TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwafahamisha waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwa imetoa orodha ya Awamu ya Tatu yenye jumla ya waombaji wa mwaka wa kwanza6,915waliopangiwa mikopo.
Kati ya waombaji hawa waliopangiwa mikopo, waombaji4,642ni wale wanaojiunga na shahada ya kwanza katika vyuo mbalimbali nchini na waombaji2,273ni wanafunzi wanaojiunga na Stashahada (Diploma) ya Ualimu wa masomo ya sayansi na hisabati katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Kwa msingi huo, Bodi inapenda kuufahamisha umma kuwa hadi sasa imekwishawapangia mikopo jumla ya waombaji mikopo wenye sifa47,751wa mwaka wa kwanza. Katika awamu ya kwanza, Bodi ilitoa orodha yenye jumla ya waombaji12,282; Awamu ya Pili wanafunzi28,554na Awamu hii ya Tatu wanafunzi6,915wamepangiwa mikopo.
Majina yote ya waombaji waliofanikiwa kupangiwa mikopo kutoka katika awamu zote tatu yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi waolas.heslb.go.tzna tovuti ya Bodi (
Higher Education Students' Loans Board -HESLB). Aidha, orodha hizo pia zimetumwa vyuoni kwa ajili ya taratibu za usajili.
Mwisho.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Novemba 13, 2015