Mkulima wa Tanzania, August 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkulima wa Tanzania, August 2011

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by LENGEJU BOB, Aug 20, 2011.

 1. L

  LENGEJU BOB Member

  #1
  Aug 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aliandaa shamba kwa panga, fyekeo na jembe la mkono, akapanda bila mbolea kwakuwa viongozi wa serikali ya kijiji na mawakala wa pembejeo walichakachua mbolea ya ruzuku. Mvua haikunyesha pamoja na maombi ya mkesha msikitini na makanisani, mazao kidogo yaliyochomoza yalishambuliwa na magonjwa na wadudu. Kipande cha robo eka alichopanda nyanya kimemzalishia tenga noja la nyanya (kama kilo 80 hivi) kwa mchumo wa kwanza. Bei ya soko ni Tsh. 6,000 kwa tenga, 500 atampa kijana aliyemsaidia kuchuma nyanya na 500 atamlipa kijana aliyemsaidia kubeba tenga la nyanya mpaka sokoni.
  Kufika sokoni, kabla ya kuuza atadaiwa Tsh 1000 ya ushuru, (analazimika kukopa kwa jirani) na baada ya kuuza na kulipia deni la ushuru anabakiwa na 4000. Anaskia kiu, njaa na uchovu, lakini anatakiwa kutembea km 10 kutoka sokoni kurudi nyumbani, akiwa n ash. 4,000 mkononi. Mkewe nyumbani amejaa taraja,anajua baba ametoka kuuza mazao, ameandaa orodha ya mahitaji nyumbani

  1. Mahitahi ya lazima ya nyumbani

  SUKARI 2,500/KG

  CHUMVI 1,000/KG

  MAFUTA YA TAA 2,100/LITA

  MAFUTA YA KUPIKIA 400/ROBO

  JUMLA 6,000  2. Mahitaji ya watoto shuleni (vinginevyo mtoto atafukuzwa shule

  DATFARI 1,000

  MCHANGO WA JENGO 1,000

  MADAWATI 1,000

  MITIHANI 1,000

  JUMLA 4,000  3. Michango ya kijisi (vinginevyo atasombwa na mgambo na kulazwa ofisi za Kijiji)


  ULINZI SHIRIKISHI 1,000

  ZAHANATI 1,000

  JUMLA 2,000


  JUMLA KUU 1+2+3 = 12,000 (-4000) = 8,000 DENI!

  MARA mkulima anakumbuka robo nyingine ya ekari aliyolima mahindi, na anapata taarifa kuwa mjini mahindi yana bei nzuri kidogo, haraka anaenda shamba, kwa kazi ya siku nzima anafanikiwa kuvuna gunia tano! Anaweka tatu ghalani kwa ajili ya chakula, anafikiria kuuza mbili kupata pesa za kujikimu. Anakodi mkokoteni, kichwani anawaza ukombozi, anajua akiuza mahidi atapata pesa kidogo ya sukari, chumvi, michango ya shule na kijiji…………….


  GHAFLA anakutana na kizuizi njiani “NI MARUFUKU KUUZA MAZAO YA CHAKULA” Mgambo wanamuamuru arudi na mkokoteni wake haraka kabla hawajataifisha na mahindi yake!.. Amechanganyikiwa, anapoteza uwezo wa kuona, kufikiri na hata kusikia, kwa mbaaaali anasikia tangazo la wizara ya afya, likihimiza watu wale mayai, kuku, nyama….Tangazo linasisitiza kuwa watanzania ni wavivu wa kula nyama na maziwa……..sauti hizo zinachanganyika na kile kibwagizo alichokisikia miaka ile ya uchaguzi………Maisha bora kwa kila Mtanzania………

  Machozi yanasombwa na Jasho!  TAFAKARI, AMUA CHUKUA HATUA……………………….
   
 2. kasopa

  kasopa JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 304
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu maneno yako ni msumari juu ya mbao, asee Dagama unawapeleka wapi watanzania?
   
 3. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145

  eti ni wavivu wa kula nyama na maziwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
  Wanazo hizo hela za kununulia nyama na maziwa?
   
Loading...