Mkopo wa Benki Bila "10%" upo?

Mkopo wa Benki Bila "10%" upo?

Kwa uzoefu wangu, ni vigumu kupata mkopo bila kutoa rushwa hata kama vielelezo vyako vimekamili.

Mimi mteja ktk bank za CRBD, ABC, Access, EFC, na NBC! Na nimechukua mikopo hupo mara kadhaa! Lakini ukienda kwa unyoofu, mkopo utachkua muda mrefu, tena hutapewa kiasi ukitakacho. Ila ukitoa kitu kidogo (TKK) ukicheleweshwa ni siku 3 tu tangu umeomba mkopo!

Ndio maana nawashangaa sana maofisa mikopo wa benki nyingi, mishahara yao midogo, lakini wanafanya mambo makubwa, ambayo hayalingani na vipato vyao.

Kuna maafisa katika Benki moja ya Biasha tawi la Tegeta, ambao hawezi kutoa mkopo hadi umekubaliana nao utawakatia kiasi gani! Hata mtu anayekopa kiasi kidogo tu lazima aombwe TKK, la sivyo hapati!

Jamani wahusika tusaidieni!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

kwanini msiende kukopa amana bank, benki ya waislam? kule natumaini hakuna rushwa wala riba!
CC: Ritz, FaizaFoxy, kahtaan Kikwajuni One
 
Last edited by a moderator:
Kwa uzoefu wangu, ni vigumu kupata mkopo bila kutoa rushwa hata kama vielelezo vyako vimekamili.

Mimi mteja ktk bank za CRBD, ABC, Access, EFC, na NBC! Na nimechukua mikopo hupo mara kadhaa! Lakini ukienda kwa unyoofu, mkopo utachkua muda mrefu, tena hutapewa kiasi ukitakacho. Ila ukitoa kitu kidogo (TKK) ukicheleweshwa ni siku 3 tu tangu umeomba mkopo!

Ndio maana nawashangaa sana maofisa mikopo wa benki nyingi, mishahara yao midogo, lakini wanafanya mambo makubwa, ambayo hayalingani na vipato vyao.

Kuna maafisa katika Benki moja ya Biasha tawi la Tegeta, ambao hawezi kutoa mkopo hadi umekubaliana nao utawakatia kiasi gani! Hata mtu anayekopa kiasi kidogo tu lazima aombwe TKK, la sivyo hapati!

Jamani wahusika tusaidieni!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
Taja jina la benki na muhusika, otherwise unajaza server bure.
Wewe ndo mlengwa usipothubutu nani atathubutu ambae hajakutwa na hali hiyo? Tubadilike
 
Kule mpaka usilimu kwanza!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

unasilimu ukishapata mpunga wako unarudi ulikokuwa! au unaogopa kuhukumiwa kifo?lakini cha ajabu nilikutana na muislamu aliyekuwa anahangaika kutafuta mkopo usio na riba na nikamuuliza kwa nini asiende amana bank akesema haijui!
 
Mii hapa ofisini kwetu Banks zinapishana kuja kuomba kuwapa wafanyakazi mikopo, NMB washakuja, wakasepa! CRDB wameleta na kibanda chao, wameeka kambi hapa hapa ofisini, Manager wa TPB branch ya ......., ananiomba niwashawishi wafanyakazi wenzangu tukachukue mikopo ktk tawi lake,! Napata tabu kujua ktk mazingira haya, nitatoaje rushwa kama nitauhitaji huu mkopo!
 
Taja jina la benki na muhusika, otherwise unajaza server bure.
Wewe ndo mlengwa usipothubutu nani atathubutu ambae hajakutwa na hali hiyo? Tubadilike

Kule juu kuna mtu kamtaja: wanasema anaitwa "jamaa" na bank pia wameitaja, wanasema ni AKIBA, wameenda mbali zaidi, wamesema ndio tabia yake!
 
Kweli kuna maafisa mikopo wengine mpka wana kupa mchongo ukope ili umkatie chake kwangu wali umia nimechukua mkopo wa ml 10 kuja nikampa lak akadai wako wengi nikamwambi bac niwachie huo mkopo wote watalipa wenye akurudia tena.
 
Mii hapa ofisini kwetu Banks zinapishana kuja kuomba kuwapa wafanyakazi mikopo, NMB washakuja, wakasepa! CRDB wameleta na kibanda chao, wameeka kambi hapa hapa ofisini, Manager wa TPB branch ya ......., ananiomba niwashawishi wafanyakazi wenzangu tukachukue mikopo ktk tawi lake,! Napata tabu kujua ktk mazingira haya, nitatoaje rushwa kama nitauhitaji huu mkopo!

Wewe ni mfanyakazi, na umesema vema kuwa unatafutwa ukakope, wakati huna sababu ya kukopa. Ila siku utakayo hitaki kukopa, na watu wa "promotion" hawapo, utaelewa vizuru. Pili mikopo ya biashara hasa ndiyo yenye utata zaidi, kwa mtazamo wangu!

Back
Top Bottom