Mkoloni wetu CCM anaaga dunia

Mkoloni wetu CCM anaaga dunia

Status
Not open for further replies.

Rev. Mtikila

R I P
Joined
Dec 1, 2008
Posts
3
Reaction score
34
Wana Jamii Jana nilifanya mkutano na waandishi nimeona niwapatie ujumbe mzito juu ya hatima ya nchi hii.
Rev C Mtikila

MKOLONI WETU CCM AIAGA DUNIA!
WAMESHINDWA KUMPATA MGOMBEA URAIS
(Fisadi John MAGUFULI hana sifa kabisa)

Kutokana na agizo la Mwenyezi Mungu katika Torati, hakuwezi kuwepo mgombea wa Urais, Ubunge wala Udiwani anayestahili katika CCM, genge ambalo ni utawala utokao kuzimu, ambao ni laana kwa Nchi! Mgombea wa CCM anaweza kupata kura ya mtu mwenye laana tu!

Katika miaka 54 ya ukoloni wao, CCM wameua kilimo kilichokuwa uti wa mgongo wa uchumi wa nchi yetu! Badala yake waliingilia kukomba raslimali zote za nchi, wakishirikiana na maharamia wa nje na ndani ya nchi, mpaka nchi yetu imemalizwa kiasi hiki!CCM wameua elimu ya watoto wetu na kufuta ajira nchini, ila watoto wao wanawasomesha nje ili waje warithi hatamu zao za ukoloni! CCM walivunja Ibara ya 27 ya Katiba ya Nchi kwa kumaliza kabisa mashirika ya Umma zaidi ya 430, mitambo ya thamani kubwa sana ya uzalishaji ikang'olewa na kuuzwa nje! Mashirika mengine ya Umma yakatiwa mifukoni, wakagawana mpaka na majumba ya Serikali! Saa ya ukombozi ni sasa!

CCM ni genge la ki-Mafia lililoifanya nchi yetu kuwa lango kuu la biashara ya madawa ya kulevya! CCM wamemaliza misitu yote mpaka nchi inageuka kuwa jangwa! CCM wamemaliza wanyamapori, kiasi kwamba katika tembo 358,000 tuliokabidhiwa na Mwingereza siku ya Uhuru wetu, leo wamesalia 7,300 tu ingawa walikuwa wanazaliana! Vifaru wamemalizwa kabisa! Chui nao wamemalizwa, na hata majoka
sasa hatunayo!

CCM wanategemea kushinda Uchaguzi Mkuu kwa goli la mkono, baada ya kupitisha mgombea urais asiye na sifa hata moja katika zile zilizoagizwa na Mungu katika Kumbukumbu la Torati, ambaye ni fisadi John Pombe Magufuli, ambaye sifa alizo nazo si za urais bali ni za kufungwa jela au kunyongwa hadharani katika nchi za wengine wanaozijali sana nchi zao.

Kwa mfano:

1. Fisadi John Pombe Magufuli ndiye haramia mkuu wa uporaji wa majumba yote ya Serikali, pamoja na fisadi Benjamin Mkapa, wakauziana na kugawiana yote! Fisadi Magufuli na wenzake wanakabiliwa na kiyama cha kuyarejesha majumba yote, na kulipa fidia ya hasara yote waliyolitia Taifa kwa muda wote tangu walipoyapora. Haramia wa kutisha kiasi hiki katika nchi za wwenzetu kama China hunyongwa hadharani! Saa ya ukombozi ni sasa!

2. Fisasdi John Pombe Magufuli katika ujambazi wake wa kopora majumba ya Serikali, alimhonga hawara yake aitwaye Kabula anayemwendeshea Kebby's Hotel iliyoko Mwenge majumba mawili ya Serikali, Plot No. MSM/201 na Plot MK/521.
Mawaziri Basil Mramba na Daniel Yona waliotumikia Taifa kwa muda mrefu sana kuliko Magufuli wamefungwa jela miaka mitatu, kwa kutumia nyadhifa zao kwa ufisadi, kwahiyo kumruhusu fisadi Magufuli kugombea urais badala ya kumtupa jela miaka 30 ni kukiuka Ibara ya 12 na 13 ya Katiba ya Nchi! Saa ya ukombozi ni sasa!

3. Kwa uharamia huu kuhusu majumba ya Serikali, fisadi Magufuli amesababisha Majaji, Makatibu Wakuu na watendaji waandamizi wa Serikali kuhifadhiwa katika mahoteli, na kuitia Serikali hasara ya zaidi ya shilingi Bilioni hamsini (Sh 50,000,000,000) kwa mwaka!
Katika nchi makini zinazojithamini, mafisadi John Magufuli na Benjamin Mkapa huwa ni wa kunyongwa hadharani. Kwahiyo kuruhusiwa kugombea urais fisadi John Pombe Magufuli badala ya kufikishwa mbele ya Sheria ni kumkufuru Mungu na kuichokoza hasira yake!

4. Fisadi Magufuli amelitia Taifa hasara ya kutisha katika uwaziri wake wa Ujenzi. Gharama za ujenzi wa barabara zinategemea upana wake, aina na kina cha usindiliaji wa udongo, na unene wa tabaka la lami. Katika ujenzi wa barabara zilizo nyingi fedha zimeibiwa kwa kupunguza upana wake, unene wa tabaka la lami na uimara wa kokoto. Magufuli hawezi kujificha nyuma ya TANROADS katika wizi huu wa kutisha, kwa ssbabu hakuna malipo yanayoweza kufanywa kabla ya yeye kujiridhisha na kuyabariki.

5. Ukame wa sifa za uongozi wa fisadi Mgufuli unaonekana hata alivyopata kuchepusha barabara katika kusalimisha majumba ya watu fulani anapobomoa ya wengine.

6. Ulemavu wa kimaadili na kifikra unaomnyima kabisa John Magufuli sifa ya uongozi hata wa kijiji ni kukosa tunda la kiasi na kutunza kisirani, kisasi na kukurupuka katika maamuzi, kama alivyobomoa kwa chuki kituo cha mafuta cha mtu, Mahakama ikaamuru alipwe mabilioni ya fedha na Serikali! Hivyo Magufuli ni wa kupelekwa Mahakamani kwa kutumia madaraka yake vibaya.

7. Ni kutokana na udhaifu wake wa chuki dhidi ya waziri mwenzake, ambapo aliweza kumkomoa kwa kuwafanyia ukatili wananchi wa Ziwa Victoria kuzuia chombo cha usafiri katika Ziwa kisipelekwe kwa barabara, lakini kikafikishwa kuhudumia wananchi kupitia Kenya.

8. Mapungufu ya Magufuli ya udhaifu mkubwa mno wa kifikra, unaomfanya akurupuke katika maamuzi, ulionekana hata alivyoifanyia ile meli ya uvuvi ya Wachina, akaitia hasara Serikali kwa mabilioni ya fedha na kuiletea aibu kubwa sana! CCM wamejionyesha kuwa watu wenye akili za ajabu sana kwa kukosa mtu wa kugombea urais wakabakiwa na Magufuli!

Kwa mujibu wa Katiba ya Nchi yetu Ibara 12, 13, 26 na 27 ni lazima fisadi John Pombe Magufuli afikishwe mbele ya Sheria kwa ajili ya hasara ya mamia ya mabilioni ya fedha ambayo John Pombe Magufuli amelitia Taifa, kwa Serikali kulipishwa fidia ya yeye kubomoa kwa chuki kituo cha mafuta cha mwananchi, serikali kulipishwa fidia ya uharamia alioifanyia meli ya uvuvi ya Kichina, wizi katika mikataba ya ujenzi wa barabara, mabilioni ya fedha ya kuhifadhi Majaji na watendaji waandamizi wa Taifa katika mahoteli kutokana na yeye na fisadi Mkapa kuuza majumba ya Serikali.

Basil Pesambili Mramba na Daniel Yona ni mawaziri waliolitumikia Taifa kwa muda mrefu sana, lakini sasa wamo gerezani wanatumikia kifungo cha miaka mitatu kwa kosa la kutumia vibaya dhamana waliyopewa na Taifa. Kwa madhambi aliyolifanyia Taifa huyu John Pombe Magufuli, anastahili kifungo cha maisha na ndiyo hukumu tunayokusudia kuitaka Mahakama impatilize, ingawa katika nchi za wenzetu angenyongwa hadharani. Saa ya ukombozi ni sasa!.

Baada ya Mkapa kuimaliza nchi yetu kwa kutokuwa na uchungu nayo kwa vile yeye si Mtanganyika, CCM wangemchunguza kwanza huyu Mnyambo aliyetoka Rwanda, kwa sababu Mwenyezi Mungu ametuagiza katika Torati kwamba tusimtawaze MGENI kuwa Rais.

MMWAGIKO WA DAMU UNAPIGA HODI NCHINI

Kwanza kabisa uzalendo na Utawala wa Sheria umepewa talaka katika Uchaguzi Mkuu wa safari hii! Wananchi wamenyimwa Haki ya msingi ya uraia ya kugombea Urais, Ubunge na Udiwani na hata uongozi wa vijiji na vitongoji, iliyoamriwa na Mahakama ya Afrika.

CCM wanauasi ukweli wa Mwenyezi Mungu, uliotetewa na Mahakama ya Bara la Afrika kwamba vipawa vya kuongoza nchi, kama uzalendo, maono na mzigo juu ya hatima ya nchi yetu na watu wetu, Mungu humpa mtu, havipi vikundi vya maslahi (vyama vya siasa). Kwahiyo Taifa linamkosa huyo anayefaa kama hapendi kujiunga na chama cha siasa. Hiki ni kitewndo kinachounyima uhalali uchaguzi mkuu wa safari hii.

Jambo la pili, wananchi wa mikoa mingi wamenyimwa kwa makusudi kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura! Kwahiyo wananchi walio wengi wanazuiwa kupiga kura, hivyo kwamba uchaguzi wa safari hii utakuwa batili kabisa! Nguzo kuu ya demokrasia imevunjwa, kwahiyo si uchaguzi bali ni uharamia wa kisiasa wa CCM. Yakizuka machafuko, moto utawaka nchini kote, kwani hata mjinga wa mwisho atauona uhalali wa kuteketezwa genge hili!.

Hata kama viongozi wa juu wa majeshi watakosa uzalendo wakakubali kuwalinda mafisadi wa CCM, historia inatufundisha kuwa sauti ya Mungu huwa na uzito zaidi katika mioyo ya binadamu kuliko kauli ya watawala dhalimu. CCM wameandaa jeshi la vijana wao kwa ajili ya mapambano ya kung'ang'ania madaraka, wakishakataliwa na wananchi katika uchaguzi. Kadhalika Chadema na CUF pia. Mmwagiko wa damu unapiga hodi nchini!

Hatari kubwa ipo katika CCM kushindwa katika Uchaguzi licha ya rafu zake zote, na kukataa kupisha utawala mpya. Chadema na CUF pia wanahofiwa kujipanga kwa rafu hiyo hiyo! Hii ndiyo hodi ya mito ya damu nchini. Njia pekee ya kuyakwepa maangamizi ni kushikamana Watanganyika wote nyuma ya DP, tuweze kuingia Kanani kwa amani.

Saa ya ukombozi ni sasa!

Mchungaji C. Mtikila
MWENYEKITI – TAIFA (DP)
 

Attachments

haaa haaa

Shikamoo Mchungaji .... kumbe na wewe umo humu lakini hauvumi

asante kwa makala yako nzuri
 
Hili chapisho sijui kama lilipendwa na watawala...
 
Lakini kwa hili la magufuri kasema kweli.!
 
Mchungaji katoa WOSIA wake. Mwenye kuukubali au kuukataa atajua yeye mwenyewe. Mungu ampe kheri ya milele kule aliko tangulia.
 
Bandiko zuri sana la Marehemu Mtikila, maneno ya shujaa, kinara wa mageuzi Tanzania. Asante baba Mtikila, uliotuacha tunaendeleza kazi yako la kumchinja mkoloni ccm na kumwondoa fisadi Magufuri. Pumzika kwa amani
 
Nilishangaa mwishowe akawa upande wa Magufuli!!!

Apumzike kwa amani amezimika kama mshumaa!!!

Duh!
Marehemu alikuwa napiga kotekote!

Hii mbona hamuijadili? au chungu?
Reverend alikuwa na staili yake ya kupiga mishare mwituni,then anatega..Maana baada ya kufyatua hili bomu lumumba walimfata wakampa gawio lake,wakamwambia ageuze fataki kuelekea ukawa..and yes,He did it! Anyway,Mungu amrehemu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom