chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 21,567
- 28,479
Habari wana-JF!!
Bado nipo mkoa wa Ruvuma hapa Songea na hawa rafiki zangu Wangoni waliojaa ukarimu wa hali ya Juu.
Baadhi ya mambo yanayowarudisha nyuma kimaendeleo ni ukosefu wa taarifa, nikimaanisha upashaji wa habari ni hafifu sana kwa huu mkoa wa Ruvuma sijajua hizi ni hila za CCM kuendelea kuukandamiza mkoa huu wasijitambue maana baadhi ya mikoa michache inayowaunga mkono CCCM kwa asilimia kubwa ni hawa ndugu zetu kutoka mkoa huu wa Ruvuma.
Radio ni chache hazizidi hata nne huku moja ikiwa ni ya mkoa huu na usikikaji wa vyombo hivi siyo mzuri kwa mawasiliano mara kwa mara yanapotea, na kuhusu magezati huku hayafiki kwa wakati na watu hawana hata muda wa kuyasoma.
Wana Ruvuma huu ni wakati wenu wa kuamka kutoka usingizini ili muanzishe vyombo vyenu vya kupashana habariza uhakika na mjue ni nini kinaendelea katika nchi yenu, CCM wamewashika masikio msikubali washike hadi akili zenu!
Nawasilisha,..