Mkuchika atoka kifungoni... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuchika atoka kifungoni...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngongo, Feb 20, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  JUKWAA la Wahariri nchini limetangaza kumfungulia rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika baada ya kutoandika habari zinazomhusu kwa kipindi cha miezi mitatu.

  Uamuzi huo wa kumfungulia Mkuchika ambao utawezesha jina lake kuripotiwa kwa uhuru katika vyombo vyote vya habari, ulifikiwa jana wakati wa kikao maalum cha wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari waliokutana katika hoteli ya New Africa, jijini Dar es Salaam.

  Mkuchika alifungiwa mwishoni mwa mwaka jana, kutokana na hatua yake ya kuamua kulifunga kwa miezi mitatu, gazeti la kila wiki la MwanaHALISI akilituhumu kuandika habari zenye mwelekeo wa kichochezi.

  Mbali ya kutangaza uamuzi huo wa kumfunguliwa Mkuchika, jukwaa hilo la wahariri lilieleza kusikitishwa kwake na uamuzi uliochukuliwa na Kituo cha Televisheni cha ITV ambacho ni mwanachama wake kuanza kuripoti taarifa zinazomhusu Mkuchika wakati waziri huyo akiwa bado kifungoni.

  Akizungumza wakati wa kikao hicho, mwenyekiti wa jukwaa hilo, Sakina Datoo, alisema katika uamuzi wao waliofikia mwaka jana, ilikubalika kwamba hatua yoyote kuhusu uamuzi wa kuendelea kumfungia au kumfungulia waziri huyo ilipaswa itokane na uamuzi wa kikao cha pamoja cha wahariri na si wa chombo kimoja kimoja kama ilivyofanya ITV na kisha kufuatiwa na vyombo vingine vya habari.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti kabla ya kufikiwa kwa azimio hilo la kumuondolea Mkuchika zuio la habari zake kuandikwa, wahariri walisema wanaamini kuwa, adhabu waliyompa waziri huyo ilimuathiri kwa kiwango kikubwa.

  “Adhabu hii tuliyompa waziri huyu kwa kipindi hicho ni tosha na bila shaka imemuumiza vya kutosha. Kauli kadhaa alizotoa kupitia vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali, zinaweza kuthibitisha namna alivyokuwa akiumizwa na hatua hiyo ya wahariri, pamoja na kuonekana akijigamba kwamba alikuwa hajatetereka,” alisema Jesse Kwayu, Mhariri Mtendaji wa gazeti la kila siku la Nipashe.

  Pamoja na kutangaza kumfungulia, jukwaa hilo la wahariri lilisisitiza uamuzi wake wa kuipinga Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976 ambayo inampa waziri mwenye dhamana ya habari kukifungia chombo chochote cha habari kuwa ni ya kikandamizaji na inayopaswa kufutwa haraka.

  Akizungumza katika mkutano huo, Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, Absalom Kibanda alisema hatua ya ITV kukiuka azimio la jukwaa la wahariri kikiwa ni chombo kinachomilikiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Reginald Mengi, ni cha kushtusha.

  Kibanda alisema yeye alikuwa akiamini kwamba, uamuzi wa ITV kutangaza habari za Mkuchika sambamba na hatua ya Mengi au MOAT kutotoa tamko la kuomba radhi au kuonyesha kuguswa na jambo hilo, inadhihirisha kwamba, mmiliki huyo anakubaliana na uamuzi wa kituo chake cha ITV wa kulipuuza Jukwaa la Wahariri.

  “Nilipokuwa nikija katika kikao hiki leo, nilikuwa nikikusudia kuliomba Jukwaa la Wahariri kutangaza mgogoro wa kikazi dhidi ya ITV na Mwenyekiti wa MOAT, Mzee Reginald Mengi hasa kwa kutambua kwamba, akiwa kiongozi wa wamiliki wa vyombo vya habari alipaswa kuheshimu maamuzi yote ya jukwaa kama walivyoahidi mwaka jana,” alisema Kibanda.

  Msimamo huo wa Kibanda ulisababisha kuibuka kwa mjadala mkali kuhusu suala hilo ambalo lilihitimishwa kwa wahariri kukubaliana kumuandikia barua ya karipio, Mtendaji Mkuu wa ITV, Joyce Mhaville, na si Mengi au MOAT, kwa maelezo kwamba makosa ya kihabari hayakufanywa na mmiliki au taasisi yao.

  Awali akichangia mada hiyo, Mhariri Mtendaji wa New Habari House inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Rai na The African, Muhingo Rweyemamu, alisema, kitendo cha baadhi ya vyombo vya habari kukiuka maamuzi ya Jukwaa la Wahariri kinaweza kusababisha baadhi ya watu kupoteza imani kwa taasisi hiyo ya wanahabari.

  Kwa upande wake, Mhariri Mtendaji wa gazeti la MwanaHALISI, Saed Kubenea, alisema hatua ya ITV kukiuka maagizo ya Jukwaa la Wahariri imewaweka wahariri wote katika hatua ngumu kiutendaji na ambayo inaweza kusababisha likapoteza heshima mbele ya jamii.

  Mbali ya hilo, Kubenea alisema wakati umefika kwa Jukwaa la Wahariri kujijengea uwezo wa kiuchumi ili kuondoa dhana potofu inayojengwa na baadhi ya watu wasiolitakia mema kwamba, linaendeshwa kwa matakwa ya mtu au kikundi fulani cha watu.

  Kwayu pamoja na kuunga mkono hoja ya kutoa karipio kwa ITV, alisema Jukwaa la Wahariri lilikuwa halina sababu wala ushahidi wa moja kwa moja ambao ungeweza kumhusisha mmiliki wa kituo hicho na taarifa waliyoiripoti.

  Likizungumzia hatua ya kuibuka kwa magazeti yanayoandika habari za kuchafua watu, Jukwaa la Wahariri liliwataka wahariri na wamiliki wa magazeti yote nchini kuhakikisha wanaheshimu msingi na maadili ya uandishi wa habari.

  Pamoja na kukemea kuibuka kwa tabia ya kuandika habari zinazohusu maisha binafsi ya watu pasipo kuzingatia maadili ya uandishi wa habari, jukwaa lilipinga hatua yoyote ya kuyafungia magazeti, likisema kutetea hatua hiyo ni kukiuka na kuingilia uhuru wa kupata habari.

  Akichangia hoja hiyo Rweyemamu alisema ni jambo la kusikitisha kwamba, baadhi ya watu wanaokabiliwa na tuhuma nzito zilizowafikisha katika hatua ngumu, wamefikia hatua ya kutaka kutumia taaluma ya uandishi wa habari kwa kuanzisha magazeti ili kupambana na wale wanaoamini kuwa ni mahasimu wao.


  Source: Tanzania Daima.
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mimi sidhani kama hiyo adhabu aliyopewa Mkuchika ilimuuma, kwa kuwa kwanza hajaonyesha dalili za kujutia uamuzi wake uliopelekea jukuwaa hilo kumdindia kuandika habari zinazomhusu! Huyu alikuwa apewe adhabu nyingine ambayo ingemfaa na ikamfanya ajutie uamuzi wake! e.g kumshinikiza ajiuzulu kwa kutumia mbinu mbalimbali!
   
 3. beth

  beth JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2017
  Joined: Aug 19, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 1,008
  Trophy Points: 180
  Ndugu George Mkuchika.. Kiongozi mwenye maamuzi tata na haiba ya jazba... Aliwahi kuingia kwenye mgogoro na TEF kiasi cha kufungiwa habari zake (kama RC Makonda) lakini IPP Media ikamkingia kifua na kukiuka makubaliano ya TEF.

  Mshale wa saa umetembea, kweli dunia duara!

  Leo Rais Magufuli ameona ni vyema Mkuchika akarudi kuiongoza Wizara ya Utumishi na Utawala Bora. Analenga matokeo gani kwa mwenendo wa nchi?!

  Muda utaamua!
   
Loading...