Mkoa wa Mara ulipewa jina hilo mwaka gani?

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,413
3,904
Naomba mwenye ufahamu huu anijuze. Ni mwaka gani mkoa huu ulipewa jina hili?

Natanguliza shukrani.
 
Mtafute Wasira a.k.a Tyson ila uwe mwanaume kweli jamaa hataki ujinga wa kuhojiana hojiana!
 
Jina linatokana na mto mkubwa mkoani humo unaitwa MTO MARA. Jina ilipewa baada ya Uhuru wakati musoma inakua makao makuu.

Niliambiwa na mzee mmoja hivi, alikua dereva makao makuu "Musoma" na baadae Bunda ofisi za wilaya. Ingawa sasa hivi ni mstaafu
 
Jina linatokana na mto mkubwa mkoani humo unaitwa MTO MARA

Asante kwa hiyo taarifa muhimu ila bado swali langu ni lini mkoa ulipewa jina hilo? Na kwa sababu ya jibu lako, naongeza swali, huo mto ulianza kuitwa hivyo lini?
 
Asante kwa hiyo taarifa muhimu ila bado swali langu ni lini mkoa ulipewa jina hilo? Na kwa sababu ya jibu lako, naongeza swali, huo mto ulianza kuitwa hivyo lini?
Mkoa uliitwa wakati Musoma inakua makao makuu ya mkoa, nadhani mwaka 1965-1967 maana source yangu hakuwa na kumbukumbu nzuri umri umeenda sana
 
Kuna faida kubwa sana kukaa na watumishi wastaafu wa Serikali, kuna vitu utaambiwa ambayo hakuna kitabu wala gazeti litaweza kusema
 
Kabla ya hapo uliitwa jina gani ?

Wakati wa ukoloni l
Mkoa huo ulikuwa ni sehemu ya Jimbo la Ziwa. Baada ya Uhuru Jimbo hilo liliiitws Mkoa wa Ziwa. Mwishoni mwa miaka ya 60 mkoa uligawanywa sehemu 2: Ziwa Mashariki na Ziwa Magharibi.
Baada ya Idi Amin mwishoni mwa miaka ya 70 kuvamia Kagera Salient na kusema lake Nyerere akaubadili jina Mkoa wa Ziwa Magharibi na kuitwa Mkoa wa Kagera na Ziwa Mashariki kuitwa Mkoa wa Mara.
Na hapo hapo kukamegwa Mkoa wa Mwanza
 
Ukitaka upate jipu zuri, ungeeleza kwanza ni nini kimekusukuma kutaka kujua
 
Wakati wa ukoloni l
Mkoa huo ulikuwa ni sehemu ya Jimbo la Ziwa. Baada ya Uhuru Jimbo hilo liliiitws Mkoa wa Ziwa. Mwishoni mwa miaka ya 60 mkoa uligawanywa sehemu 2: Ziwa Mashariki na Ziwa Magharibi.
Baada ya Idi Amin mwishoni mwa miaka ya 70 kuvamia Kagera Salient na kusema lake Nyerere akaubadili jina Mkoa wa Ziwa Magharibi na kuitwa Mkoa wa Kagera na Ziwa Mashariki kuitwa Mkoa wa Mara.
Na hapo hapo kukamegwa Mkoa wa Mwanza
It means mkoa wa mara ulikuwepo kabla ya mkoa wa Mwanza?
 
Wakati wa ukoloni l
Mkoa huo ulikuwa ni sehemu ya Jimbo la Ziwa. Baada ya Uhuru Jimbo hilo liliiitws Mkoa wa Ziwa. Mwishoni mwa miaka ya 60 mkoa uligawanywa sehemu 2: Ziwa Mashariki na Ziwa Magharibi.
Baada ya Idi Amin mwishoni mwa miaka ya 70 kuvamia Kagera Salient na kusema lake Nyerere akaubadili jina Mkoa wa Ziwa Magharibi na kuitwa Mkoa wa Kagera na Ziwa Mashariki kuitwa Mkoa wa Mara.
Na hapo hapo kukamegwa Mkoa wa Mwanza

Aha!! Nimekupata. Shukrani sana.
 
Kabla ya hapo uliitwa jina gani ?
Kabla ya hapo eneo lote hilo lilikuwa ni wilaya za jimbo la ziwa (lake province) wilaya moja makao yake yalikuwa tarime hii iliitwa north mara, na wilaya nyingine ya south mara makao yake yalikuwa Musoma mjini.hii ni kutia ndani na visiwa vya ukelewe na ukara.
 
Maana ya neno MARA kibiblia Ni UCHUNGU...kwa mfano wana Wa Israel walifika mahali wakanywa Maji machungu na hapo mahali pakaitwa MARA....na watu Wa mkoa huu Ni wenye mwelekeo huohuo....nawasilisha
 
Maana ya neno MARA kibiblia Ni UCHUNGU...kwa mfano wana Wa Israel walifika mahali wakanywa Maji machungu na hapo mahali pakaitwa MARA....na watu Wa mkoa huu Ni wenye mwelekeo huohuo....nawasilisha

Exodus 15:22-25. Kwa kuwa umesema hivyo ngoja niweke wazi. Nimekuwa natafakari mambo fulani kuhusu hiyo chapter kwa muda fulani sasa na nimekuwa najiuliza kama Mwalimu Nyerere aliupa mkoa huo jina hilo kutokana na chapter hii. Vilevile inaelezea Musa alipewa mti auweke katika maji ya Mara ili yame matamu.
 
Back
Top Bottom