MKUHUMI ndio nini jamani?

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Nov 27, 2010
2,591
1,599
Habari wanaJF, hivi majuzi nilimsikia waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira akizungumzia kuwa kuna mkakati unaoitwa MKUHUMI au kwa kizungu REDD ambao lengo lake ni kuhamasisha wananchi kutunza misitu na kulipwa fedha baada ya kuhifadhi hiyo misitu yao. Lengo ni kupambana na uharibifu wa misitu ili kukabiliana na hili tatizo la mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa wenye data kamili kuhusu mpango huu tafadhali naomba mnifafanulie ili nifahamu zaidi kwa sababu na mimi ni mkereketwa wa mazingira.
Nawasilisha!!!
 
:embarassed2:

M
kakakti wa KUHujumu Uchumi kupitia mgongo wa MIsitu baada ya kumaliza kwenye migodi na umeme
 
:embarassed2:

M
kakakti wa KUHujumu Uchumi kupitia mgongo wa MIsitu baada ya kumaliza kwenye migodi na umeme

Mhhhh, hii ya kwako inaonekana kali.....kwa hiyo jamaa wanahamia kwenye misitu baada ya kumaliza madini. sasa mbona naskia watu watakuwa wanalipwa lkn miti haikatwi? itakuwa uhujumu kweli huu, hebu fafanua...
 
Ukitaka ufafanuzi angalia maneno yao wakati wanaanzisha mikakati yao....Utahis ndani ya muda mfupi Tanzania iko peponi

Fuatilia utendaji na matumizi,....vikao, posho, pesa za makalio wanaita seating allowances etc
 
hilo nalo neno.....posho ya makalio?????
 
asante sana mkuu, kwa mawazo yako, unadhani mkuhumi utawafaidisha wananchi wa hali ya chini kabisa?

Mkuu, si unajua tena siasa za nchi yetu? Kwenye makaratasi huu mpango unaonekana ni mzuri sana na utawafaidisha hata watu wa chini. Lakini kwenye utekelezaji ni jinamizi tupu, utachakachuliwa hadi ushangae.
 
hilo nalo neno.....posho ya makalio?????

Sasa mkuu kama hazina tija na wengine wanaenda tu kukaa na kuchapa usingizi tuziite nini kama sio fidia kwa kuitwa na kuyakalisha makalio yao kwa muda mrefu vitini mpaka kuumia na sio kuumiza vichwa kuja na something valuable that can be implemented?

Tunaongoza kwa mikakati na sio kwa matokeo ya mikakati....mapungufu makubwa haya
 
Back
Top Bottom