Mkopo wa fedha.

Nahitaji msaada wako ila namba niko tayari kuku PM sio kuweka hadharani.
 
Pole sana ndugu...bahati mbaya sipo karibu...ila ningekukopesha na ungenirejeshea pasi riba yoyote. Nakuombea kila la kheri.
 
Weka namba adharani watu wakuchabgie kidogo kidogo walichonacho...!ata nami ningekutupia kidogo..lakini umekuwa mbishi..unakazania PM tuuh.
 
mkuu iyoka samahani kwa hukumu ya kuhisi ladha ya UMASIKINI JEURI katika majibu yako. najihakikishia hauba shida husika, wadau tumeona njia mbadala ya kusaidia lakini huiweki hadharani badala yake umechagua kufa na tai shingoni. kila la heri. pm siendi-kwanza zinasumbua kwasasa
 
....dah,mkuu shida yako ilisound urgent sana,na hii ni wiki ya 3 sasa bado unaomba msaada/mkopo
..cha ajabu,imekuchukua takribani wiki mbili kuweka namba hadharani ili wadau walioguswa tukuchangie kwa tutakachojaaliwa badala ya kukopa,tena kwa riba
......shida nini,watu wakihisi unataka kuwapiga cheusi chekundu utaona wamekuonea!?
 
Wewe ni mchawi mbobezi,au ndio wewe ulikuja PM na kutaka kunitapeli TV kisa nina shida.

Nimetoa maelezo ya kutosha kuanzia post ya kwanza hadi majibu kulingana na maswali.

Nimeandika hapo kuwa dhamana ni vyeti vyangu kuanzia O level hadi Chuo kikuu,nilikuwa tayari kulipa kwa riba sio kupewa bure.

Namba ya simu nimeondoa kulingana na maneno yako,pia namba ya simu sio lazima kila mmoja aione ndiomaana kuna option ya PM.

Cheka sana omba yasikukute.
 
Nakupa tsh.200,000/= LEO LEO hiyo tar 31 unanipa tsh.300,000/= ila nachukua tv kama collateral mpaka hyo tar. 31......sitaki vyeti..... Nipo Ubungo
 
Nakupa tsh.200,000/= LEO LEO hiyo tar 31 unanipa tsh.300,000/= ila nachukua tv kama collateral mpaka hyo tar. 31......sitaki vyeti..... Nipo Ubungo
Nalifanyia kazi,ujumbe nimeupata.
 
....salaaalee..,nishakuwa 'mchawi mbobezi' na nimejaribu kukutapeli TV tena!??
...maadamu umereact badala ya kurespond,nimechagua kukupuuza!
.naona una shida zaidi kichwani kuliko hii ya fedha!
 
Mhi! Ila kweli tusimdhihaki, me ningua nayo ningekusaidia ila ndo hivyo sina, kwani najua maumivu uliyonayo me ilishanitokea mtoto akiumwa na ilikuwa yahitajika Milion moja laki mbili, nilihangaika kila mahali sikupata msaada na ndugu walinitenga mpaka nikaweka rehani shamba langu ila namshukuru Mungu nimemalizia kulipa deni mwezi wa kumi. Riba ilikuwa laki tatu
 
....salaaalee..,nishakuwa 'mchawi mbobezi' na nimejaribu kukutapeli TV tena!??
...maadamu umereact badala ya kurespond,nimechagua kukupuuza!
.naona una shida zaidi kichwani kuliko hii ya fedha!
Namimi nimekupuuza kulingana na maneno yako ya kuingiza mambo ya utapeli kwenye shida yangu,acha kuandika ujinga kwenye post yangu ipo siku utapatwa na shida.

Eti utapeli wakati nahitaji pesa kwa dhamana,umeniudhi mno,pia inawezekana ni mtu mwenye njaa ila hapa unaamua kujiweka kama hujawahi kupatwa na shida.
 
Pole sana mkuu,yaani shida isikie kwa jirani.
 
....teh hee hee..,umefika chuo ila matumizi ya alama ya kuuliza,tena humbly yamekushinda!..,hilo si kosa langu,au sio!
...na kwa kumbukumbu tu ujione ulivyo mjinga,nilikuwa mtu wa pili kuwa positive kwenye huu uzi wako,na mtu wa kwanza kukuombea msaada kwa mtu nilieamini anaweza kukusaidia kwa haraka!..angalia post ya 5 ya huu uzi wako..
..next time jifunze kutuliza akili kabla ya kujibu tu dogo!
.hasira hasara!
 
Una uhakika mimi ni dogo kwako?
Soma post ya 47 kwa umakini ulichoandika,mimi nimeomba mkopo sio msaada,wewe unaleta mambo ya utapeli.

Acha ujinga,ndio nimefika chuo ila suala la shida halikuwa kwenye bajeti ila tulikubaliana kuchanga kama familia ili mgonjwa asafiri hadi Muhimbili.
 
Wewe huna akili kweli,mimi niliomba mkopo wa 200,000 na kurudisha 280,000 kwa miezi miwili,yaani tangu nilipoomba hadi tarehe 31 mwezi wa kwanza.

Yeye anataka kunipa 200,000 nirudishe 300,000 kwa mwezi mmoja.

Nimemjibu kwa lugha nzuri ila siwezi,mimi nilihitaji kwa miezi miwili na riba ya 80,000 sio 100,000 kwa mwezi mmoja.

Acha kujitapa hapa ipo siku nawewe utapata shida.
 
Una uhakika sijatafuta wateja kama hujui shida kaa kimya,unaweza kutafuta mteja na usipate mtu anakuja anakuambia nimuuzie TV na Radio kwa 200,000 wakati vyote vina thamani ya 700,000 sasa sijui utauza au unaamua kutafuta njia nyingine.

Wewe na ujinga wako unabadili lengo la post,mimi nilihitaji mkopo wa riba,sio kupewa bure,hakuna cha bure chini ya jua.

Endelea kuandika eti sina mgonjwa na tapeli ila tambua tayari yupo Dar kwa ajili ya matibabu.

Sichagui vya kujibu ili naona unaandika pumba tu na kujitapa kama huwezi kupata shida.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…