Mkubwa Fella:Juma Nature amekosa kampani yangu ndio maana ‘anafeli’

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,692
2,000
FELA.jpg

Mkurugenzi wa Yamoto Band na TMK Wanaume Family, Mkubwa Fella amedai Juma Nature anashindwa kufanya vizuri kwenye muziki kutokana na kukosa huduma yake.

Meneja huyo amedai yeye alikuwa anajua njia za kupita kumpromote muimbaji huyo na kuhakikisha kazi zake zinafika kwa wananchi.

“Juma Nature muziki wake haujapungukiwa chochote, yule kapungukiwa kampani yangu. Kwa sababu alichokuwa anafanya ni kile kile, ila kwa sasa amekosa kampani yangu,” alisema Mkubwa Fella. “Mimi naweza kuongea na mwenye redio vizuri, mimi naweza kuongeza na Dj vizuri. Juma Nature anaimba vizuri pia ni mtunzi mzuri kwahiyo mimi nachoweza kusema kwa Nature ni hilo,”

Fella alisema yupo tayari kufanya tena kazi na Juma Nature lakini Nature ameonekana kutokuwa tayari kufanya tena kazi na meneja wake huyo wa zamani.

Nyimbo nyingi za Juma Nature za hivi karibuni zimeshindwa kufanya vizuri.

Chanzo: Bongo5
 
kalagabaho

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,184

Nature ndio kamuingiza fela kwenye mziki ..fela kama añaona anaweza kufanya kitu na nature ni bora wakayazungumza kiutu uzima kuliko kupayuka payuka ..huko ni kumkosea adabu mtu aliyemuonyesha njia
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom