,Sasa ndio mnavuka mipaka ,mbona ukisuka mnyoosho,vitunguu unapendeza tu na misuko kibao ya kulusha loho ,ila hii ya kujizimua naiona imekalia sivyo.
Kuna siku nilienda mbio ,bado nilikuwa sijajua kama wanawake wanajigeuza rangi na nywele ,natokea dukani nyakati za jioni jioni kiza kimeanza kutanda na ubaridi wa kuleta mvua ukipepea ,mbele kwa mbali nikaona mwananmke anakuja face to face nikamtupia macho aloo ni mweupe halafu inaonekana amependeza kweli huwezi kuamini nilivyohisi ndani ya moyo lakini sio weupe niliouzoea ,kishindo alipofika karibu tutapishana nikatupa macho kwenye miguu ni meusi kunguru kasingiziwa ,sasa kwa jinsi mawazo ya mtu yanavyokwenda mbio katika kufikiri ikanipiga kwenye akili kuwa ni shetani ,na jioni hii na kaupepo haka huyu ndie tu shetani ,nilienda mbio kwa speed ya ajabu nikiruka matuta ya mihogo hadi palipo na mkusanyiko wa rafiki na vijana wenzangu ,nikawamegea ile stori wakaniambia usipende kutembea tembea sehemu zile ile hawajamaliza kusema yule mdada anarudi ,nikawasitua ,jama kile kiumbe naona kinajia huku ,na ndio chenyewe ,kwa kweli wakashtuka na kwa vile tupo wengi tukajikaza lakini kila mtu amekaa mkao wa standby go ,mimacho tumeitoa hakuna anepwesa ili asije akakosa kuona ,mara mwenzetu mmoja akaruka ,na nyinyi mbona mnataka kuzinguana ,huyu si flani huyu ametoka mjini alikuwepo huko kwa muda ,akiongea kwa sauti ya chini na alipokaribia alitusalimia ,ila nilijificha kiana ,hapo nikahoji ndipo nilipofahamishwa kuwa kuwa ndio mtindo mkuu umeingia.
Nikauliza mbona miguuni hakujibadilisha ,jawabu nililojibiwa niliridhika nalo ...eti kasahau !
Hawaeleweki kabisa wanataka nini ,hivi ndio urembo wa kumvutia mtu,mtu anavutiwa na wewe kwa sababu umweupe kama ungekuwa mweusi kama kolosho ilioungua hakutaki...mimi mweusi lakini mademu wengi huwa hawatoki kwangu sema nimetulia tu, na wala haijanijia hamu labda niseme weusi wangu utanikosesha wanawake wazuri ,haipo kwenye akili kabisa ,.
Tumebakiza mida kdogo tu Tz itakosa wanawake weusi ?
Urembo kwa mwanamke ni sawa lakini si kwa kuaribu ngozi na kuwa kama kitimoto au Avatar blue si wa blue kijani si kijani haujulikani rangi ya pink au njano!! Kama unataka Urembo lala kwa wakati atlst masaa 8 kwa siku,kula matunda,kunywa maji ya kutosha,fanya mazoezi ya kutembea kwa nusu saa kila siku,usitembee kwenye jua kali(kama ikibidi tumia mwamvuli),Usiwe unatumika kila siku kwa ligwaride 2 per week yatosha,ukifanya hayo mbona ngozi inakuwa soft kama ya mtoto mchanga,mie napenda demu soft natural color ,chotara usoni no pimples mweusi mng'avu ng'avu maji ya kunde kaenda hewani sekunde!!
Basi karibu watamalizika ni muda tu ,usizani natania ,hii kitu sasa inavua mipaka,mle bungeni kabakia Tibaijuka tu ,ila wale wengine ni sheeedah na balaa ,tatizo huwa wanashindanaga nani zaidi ,mwisho watabaki nyama tupu !yaani waschana wote uliokutana nao Masharik, magharibi, kas na kus wote wametumia mkorogo hakuna hata mmoja mwenye natural colour? Uko mji gani mkuu? Hata huku kwetu wapo ila si wote
Kila mtu na taste yake....
kwangu mwanamke akishakuwa wa kujikwatua sura na uasili wake, baaas...!
Uso una sura yake, mikono na miguu ina rangi yake...aaaah!
Sasa kujikoboa ndio msamiati gani tena,yaani kumbe hata wenyewe kwa wenyewe mnachimbiana ,nikiwa Raisi nitatangaza kuwa hali hii ni Janga la Taifa.atakejizimua tutamchuna ngozi.Hakuna kitu najivunia kama weusi wa ngozi yangu na kamwe sitakaaa nikajikoboa
Hahaha mshenga skuiz tunapiga deki mwili mzima hutojua...hatujichubui tena tunaita kujing'arisha😉
Tatizo la mikorogo unabidi uwe unapaka kila siku hili ubakie hivyo hivyo mweupe siku vikidunda au ukiacha unakuwa kama papai kijani si kijani njano si njano mweusi si mweusi yani sura inakuwa na rangi zaidi ya tatu yani ni shiiidddddddaaaaa!
Sasa kujikoboa ndio msamiati gani tena,yaani kumbe hata wenyewe kwa wenyewe mnachimbiana ,nikiwa Raisi nitatangaza kuwa hali hii ni Janga la Taifa.atakejizimua tutamchuna ngozi.
Hakuna kitu najivunia kama weusi wa ngozi yangu na kamwe sitakaaa nikajikoboa
Tatizo la mikorogo unabidi uwe unapaka kila siku hili ubakie hivyo hivyo mweupe siku vikidunda au ukiacha unakuwa kama papai kijani si kijani njano si njano mweusi si mweusi yani sura inakuwa na rangi zaidi ya tatu yani ni shiiidddddddaaaaa!
Mwanamke urembo babu natural iachie misitu....
Hongera...mi ntaendelea kujikoboa mpaka ngozi iseme 'yatosha'
Yep ,hii inakaribia kutupotezea rangi ya asili ya jamii yetu ,hivi huupendi weusi wako ? Hivi unajitia mapodozi ya kubleach ili iweje ?
Nimezunguka mashariki kaskazini,mangaribi na kusini ,mademu kila unaemuona amebadilika sura ,mzungu si mmzungu mhindi si mhindi alimuradi ,nilishughulika kuona maajabu mjini si kawaida tena kumuona mwanamuke mweusi.kimezidi nini ,kwenye madisco ndio usiseme ,kwenye mikutano hata wabunge ni weupe ,nikajisemea hivi kumbe tuna waarabu au hawa wamechanganya na wazungu ,mradi ilikuwa kizaazaa ndani ya roho yangu ,niliwaona siwo nilipowasogelea karibu ni kama mahindi ya kuchoma yale machanga .
Yote tisala kumi nywele, siku hizi hakuna tena anetumia shanuo kweli uwongo ? Jawabu nafikiri mnalo ,utaona demu anazungusha kichwa kwa gafula ukichunguza kumbe anaweka nywele sawa ,aloo waliniwacha hoi kabisa ,kila unaemuona ,nimetafuta walio na natural zile za shanuo ,nilipata shida ,ila hadi leo sijawafahamu yanini yote haya ? Najisemea labda ndio wanaona ndio uzuri !
Nyie ndo mnafanya wadada wahahe na mikorogo....kwamfano wew ushasema ni mweusi ukipata demu mweusi tena utakubali???