hb81
JF-Expert Member
- Jul 22, 2016
- 289
- 181
Jamani ndugu zangu wakulima wa tanzania hivi tumeikosea nini tanzania maana sasa hivu bei ya mazai umeshuka kiasi kwamba hakuna faida yeyote ile ya kulima mahindi maharage mpumga nk kwa sababu ya bei nchi hii kila mkoa unakubali kwa kilimo hivo sio rahisi mkulima wa moshi kupeleka mazao yake arusha au mkulima wa ruvuma kupeleka mazao yake iringa mkoa pekee ambao ni kimbilio la mazao mengu ni dar es salaam sasa miioa yote tanzania tukipeleka mazao yetu dar es salaam kunabiashara tena hapo suluhisho la mkulima wa nchi hii ni mipaka ya nchi kufunguliwa na kuruhusu mazao kwenda nje ya nchi tunaiomba s serekali yetu tukufu gharama za kilimo ni kubwa sana kuanzia kukodi shamba kulima pembejeo ni ghali nk .sasa hivi kwa maadhi ya mikoa mahindi gunia la sado 30 ni 24000/35000 hakuna zaidi sasa ukiangalia hapo na gharama halisi za kilimo ni hasara kubwa sana kwa mkulima wa nchi hii tunaomba wadau wa kilimo ikiwemo wizara ya kilimo kuangalia suala hili la bei ya mazao kwa ujumla yake sisi wakulima tunapata hasara sana kwa sababu ya mipaka kufungwa tuanajua nia ya serekali ni njema kwa wananchi wake ila kwa sisi wakulima hali ni tete na kuna uwezekano kwa miaka ijayo tukashindwa kabisa kuwa na mitaji ya kilimo. Asante Tanzania