"Mkichagua wapinzani amani ya nchi itatoweka"

"Mkichagua wapinzani amani ya nchi itatoweka"

Msulibasi

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
5,957
Reaction score
8,005
Tukiwa tuna kumbukumbu ya chaguzi serekali za mitaa na tukiwa tuaelekea katika uchaguzi mkuu urais wabunge na madiwani tujikumbushe baadhi ya kauli za viongozi wa serekali katika mikutano mbalimbali iwe ya kisiasa ama ya kijamii.

Kauli hii ni ile ya kwamba mukichagua wapinzani amani itatoweka ,tutakuwa kama Rwanda .Somalia na nchi nyingine zilizowahi kuwa na vita.Kauli hii ilikuwa na nguvu sana katika chaguzi za mwaka 1995,2000 na 2005 na dakika za mwisho za uchaguzi 2015.

Hoja hapa ni kwa kiwango gani ni halali kutamka hivyo katika kampeni na mikutano,ya pili hii kauli ina maanisha nani ataanzisha vita?Ukichagua wapinzani CCM itaanzisha fujo ? Inawezekanaje mtu achaguliwe kisha aanzishe vita ?.Hoja ya tatu ni namna gani wapinzani wameweza kuipangua hii hoja maana ndio hoja kuu ya kuwamaliza,Ama nisadiki kuwa wapinzani wataleta shida?

Nasubiri miezi haipiti miwili kauli hii tutaisikia kwa wakuu wa wilaya,wakuu wa mkoa ,mawaziri, wabunge hata wanahabari.Lisemwalo lipo?
 
Kwani amani ya nchi inaletwa na CCM??, kwa taarifa yako CCM tena ndio wameivuruga amani kwa kutuibia na kutulaza njaa. Hakuna amani kwa mwenye njaa na wasiojua majaliwa ya kesho.

Amani ni zao la Haki, Kama CCM hawatatenda haki kwa kuchakachua, na kupora ushindi ikiwa ni pamoja na Kutokukubali kushindwa kama walivyotuonyesha kwenye uchaguzi s/mitaa basi watatuletea vita. Vinginevyo hizo ni kelele za chura hazitamzuia ng'ombe kujwa maji.

Tumechoka na Kudanganywa na utawala mbovu ni vema tuwajaribu hao wapinzani. Nchi hii CCM hawana hati Miliki hivyo lazima wang'oke tu hawana jinsi.
 
Kauli hii inafaa sana miaka ya 1950s. You are rate now
 
Jiulize mwenyewe kwenye majimbo zaidi ya 50 ya upinzani je kuna fujo? Je hakuna aman?

Ukimaliza kujiuliza na kujijibu ndio uje hapa.
POMPO bana! Komenti yako inamkejeli mtoa thread.Yeye katoa thread ya kutufikirisha ili tujue jinsi ya kukabiliana na kauli za kimagamba.

Labda kama unamfahamu mtoa thread personally!
 
Last edited by a moderator:
Magamba lazima yachapwe kila kitu wizi hadi uchaguzi wa vitongoji,safari hii hayatoki, amani itaendelea kuwapo ila kama wizi wa kura unaendelea wananchi hawakubali kamwe si mnaona nchi nzima, waliposhinda magamba kwa uhalali hakuna vurugu lakini popote wanapochakachua wananchi wapo macho, CCM habari ndo hiyo
 
CCM hawakumanisha kuwa wapinzani ndio watakao leta vita Bali vita vitaletwa na CCM wenyewe kwa kuwa hawatakuwa tayari kukabidhi nchi kwa wapinzani baada ya CCM kushindwa.Cc Komba mzee wa mstuni.
 
CCM hawakumanisha kuwa wapinzani ndio watakao leta vita Bali vita vitaletwa na CCM wenyewe kwa kuwa hawatakuwa tayari kukabidhi nchi kwa wapinzani baada ya CCM kushindwa.Cc Komba mzee wa mstuni.

Sasa kama ni hivyo kwanini mnazidi kuwabana na kuwanyima pumzi hao CCM hadi wavuruge amani?au hampendi amani?hamjui waathirika ni kina mama na watoto wetu wenyewe?tuwaache watawale si tufaidi amani tele
 
hii ilikuwa kauli ya kishamba ya vitisho , hata hivyo wananchi wameitupilia mbali , POOR CCM !

hatujaribu semen tutachagua na uhakikishe unalinda kura yako. ila ss wtz wengi n washamba na waoga na wenzen wanalijua hilo.. kuna sehem zngne e.g mwanza watu hawaogopi kulinda na kusimamia haki zao
 
Siku moja kabla ya siku ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa, nilimpigia simu mother baada ya kuambiwa anawapigia kampeni wagombea wa CCM.

Baada ya salam nilienda moja kwa moja kwenye point.

Sangarara: Vipi maandalizi ya uchaguzi yanaendeleaje huko?

Mother:Yanaendelea vizuri tu.

Sangarara: Nasikia (abc cba) anagombea kwa ticketi ya CHADEMA?

Mother: Ndio

Sangarara: Mtamchagua likini?

Mother: Mi nampigia Kampeni mgombea wa ccm.

Sangarara: Mnh??

Mother: Nampigia Kampeni mgombea wa ccm XYZ mtoto wa mzee ZYX.

Sangarara:Kwa nini

Mother: CHADEMA wakishinda wataleta vita.

Sangarara: Hiyo ni sababu ya kutoichagua CHADEMA, sababu ya kuichagua CCM ni ipi?

Mother: CCM ni chama cha amani na ndio kilichotulea.

Sangarara:Kwani Mbunge wa hapo ni nani?

Mother: Wenje

Sangarara: wa CHAMA gani?

Mother: CHADEMA

Sangarara: Ameleta vita?

Mother : Kimya

Sangarara: na yule wa Ilemela wa CHADEMA ameleta vita?

Mother: Kimya.

Sangarara: Mama!

Mother:Bee mwanangu.

Sangarara:tena nimekumbuka,yule mbunge wa Ilemela alikatwa mapanga na CHADEMA au CCM?

Mother: Kimya

Sangarara: hivi ameishapona.

Mother:Nasikia anaendelea vizuri.

Sangarara: Mimi si unajua niko CHADEMA.

Mother:ndio

Sangarara:Kwa hiyo mimi kwa unavyonifahamu nitaleta vita?

Mother: Hapana.

Sangarara: Sasa mbona unasema CHADEMA italeta vita, au haujui kama CHADEMA ni sisi?

Mother: Kimya.

Sangarara:Kwa hiyo mimi niko huku naangahika kutafuta maisha kumbe mama angu unazunguka mitaani kutangaza mimi nitaleta vita?

Mother: Kimya

Sangarara:Mama?

Mother: Nakusikia mwanangu..

Sangarara: Umenielewa?

Mother: Ndio

Sangarara:Umenielewa nini?

Mother: hizo habari za vita ni uongo tu.

Sangarara: Sawa ngoja nimtafute mgombea wa CHADEMA nimuambie aje akusalimie.

Mother:Mi niko hapa dirishani naona wanajikusanya waende kwenye Kampeni.

Sangarara: Muite niongee nae.

Mother: ABCiiiiiiiiiiiiiiiiiii njoo uongee na ndugu yako hapa.

Mother: anakuja, na haya magwanda yenu haya, sasa mtu anavaa makombati na jua lote hili.

Sangarara:hhahahaaaa hayo ndo kiboko ya CCM na kesho wakijaribu kuiba kura tutawatandika kweli kweli.

Mother:ahhhaaaaa na mjiandae kulinda kura CCM ni wezi sana

Sangarara: hahahahhaahaa yuko wapi ABC

Mother: amezunguka nyuma huku anakuja.

Sangarara:tena umpe kabisa ile sime yangu mtu akileta wizi ni kukata mikono tu haaahahhh
 
Tukiwa tuna kumbukumbu ya chaguzi serekali za mitaa na tukiwa tuaelekea katika uchaguzi mkuu urais wabunge na madiwani tujikumbushe baadhi ya kauli za viongozi wa serekali katika mikutano mbalimbali iwe ya kisiasa ama ya kijamii.Kauli hii ni ile ya kwamba mukichagua wapinzani amani itatoweka ,tutakuwa kama Rwanda .Somalia na nchi nyingine zilizowahi kuwa na vita.Kauli hii ilikuwa na nguvu sana katika chaguzi za mwaka 1995,2000 na 2005 na dakika za mwisho za uchaguzi 2015.Hoja hapa ni kwa kiwango gani ni halali kutamka hivyo katika kampeni na mikutano,ya pili hii kauli ina maanisha nani ataanzisha vita?Ukichagua wapinzani CCM itaanzisha fujo ? Inawezekanaje mtu achaguliwe kisha aanzishe vita ?.Hoja ya tatu ni namna gani wapinzani wameweza kuipangua hii hoja maana ndio hoja kuu ya kuwamaliza,Ama nisadiki kuwa wapinzani wataleta shida? Nasubiri miezi haipiti miwili kauli hii tutaisikia kwa wakuu wa wilaya,wakuu wa mkoa ,mawaziri, wabunge hata wanahabari.Lisemwalo lipo?

akili yako ipo katka kiwango kidogo sana
 
POMPO bana! Komenti yako inamkejeli mtoa thread.Yeye katoa thread ya kutufikirisha ili tujue jinsi ya kukabiliana na kauli za kimagamba.

Labda kama unamfahamu mtoa thread personally!

Mkuu SHIEKA

Nami pia najaribu kumfikirisha, ajue mpaka sasa kuna maeneo mengine CCM ni chama pinzani.

Vipi amani yake hapo ambapo UKAWA ndio chama tawala??

Kuna halmashauri za miji, majimbo zipo chini ya upinzani wa ccm.

So hiyo sera ama siasa ya ulaghai imepitwa na wakati.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu SHIEKA

Nami pia najaribu kumfikirisha, ajue mpaka sasa kuna maeneo mengine CCM ni chama pinzani.

Vipi amani yake hapo ambapo UKAWA ndio chama tawala??

Kuna halmashauri za miji, majimbo zipo chini ya upinzani wa ccm.

So hiyo sera ama siasa ya ulaghai imepitwa na wakati.
Tambua kuwa Tanzania kuna utulivu tu c amani,
 
Last edited by a moderator:
lazma isitawalike kwasababu wale mbuzi wa kizamani hawatakubali kushindwa.... 2015 ndio hii sasa bila ajira eti vijana tujiajiri akati mnajua mmetunyima fursa za mitaji?? Kitaeleweka tu.
 
Sehemu zote duniani amani huvurugwa na wanaotawala kwa kutosikia maoni,mahitaji na matakwa ya wananchi na kung'ang'ania madaraka.refer misri,tunisia,libya,souh sudan nk.
 
Nchi hii ni yetu wote hakuna mwenye hatimiliki kutawala wenzie siku zote kila mtu ana haki ya kutawala na kuongoza. Tusitishane huo ni ushamba na ujinga.
 
Back
Top Bottom