Mkoa wa Kilimanjaro unavyouaibisha mkoa wa Dar e Salaam kitaaluma

Oct 7, 2019
51
156
Mkoa wa Kilimanjaro pekee una shule 66 za Advance yaani mara sita ya shule zote za Mkoa wa Mtwara na Geita ambayo mtwara inashika nafasi ya kwanza na Geita ya Tatu, Kilimanjro ina Shule za Advance zaidi ya mara nane ya shule zote Lindi na karibu mara tatu zaidi ya shule zote za Morogoro na mara Mbili zaidi ya shule zote za Tanga.

Mikoa yote niliyotaja imeipita Kilimanjaro kwenye swala la Ufaulu ila kwangu Kilimanjaro ndio mkoa bora kabisa kielimu mwaka huu. Kwa wingi wa shule zake Kilimanjaro angalau ilipaswa kushindanishwa tu na mkoa wa Daresalam japokuwa Daresalam nayo imezidiwa kwa shule Sita na Kilimanjaro.

Kilimanjaro pekee imetoa division One 1,023 wakati anayeshika nafasi ya kwanza akiwa na one 172, wa pili one 95 wa tatu one 233 wa nne one 433 na wa tano one 435. Unaweza ukaona hilo Gape ni kubwa kiasi Gani. Anayemfuatia angalau kwa mbali sana Kilimanjaro ni mkoa wa Daresalam wenye One 747.

Trend ndio hiyo hiyo kwa division two Kilimanjaro inaongoza kwa idadi ya waliopata Two ikifuatiwa na Mbeya huku Divison Three Kilimajaro ikipitwa kidogo sana na Mkoa wa Daresalam. Haya kwangu ndio madaraja ya Ufaulu achana na four na Ziro.

Nini cha kujifunza hapa.

Daresalam na Kiliamanjaro ilikuwa na karibu idadi sawa ya watahiniwa Kilimanjaro ikiwa na watahiniwa 7,707 huku ikifuatiwa na Daresalam ambao walikuwa watahiniwa 6,663.

Kwa wingi idadi hiyo ya watahiniwa wa Mkoa wa Kiliamanjaro na perfomance waliyoionyesha ni dhahiri kuna factor ya ziada ya shule nyingine kujifunza.

Kilimanjaro naishindanisha na Daresalam kwa kuwa kwanza zote zina karibu uwiano sawa wa shule na uwiano sawa wa watahiniwa lakini matokeo yao ni Ardhi na Mbingu.

Daresalam shule zake nyingi hazili chakula cha mchana huku kwa shule zote za Advance Mkoa wa Kilimanjaro na hata za msingi na O level zikipata mlo wa mchana. Hii ni facto ya kwanza Kubwa mno na haipaswi kudharauliwa kama tunavyofanya.

Shule karibia Zote za advance mkoa wa Kilimanjaro wanafunzi wake wanalala shuleni huku kwa mkoa wa Daresala ikiwa ni karibia nusu kwa nusu. Yaani nusu wanalala na nusu wanarudi nyumbani.

Kimazingira Daresalam ingepaswa kuwa juu ya Kilimanjaro kutokana na access ya mambo mengi waliyoanayo katika mkoa wao. Hawa wana kila kitu kasoro tu mambo mawili niliyotaja hapo juu chakula na Baadhi kulala nyumbani.

Kwa bahati mbaya sana swala la chakula mashuleni si kipaumbele chetu. Swala la Boarding ni mpaka msichana abakwe au apate mimba ndio tuanze kuhamasiashana kujenga bweni.

Unawezaje kumfundisha mwanafunzi mwenye njaa? Atajifunza au atawaza chipsi za Kwa mangi?

Unawezaje kumdhibiti mwanafunzi mara baada ya masomo? Naamini hawa wa Dar karibia wote wana smart phone hawa, wanajichamganya na sisi jioni, watasoma saa ngapi?

NILIWAHI KUSEMA
Mara nyingi viongozi wetu wamekuwa wakifanya mambo bila Tafiti. Nikitolea mfano viongoz wa mkoa Wa Daresalam kuwa wanachapa kazi sana lakini impact ya kazi zao haionekani sana kutokana na kutokufuata misingi ya tafiti kwanza.

Nilipinga ujenzi wa Ofisi kwanza kama kweli tulihitaji ufaulu wa haraka rafiki yangu Fredy Dotto Mauki alinipinga moja kwa moja kuwa swala la Ofisi za waalimu ni kipaumbele. Nikamwambia hakuna significant relationship kati ya Ofisi na matokeo ya mwanafunzi. Yaani hakuna uhusiano wa moja kwa moja, uhusiano uliopo ni mdogo sana.

Mwaka jana Daresalam haikuwa na Ofisi lakini ilikuwa ya 20 mwaka huu Ofisi zina mpaka kiyoyozi imekuwa ya 26. Hapa tuongee kitaalamu kumsaidia Mhe. Makonda apige hatua kubwa zaidi kwenye scandal hii ya Elimu katika mkoa wake inayomchafulia Taswira ya kazi zake.

Kama Daresalam wakigusa tu haya mambo mawili Chakula na Hostel hakika watatuletea tabu kubwa sana. Hawataki kusikia waache wakimbizane na Ofisi tu.

Zipo factor nyingine ila hizi ni za msingi kuliko yote.

Hongereni viongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro kuanzia mkuu wa mkoa hadi staff za waalimu. Mmetisha sana. Na hongereni pia wazazi kwa kuendelea kukataa siasa Mashuleni na kuamua kuwekez haswa kwenye Elimu.

Unaruhusiwa kubisha. Ngoja niingie class kufundisha tutakutana baadaye.
37056753_2111729535534939_667787510956425216_n.jpg
 
[Daresalam japokuwa Daresalam nayo imezidiwa kwa shule Sita na Kilimanjaro.



[/QUOTE]

Mwaka jana Daresalam haikuwa na Ofisi lakini ilikuwa ya 20 mwaka huu Ofisi zina mpaka kiyoyozi imekuwa ya 26. Hapa tuongee kitaalamu kumsaidia Mh #Makonda apige hatua kubwa zaidi kwenye scandal hii ya Elimu katika mkoa wake inayomchafulia Taswira ya kazi zake.

Kunenge
 
Asante kwa uchambuzi mahiri, unaonekana kweli mwalimu tena wa kiwango kizuri. Hongera kwa Kilimanjaro, nakumbuka hasa miaka ya hadi 1990 Kilimanjaro ilikuwa inaongoza kwa kila kitu kizuri; elimu, uchumi, maji safi, umeme, hospitali, n.k. Mwalimu Nyerere alifanya kosa moja kubwa katika maisha yake kuhusu Kilimanjaro na watu wake: badala ya kujifunza na kuendeleza mazuri ya Kilimanjaro, aliishia kuzuia ufaulu wa darasa la saba, baada ya kuona bado watu wa huko wanajenga shule binafsi, basi akataifisha mashule binafsi pamoja na yale ya mashirika ya dini kuwa mali ya serikali

Baada ya Mwalimu kuona uchumi wa Kilimanjaro unakuwa sana kupitia zao la kahawa lililosimamiwa kikamilifu na chama cha ushirika cha KNCU, mwalimu akafuta vyama vyote vya ushirika kwa madai ya ukabila mwaka 1977, lakini ghafla akagundua kuwa anakosea na mwaka 1978 akavirudisha.

Sishangai kwanini mwalimu alistaafu 1984 kwani alijua kwamba amekosea. Badala ya kuwavuta shati waliombele unatakiwa kujifunza kwaoNimeona Kilimanjaro ikiwa na shule za sekondari 325, Dar ilikuwa na shule 298. Ufaulu kwa ujumla ni mzuri. Awamu hii ndio kabisa hawataki kusikia chochote kizuri kuhusu Kilimanjaro zaidi ya mkuu kutamka hadharani kwamba kwanini mnawapa watu kutoka kule ......! Hata akifanya ziara akifika Arusha anarukia Tanga.

Hatutafika kwa namna hii watanzania, tunapaswa kujifunza kwa wale waliojitahidi na sio kutafuta namna ya kusawazisha maendeleo. Hili ndilo tatizo kubwa la Afrika.
 
Elimu sio vita wala mashindano, nilitegemea ungekuja na facts kuonesha impact kwa taifa ya hao wasomi, nyie ndo akili zenu zimeishia kuangalia div one na sio ubora wa elimu na inaisaidiaje nchi.
 
Unaruhusiwa kubisha. Ngoja niingie class kufundisha tutakutana baadaye.

Jedwali limekaa kisiasa zaidi.

Hii haimanishi Mtwara na Lindi kuna elimu bora overall. Jedwali hili ni sawa na Medali za Olimpics.

Nchi mfano Tanzania ikapeleka mwanariadha mmoja akashinda medali ya dhahabu moja halafu China ikapeleka wanariadha 1,000 walioshinda medali za fedha 999 na shaba 1 katika msimamo wa medali Tanzania itakuwa juu ya China lakini hiyo siyo sababu ya kujigamba kuwa Tanzania ni bora zaidi kimichezo kuliko China.
 
Back
Top Bottom