chini. Kwa upande mwingine, uwiano huu ukiwa mdogo, tafsiri yake ni kinyume cha haya mambo matatu. Kwa Tanzania, Tax to GDP Ratio hutajwa kuwa ni 16% ya pato la taifa, lakini vyanzo vingi vya uchambuzi vinafafanua kiwango hiki kuwa kipo chini zaidi ya hapo i.e. kati 12% na 14%. Nchi zinazoongoza duniani katika ufanisi wa ukusanyaji wa kodi ni: Denmark (48%), Sweden (47%), Belgium (46%), Cuba (44%), na Finland (43%). Tano bora Afrika ni Swaziland (39%), Botswana (35%),Seychelles (32%), Namibia (29%), na Afrika ya Kusini (28%).

  Katika bajeti yetu ya 2010-2011, serikali iliweka malengo kukusanya kodi 17% ya GDP, lakini malengo haya hayakufanikiwa. Pamoja na malengo haya mazuri, imekuwa vigumu kwa serikali yetu kuongeza uwiano huu ‘consistently’. Uwiano huu haujawahi kuvuka 15%. Tulipata mafanikio kidogo katika miaka ya mwanzo ya kuzaliwa kwa TRA (1997 – 2000), lakini sio kwa muda mrefu. Pamoja na kwamba kwa katika kipindi cha 2000-2011, uchumi wa Tanzania umekuwa kwa wastani wa karibia 7%, takwimu hii haiendani na ongezeko la Tax to GDP Ratio. Hili ni jambo la kustaajabisha sana kwani ni kinyume kabisa na kanuni za msingi kabisa za uchumi.

  Wanasiasa wamekuwa wanatoa maelezo mbalimbali kuhusu sababu ya tatizo hili, kubwa ikiwa ni hali mbaya ya uchumi duniani. Lakini ukweli unabakia wazi kwamba, chanzo kikubwa ni Rushwa na Ukwepaji kodi, kwani, given kwamba kiwango cha tax to GDP ratio kina uhusiano wa moja kwa moja na kasi ya ukuaji wa uchumi, kiwango hiki kubakia chini licha ya kasi ya kukua kwa uchumi inatoa tafsiri kuu mbili tatu: Moja, wanao faidika na ukuaji uchumi ni wahujuhu uchumi; mbili, wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yetu ni wahujumu uchumi; na tatu ni sababu zote mbili hapo juu. Hivyo, kuna kila dalili kwamba hali ya mapato duni kwa taifa letu inatokana zaidi na mapungufu yaliyopo ndani ya nchi yetu, kuliko nje. Nitajadili mambo makuu kumi na tatu

  Moja, sehemu kubwa ya mapato yetu inatokana na VAT. Michango toka vyanzo kama Corporate Income na Personal Income Taxes bado vipo chini sana. Nchi nyingi zenye mafanikio, Corporate na Income Tax huchangia sana, mara nyingine kuliko VAT.

  Pili, ‘Wigo wa Kodi’ (Tax Base) Tanzania umefikia kikomo. Ni vigumu sana kuupanua zaidi kama njia ya kupata vyanzo vipya vya kodi. Asilimia kubwa ya shughuli za uchumi bado zipo ‘informal sector’, na wananchi wengi bado hawana mwamko wa ku ‘formalize’ shughuli zao, kwa sababu kuu mbili: (1) Ku ‘formalize’ kunawaongezea gharama za uendeshaji; (2) hawaoni uwiano baina ya wingi wa kodi na ‘maisha bora’.

  Tatu, Tanzania ina jumla ya walipa kodi wakubwa 400, idadi ambayo ni ndogo ikifafanishwa na kwingine Afrika. Hii ni sawa na 8% tu walipa kodi Tanzania. Walipa kodi hawa wakubwa huchangia 70% ya kodi yote Tanzania. Sasa kutokana na tatizo lililopo la serikali kushindwa kuongeza wigo wa kodi (tax base) kwa sababu tulizoziona awali, walipa kodi hawa 400 ndio ubeba mzigo wote, na ndio maana wanaongoza kwa kutoa rushwa kama njia ya kujipunguzia mzigo huu mkubwa.

  Nne ni Personal Income Tax (PIT). Wamiliki wengi wa makampuni wana tabia ya kutowasajili wafanyakazi wao, ili kuwalipa chini ya meza, kama njia ya kukwepa kulipa Personal Income Tax. Tabia hii huinyima TRA mapato mengi kila mwaka.

  Tano ni ‘Capital Gain Tax’.Kwa kawaida, Capital Gain Tax or Loss inajumuishwa in the business or investment income. As matter of “Principle”, kodi yake ni asilimia 30%, but as a matter of “Practice”, kodi hii ni rahisi sana kuikwepa Tanzania.

  Sita – Nje ya mapato ya TRA, serikali pia inavyanzo vingine kama vile mapato from renewable natural resources, kama uvuvi, misitu, wanyama pori n.k. Mapato haya hukusanywa na taasisi/wizara husika pamoja na halmashauri mbalimbali, na sio TRA. Lakini ni jadi kwa serikali kupokea mapato kidogo sana kutoka vyanzo hivi kutokana na ufisadi. Kwa mfano, wakati bajeti ya 2011-2012 ilitokana na mapato ya TRA ya kama Shilingi trilioni 6.2; mapato yasiyo ya kodi yalikuwa ni shillingi bilioni 547 tu. Hiki ni kiasi kidogo sana ikilinganishwa na shughuli kubwa zinazoendelea katika sekta za uvuvi, misitu, wanyamapori n.k.

  Saba - Sekta ya Madini. Sekta hii ina ‘potential’ kubwa sana ya kuokoa uchumi wetu kifedha, lakini tatizo kubwa lililopo ni kwamba, bado madini yanamilikiwa na makampuni binafsi kwa 100%, hivyo kuzipa ugumu mamlaka husika kupata ukweli juu ya gharama za uendeshaji wa migodi hii. Ndio maana imekuwa jadi kwa mamlaka zetu kupokea taarifa za ‘biashara kichaa’ kutoka migodini bila kuhoji.

  Nane, uwezo wa TRA kusimamia ukusanyaji kodi bado ni mdogo sana. Kwa mfano, tax administrator available kwa kila watanzania 1,000, ni 0.087, licha ya TRA kufanya kazi masaa 24.

  Tisa, katika mazingira ya kawaida, Mamlaka za Ukusanyaji Kodi huwa zinajiendesha kwa ku ‘retain’ asilimia kadhaa ya mapato yonayokusanywa. Kwa mfano, Organization for Economic Cooperation and Development (OECD) inazitaka nchi kuziruhusu mamlaka hizi ku ‘retain’ 1% ya mapato kwa ajili hiyo. Vilevile Serikalu hushauriwa kuwa watumishi za Mamlaka ya mapato mishahara na marupurupu mazuri kama incentive ya kuwaongezea ufanisi. TRA ilianza kulipa watumishi wake mishahara minono tangia miaka ya mwisho ya 1990. Lakini kuhusu retaining 1%, ilikuja bainika kwamba kiwango hiki ni kidogo sana kuwezesha TRA kujiendesha kwa ufanisi. Hivyo serikali ikapandisha kiwango hiki hadi kufikia karibia 3% ya mapato ya TRA kwa mwaka. Lakini pamoja na haya yote, bado ilizidi kubainika TRA inapata wakati mgumu kuendesha shughuli zake za ‘modernization’, hasa uboreshaji wa miundombinu, gharama za ICT – Hardware, Software, Training n.k. Kutokana na hali hii, WorldBank na DANIDA ndio wamekuwa wanagharamia shughuli nyingi za modernization ya TRA, kitu ambacho kidogo kinashangaza, hasa kwa kuwa - WorldBank na DANIDA hawafanyi haya bure, bali gharama hizi zinalipiwa na walipa kodi wa Tanzania.

  Kumi – ni kuhusu Serikali za Mitaa. Kodi nyingi zinazotozwa na halmashauri zetu zinaleta vikwazo vingi sana kwa wananchi. Tumeona awali kwamba mapato kutoka halmashauri zote nchini katika bajeti iliyopita ilikuwa ni 2.59% tu ya jumla ya mapato yote. Sababu kubwa ya kiasi hiki kidogo ni ufisadi, lakini pia urasimu usio wa lazima. Kwa mfano, mfumo wa sasa wa kodi katika halmashauri hautoi incentives zozote za maana kwa wananchi wenye nia yak u ‘formalize’, katika kilimo cha kisasa na ujasiriamali, badala yake, structure zilizopo zinazidi kuwavunja moyo, hivyo kupelekea wengi kuchagua kubakia kwenye ‘informal sector’. Kwa mfano, ni kawaida kwa halmashauri nyingi kutoza fees mbalimbali ‘up front’. Pia fees na kodi nyingi mara nyingi hazijali ukubwa au udogo wa biashara husika. Vilevile kuna tatizo la wananchi kutozwa kodi mara mbili (double taxation), ambapo hutakiwa kulipa kodi Serikali kuu na Halmashauri/manispaa, badala ya kuwa na mfumo wa aina moja.

  Kumi na moja ni Ufisadi – Ufisadi na Ubadhirifu wa fedha za Bajeti za serikali unakadiriwa kugharimu karibia 25% ya bajeti.

  Kumi na Mbili – ni Capital Flight (Fedha zinazotoroshwa nje ya nchi kwa hila). Tabia huchangia sana mmomonyoko mkubwa sana katika wigo wetu wa kodi (Erosion of the Tax Base). Kuna utafiti unaonyesha kwamba, mwaka 2008, Tanzania ilipoteza zaidi ya USD million 350, kupitia mtindo huu. Lakini mwaka 2004 ndio uliovunja rekodi kwani, kiwango hiki kilikuwa zaidi ya USD Bilioni 1.1; Katika kipindi cha 2000 – 2008, jumla ya USD 2.6 Billion zilipotea kwa mtindo huu. Vilevile, kwa wale wanaokumbuka, Gavana wa Zamani wa Benki Kuu, Marehemu Balali aliwahi tamko miaka kama sita iliyopita kwamba, kwa taarifa alizonazo, kuna zaidi ya Dollar Billioni Mbili za watanzania zinazotambulika rasmi katika mabenki ya nje. Tutambue kwamba hizi ni zile zinazotambulika rasmi, na hazihusishi mamilioni mengine ya dollar ambayo yamefichwa kwenye kwenye off-shore accounts huko Jersey Island, Mauritius n.k., ambako nchi hizo huwa na mikataba maalum ya kutotoa siri hizi. Vilevile idadi ya Balali haiusishi mamilioni ya dollar ambayo yametumika kununua majumba na hisa za mabilioni ya dollar nje ya nchi. Katika mazingira ya kawaida, fedha zote hizi ilitakiwa zilipiwe kodi. Kwahiyo ni muhimu sana kwa mjadala wowote kuhusu serikali kuongeza ‘tax base’ pia uhusishe suala la Capital Flight, vinginevyo tax system haitakuwa equitable. Kabla ya kulazimisha wananchi to 'formalize' shughuli zao ili wawe walipa kodi, tuanze na 'capital flight', kwani hizi fedha zipo na nyingine nyingi zinazidi kutoroshwa kila siku.

  Na Mwisho ni juu ya Misamaa ya kodi. Hivi sasa, misamaha hii ni zaidi ya 20% ya mapato ya TRA kwa mwaka, na karibia 10% ya bajeti yetu. Hii ina maana kwamba, ubadhirifu wa mafungu ya bajeti, misamaha ya kodi, n.k, upelekea zaidi 35% ya bajeti yetu ya mwaka kwenda into ‘waste’.

  Tunakumbuka jinsi gani mpango wa Serikali wa kuanza kutoza kodi NGOs and taasisi za kidini ulivyokwama bungeni mwaka 2010, na hivyo kuifanya serikali iendelee kuzisamehe kodi taasisi hizi. Lakini bunge lile halikutupatia wananchi picha halisi juu ya suala hili.

  Je, nani ni mabingwa wa misamaha ya kodi?

  1. TIC 39.28%
  2. VAT Exemptions: 25.96%
  3. DFP (Exemptions to donor’s projects) 10.4%
  4. Government Institutions Exemptions 7.55%
  5. Mining Companies Exemptions 7.14%
  6. Private Companies and Individuals Exemptions 5.13%
  7. Parastatal organizations Exemptions: .01%
  8. Duty Free Exemptions 0.04%
  9. Taasisi za kidini Exemptioons 0.04%


  Ni dhahiri kwamba taasisi za dini zilistahili kuachiwa ziendelee kutolipa kodi kwani kama tunavyoona, misamaha kwao ni kidogo sana ikilinganishwa na sekta nyingine za uchumi.
   
Loading...