Mkoa wa Kagera na Majanga Mazito!

Mkoa wa Kagera na Majanga Mazito!

Wakuu,

Mkoa wetu wa Kagera umekutana na majanga mazito kuliko mkoa wowote Tanzania. Pengine kila Rais aliyetawala Taifa hili kakutana na hayo mapigo ya mkoa wa Kagera!

Mwl Nyerere alipigana vita kuukomboa mkoa wetu mikononi mwa Idd Amin! Mh Mwinyi yeye akakumbana na pigo la ugonjwa wa ukimwi kuteketeza wananchi na kuacha miji ya watu ikijaa makaburi na yatima wengi.

Mh Ben Mkapa yeye akakutana na ajali nzito ya Mv Bukoba iliyoua watu zaidi ya 800 wengi wakiwa wakazi wa huko. Mh Kikwete akakutana na ugonjwa wa mnyauko ulioteketeza migomba kama ugonjwa wa ukimwi ulivyotekeza watu! Mpaka leo bado kuna athari za ugonjwa huo wa Mnyauko.

Mh JPM yeye akakutana na tetemeko la ardhi lililoacha uharibifu mkubwa kuwahi kutokea. Sasa Mh Rais Samia tayari nae amekutana na ajali mbaya ya ndege!

Nafikiri mkoa wetu unahitaji maombi ya kipekee sana! Imekuwa ardhi inayokumbana na kila janga baya linaloibuka. Inawezekana kwenye ulimwengu wa kiroho mkoa huu una potential nzito ndio maana umejaa mashambulizi ya kila aina.

Kama Taifa upo umuhimu wa kufikiria mkoa huu kimkakati kutokana na historia hizi zinazojirudia!
Ama umemsahau au ni makusudi kwa kutokataja kagonjwa chetu Kya nyumbani aka Ukimwi,umeme,Juliana ama kasilimu.
 
Mkoa wa kagera ni moja ya mikoa yenye laana Tanzania.. unaikumbuka vita ya Kagera? kama hujui ifuatilie kwa kina ndiyo chanzo cha hayo yote .. ukifika kagera tu kama hali yako ya kiroho ipo active utagundua mambo mengi sana..
 
Ukiona mtoto anakumbana na kila mashambulizi jua ana kitu sio bure. Huu Mkoa unahitajika kuwa wa kimkakati kutokana na uzoefu huu.
Yaan kukutwa na majanga ndo uwe mkoaa wa kimkakati!! We muhaya au
 
Back
Top Bottom