Mkopo wa milioni 10

Mkopo wa milioni 10

Naleta swali la ndugu yangu ambaye ni
mwajiriwa miezi miwili sasa! mshahara wake ni
laki sita na hamsini na ushee hela za kitanzania!
anataka kuomba mkopo wa milioni 10 benki
yoyote japokuwa mshahara wake unapitia
NMB,kama nilivyosema ana miezi miwili tu
kwenye utumishi! je anaweza kupata kiasi hicho
cha pesa kwa haraka? riba yake ni kiasi gani na
kama si benki ni wapi anaweza kupata mkopo
huo kwa riba nafuu? Lengo la mkopo ni kununua
gari! Nawasilisha

Wasikuzingue hao watu wanaokosoa Mipango yako ya pesa..

kila mtu anayo vipaumbele vyake kwenye maisha..

wakati wengine wanataka pesa kwa ajili ya mahari, wengine wanataka pesa za kufanya biashara, kujenga, Kulisha familia n.k.

ili kutimiza masharti, nafikiri kwa taasisi ya fedha isiyoumiza kwa makato( siyo makanjanja) watahitaji salary slips, barua ya ajira na dhamana ya mwajiri kwa kujaza fomu ya taasisi husika.

ukivipata hivyo vitu mkopo unao ila bado una gap ya miezi kadhaa kwa sababu salary slips hazifiki haraka.

Pesa ukipata ni yako mtu asikupangie matumizi tumia ulivyodhamiria.
 
unaelewa maana ya liabilities?
Hahahahaha kila mtu ana jifanya ana jua maana ya finance ndo maana Gari lina weza kuwa asset au liability inategemea unafanyia nini lakini haja sema hapo hilo Gari ana mpango nalo gani. Tatizo watu bado tunayo ile dhana ya watu wa kale kwamba Gari sio muhimu bado hamjui kazi ya mtu husika na mishe zake
 
Huyo mwambie asubiri mpaka apate comfirmation letter i.e apate utambulisho rasmi kuwa ni mwajiriwa wa serikali. Nafikiri ni baada ya miaka miwili kwa permanent government employement.
Hata hivyo sizani kama anaweza kupata kiasi hicho chote.
Pia kuchukua mkopo kwajili ya kununua gari ni ulimbukeni usio na maana. Mwambie asikubari kuendekeza utumwa, huo mshahara ni mdogo sana kama ataendekeza mikopo isiyo na tija maisha mazuri atayasikia kwenye radio na kuyashudia kwa majirani.
Confirmation ni mwaka mmoja, huenda taasisi chache hutumia hiyo miaka miwili
 
yaaaani wabongo ni watu EGNSEAW SANA mtu anatka mkop wa gari afu wabongo wanataka kumpangia matumizi mengine, kila mtu na matumizi yake maana hakuna anaye msaidia mtu kulipa ilo deni.
 
Akanunue tu gari akale Hilo gari na atalala kwenye gari hilo nyambafuuu
 
Akanunue tu gari akale Hilo gari na atalala kwenye gari hilo nyambafuuu
Wewe unajua hilo Gari anataka kufanyia nini? Au ndo kama kawaida ya wabongo kuhukumu pasipo kujua chanzo na sababu za mtu. Kasema anataka 10M akanunue Gari yeye ni mtu mzima anajua kwanini anataka hilo Gari pia tuache kujudge mawazo ya watu

Sent from my SNE-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Akanunue tu gari akale Hilo gari na atalala kwenye gari hilo nyambafuuu
Hivyo vingine vyote unavyoviwaza tayari anavyo, si wote wanaanza maisha kama ulivyoanza wewe punguza panic
 
Watanzania wengi ni vichaaa na wamechanganyikiwa, Mtu anataka 10M ili anunue gari so utaona hiyo ni mipango binafsi wala hajaja kuomba ushauri wa mtu mwingine yoyote.

Unachotakiwa ni kumpa guideline ya namna ya kuzipata hizo fedha, wala sio ushauri nasaha. Pia haya mawazo ya kipuuzi kuwa gari sio muhimu hebu tuache.
 
Naleta swali la ndugu yangu ambaye ni
mwajiriwa miezi miwili sasa! mshahara wake ni
laki sita na hamsini na ushee hela za kitanzania!
anataka kuomba mkopo wa milioni 10 benki
yoyote japokuwa mshahara wake unapitia
NMB,kama nilivyosema ana miezi miwili tu
kwenye utumishi! je anaweza kupata kiasi hicho
cha pesa kwa haraka? riba yake ni kiasi gani na
kama si benki ni wapi anaweza kupata mkopo
huo kwa riba nafuu? Lengo la mkopo ni kununua
gari! Nawasilisha
Huyo ndugu yako ni WEWE hapo kumbe

Sent from my M2101K6G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom