Lawkeys
JF-Expert Member
- Nov 16, 2009
- 1,118
- 287
Hivi karibuni nimesikia jitihada za serikali kuzuia uuzaji wa mazao ya chakula nje ya nchi. Sina shaka kwamba hatua hizo ni kinyume cha kanuni za biashara huria, na pia kwamba zina madhara ya moja kwa moja kwa mkulima kwani itamlazimu kuuza mazao kwa bei ya chini. Hakuna asiyejua jinsi sekta ya kilimo ilivyosahaulika. Wengi mashahidi, mlisha nchi mpaka kesho anatumia jembe la mkono, jua kali. Serikali makini ingesoma inadvance demand ya chakula na kuwawezesha watanzania kuzalisha ziada na wao kunufaika na kazi yao na sio kukaa chini kujadili jinsi ya kudhibiti soko la chakula.
Mimi naona hapa mkulima hatendewi haki.
Mimi naona hapa mkulima hatendewi haki.