Mkitumbua mkumbuke na kuweka dawa! Mnatutesa

Mkitumbua mkumbuke na kuweka dawa! Mnatutesa

nyamva

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2015
Posts
249
Reaction score
163
Naimani jioni ni njema kwenu wanajukwaa!!!
Kero yangu inatokana na utumbuaji uliofanywa na Dr. Laurian ndumbaro kwa maafisa utumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kwimba.kinachonikera si suala la hao maafisa NO!. wao wale jeuri yao!.lakini niziombe mamlaka husika zituonee huruma sisi watumishi wa wilaya hiyo tunaopata adha ya kukosa huduma ya maafisa hao. ieleweke kuwa ofisi hiyo ni nyeti mno kwa huduma za kiutumishi.ofisi hiyo ni signatory wa mambo mengi ya kiutumishi m.f barua za uhamisho, masuala yakinidham kwa watumishi, mikopo ya watumishi n.k.


Kuendelea Kuifunga ofisi hiyo ni kuwapa adhabu watu wengine wasiohusika na madudu ya maafisa hao!!

OMBI LANGU:naomba ofisi ya mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya atoe njia mbadala ya kutatua tatizo hilo ikiwezekana huduma hiyo kama haitarajii kutengemaa punde tutumie ofisi za utumishi za wilaya jirani kwa recomendations za mkurugenzi wetu . Mf tupewe barua maalum ili tuhudumiwe ofisi za utumishi katika halmashauri za wilaya jirani.


Najua humu wapo watu walio karibu na ofisi ya mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kwimba CHONDE CHONDE LIFIKISHENI HILI. NAWASILISHA
 
Mkuu hapo hakuna lile sanduku la maoni? Hao ulowatarget huku hawaingii sana wanaogopa kugeuzwa majipu
 
Ombi lako nalifanyia kazi, jumatatu njoo uhudumiwe kuanzia sa nne, sio uje sa moja asubuhi.
 
Back
Top Bottom