Mkoa kipolisi ni suluhisho Rufiji na Kibiti?

ubuntuX

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
1,977
2,200
Wakuu,

Kwanza nitoe pole zangu kwa ndugu jamaa na marafiki wa wanaouliwa kwa kupigwa risasi huko Kibiki na Rujifi na kwa Tanzania na ujumla wake.

Pia nitoe pongezi kwa serkiali na jeshi la polisi kwa njia wanazotumia kuhakikisha wanadhibiti matendo haya ya kihalifu kibiti licha ya kutokufanikiwa, mauaji bado yanaendelea na inasikitisha sana.

Moja kwa moja, njia iliyoafikiwa na wizara ya mambo ya ndani ya kuamua kuanzisha mkoa wa kipolisi Rufiji na Kibiti, haitafanikiwa dhidi ya wahaini hawa wanaua raia wema na viongozi mbalimbali pia askari.

Kupeleka jeshi Kibiti itakuwa ni kuendelea kurisk maisha ya askari wetu, viongozi na raia kwa ujumla, haya majambazi hayahitaji vitisho, wala njia mlizotumia ikiwa ni pamoja na kukamata kamata raia wasio na hatia kwa kuwahisi tu na kuwaua mkidhani ndio wahusika sio njia sahihi.

Polisi inanjia na mbinu njingi dhidi ya uharifu na wahalifu, ni muda muafaka sasa wa nyie vyombo vya ulinzi kutumia hizo mbinu ili mtunusuru wananchi dhidi ya majambazi haya pia tujitafakari mafanikio ya njia zilizotumika mpaka sasa na matakeo yake kwa ujumla yapi katika hili jeshi kufanikiwa kwake linahitaji ukatibu na wananchi kwani wahalifu wapo miongoni mwetu wananchi, mbinu shirikishi itumike.

Hadi sasa ni ngumu kuamini kwa jeshi imara kushindwa kugunduà chanzo na kuwakamata waharifu ilhali jeshi letu limewezeshwa kwa kila kitu, tangu mauaji ya mwanzo mpaka sasa watu 30 na bado wahusika hajapatikana na haijulikani kitu wanachokitafuta na jeshi letu lipo zaidi ya kuua wasio na hatia tu au mpaka kiongozi wa ngazi za juu nchini waje kuuawa ndio tutayajua haya na kuona mbinu zenu hizo za kijeshi? Tunahitaji jeshi likamate wahalifu maramoja kuokoa maisha ya raia askari na viongozi na sharia itumike dhidi yao.
 
Yaani utendaji wa taasisi nyingi za kiserikali unatia kichefuchefu sana.

Wale watu wanataka mchezo kama wanaoucheza wao, huo wa kikomandoo watawamaliza askari wote.
 
tatizo la kibiti hata ingekuwa mimi na wewe tungeogopa kuwapa information vyombo vya ulinzi kwasababu ukifanya hivyo tu basi maisha yako unayaweka rehani
hawa magaidi walianza kitambo kujipenyeza kwa baadhi ya wananchi wasio waaminifu ndio maana mipango na mikakati inayofanywa na serikali ili kuwadhibiti wanaijua.sidhani kama kuna raia anaweza kutoa ushirikiano na jeshi la polisi kutokana na jiografia na utamaduni wa wakazi wa maeneo hayo
 
tatizo la kibiti hata ingekuwa mimi na wewe tungeogopa kuwapa information vyombo vya ulinzi kwasababu ukifanya hivyo tu basi maisha yako unayaweka rehani
hawa magaidi walianza kitambo kujipenyeza kwa baadhi ya wananchi wasio waaminifu ndio maana mipango na mikakati inayofanywa na serikali ili kuwadhibiti wanaijua.sidhani kama kuna raia anaweza kutoa ushirikiano na jeshi la polisi kutokana na jiografia na utamaduni wa wakazi wa maeneo hayo
Kama ni hivyo intelijensia inabidi ihusike kiuweledi zaidi yakutumia hawa wa vaa sare kushughulikia hilo suala.
 
Mimi rai yangu ni kuwa eneo la huko liangaliwe kwa jicho la pili....maana mambo yakiachwa yaendelee hivi hivi mwisho wake unakuwa mbaya.....

Makundi mengi ya kigaidi yalianza hivi hivi....na mamlaka kuchukulia mambo kwa urahisi...na matokeo yake tunayaona....

Hivyo basi mamlaka husika kupitia vyombo vyake viache masikhara katika maisha wananchi.....
 
Back
Top Bottom