Siku moja kabla ya siku ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa, nilimpigia simu mother baada ya kuambiwa anawapigia kampeni wagombea wa CCM.
Baada ya salam nilienda moja kwa moja kwenye point.
Sangarara: Vipi maandalizi ya uchaguzi yanaendeleaje huko?
Mother:Yanaendelea vizuri tu.
Sangarara: Nasikia (abc cba) anagombea kwa ticketi ya CHADEMA?
Mother: Ndio
Sangarara: Mtamchagua likini?
Mother: Mi nampigia Kampeni mgombea wa ccm.
Sangarara: Mnh??
Mother: Nampigia Kampeni mgombea wa ccm XYZ mtoto wa mzee ZYX.
Sangarara:Kwa nini
Mother: CHADEMA wakishinda wataleta vita.
Sangarara: Hiyo ni sababu ya kutoichagua CHADEMA, sababu ya kuichagua CCM ni ipi?
Mother: CCM ni chama cha amani na ndio kilichotulea.
Sangarara:Kwani Mbunge wa hapo ni nani?
Mother: Wenje
Sangarara: wa CHAMA gani?
Mother: CHADEMA
Sangarara: Ameleta vita?
Mother : Kimya
Sangarara: na yule wa Ilemela wa CHADEMA ameleta vita?
Mother: Kimya.
Sangarara: Mama!
Mother:Bee mwanangu.
Sangarara:tena nimekumbuka,yule mbunge wa Ilemela alikatwa mapanga na CHADEMA au CCM?
Mother: Kimya
Sangarara: hivi ameishapona.
Mother:Nasikia anaendelea vizuri.
Sangarara: Mimi si unajua niko CHADEMA.
Mother:ndio
Sangarara:Kwa hiyo mimi kwa unavyonifahamu nitaleta vita?
Mother: Hapana.
Sangarara: Sasa mbona unasema CHADEMA italeta vita, au haujui kama CHADEMA ni sisi?
Mother: Kimya.
Sangarara:Kwa hiyo mimi niko huku naangahika kutafuta maisha kumbe mama angu unazunguka mitaani kutangaza mimi nitaleta vita?
Mother: Kimya
Sangarara:Mama?
Mother: Nakusikia mwanangu..
Sangarara: Umenielewa?
Mother: Ndio
Sangarara:Umenielewa nini?
Mother: hizo habari za vita ni uongo tu.
Sangarara: Sawa ngoja nimtafute mgombea wa CHADEMA nimuambie aje akusalimie.
Mother:Mi niko hapa dirishani naona wanajikusanya waende kwenye Kampeni.
Sangarara: Muite niongee nae.
Mother: ABCiiiiiiiiiiiiiiiiiii njoo uongee na ndugu yako hapa.
Mother: anakuja, na haya magwanda yenu haya, sasa mtu anavaa makombati na jua lote hili.
Sangarara:hhahahaaaa hayo ndo kiboko ya CCM na kesho wakijaribu kuiba kura tutawatandika kweli kweli.
Mother:ahhhaaaaa na mjiandae kulinda kura CCM ni wezi sana
Sangarara: hahahahhaahaa yuko wapi ABC
Mother: amezunguka nyuma huku anakuja.
Sangarara:tena umpe kabisa ile sime yangu mtu akileta wizi ni kukata mikono tu haaahahhh
Huu ubunifu wako nimeukubali 100%