Mkoa wa Katavi sasa waiva


Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Messages
2,525
Likes
8
Points
135
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2009
2,525 8 135
Mwandishi Maalum


WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema kuna uwezekano wa kuanzishwa mkoa mpya ambao umependekezwa uitwe Katavi utakaozihusisha wilaya za Mpanda (Rukwa) na sehemu ya Wilaya ya Urambo (Tabora).

Alisema lengo la kuanzisha mkoa huo ni kusogeza maendeleo karibu na wananchi.

Waziri Pinda alisema hayo juzi wakati akizungumza na wakazi wa mji wa Kaliua wilayani Urambo, Tabora katika mkutano wa hadhara akiwa katika siku ya sita ya ziara yake mkoani hapa.

Alikuwa akijibu maombi ya wananchi na viongozi wa wilaya ya Urambo ya kutaka wilaya hiyo igawanywe.

Alifafanua kuwa miongoni mwa vigezo vya kugawa wilaya ni kuwa na eneo la ukubwa wa kilometa 5,000 za mraba hivyo wilayo hiyo imekidhi kigezo hicho kwa kuwa ina ukubwa wa
kilometa 28,000 za mraba. Alisema maombi yao ni ya msingi na sababu walizotoa ni za msingi.

"Maombi ya Urambo kugawanywa tumeshayapokea, kwa vigezo vyetu Urambo inayo sifa, sifa zote mnazo, nawahakikishia kuwa mkipata wilaya, halmashauri mtakuwa na fungu la bajeti, mimi ni mjumbe tu na mjumbe hauawi, nitaufikisha ujumbe huu kwa Rais Jakaya Kikwete.

Akiwahutubia wakazi hao, Waziri Mkuu alisisitiza kilimo bora chenye tija na ufugaji wa kisasa unaoweza kuwanufaisha wananchi ili waondokane na umasikini kwani wilaya hiyo ina rasilimali kubwa ya ardhi na watu.

Alisema yeye mwenyewe amekulia kwenye kilimo na inamsikitisha kuona Watanzania hawaendelei kutokana na kilimo na kwamba bado wanatumia jembe la mkono ambalo alisema haliongezi tija.

"Mimi nimekulia kwenye jembe, nimesomea kwenye jembe, lakini leo hii bado naona kuna Watanzania wanalima kwa jembe la mkono... wataalamu wanasema ukilima vizuri na kufuata kanuni za kilimo ni lazima utavuna kwa wingi," alisema.

Alisema atafuatilia maombi yao ya mbolea ya ruzuku kwa ajili ya mazao ya chakula ili waweze kuongeza uzalishaji.
Katika hatua nyingine, Waziri Pinda alisema dhana ya mashamba darasa inapaswa kusambazwa kwenye sekta ya mifugo na ufugaji nyuki na siyo kwenye kilimo pekee kwani mkoa wa Tabora una mifugo mingi lakini mchango wake kwenye uchumi wa mkoa hauonekani.
 
Ngisibara

Ngisibara

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2009
Messages
2,312
Likes
638
Points
280
Ngisibara

Ngisibara

JF-Expert Member
Joined Jan 2, 2009
2,312 638 280
Msuya=Mwanga
Sumaye=Manyara
Pinda=Katavi?
 
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Messages
2,525
Likes
8
Points
135
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2009
2,525 8 135
Hakuna tofauti na Sera ya CHADEMA ya majimbo ni yale yale tu
 

Forum statistics

Threads 1,251,743
Members 481,857
Posts 29,783,321