Mkewe kiongozi wa IS akamatwa

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,884
49,035
141202090747_baghdadi_624x351_ap.jpg

Kiongozi wa IS Abu Bak

Vikosi vya usalama nchini Lebanon vimemkamata mkewe kiongozi wa kundi la wapiganaji wa kiislamu la IS Abu Bakr al-Baghdadi karibu na mpaka na Syria na mwanawe mvulana.

Jeshi linasema kuwa Mkewe Baghdadi alikamatwa pamoja na mwanawe ingawa majina yao hayajatolewa. Walikamatwa na wakuu wa ujasusi baada ya kuingia Lebabon siku kumi zilizopita.

Jarida la al-Safir liliripoti kuwa mkewe Baghdadi anahojiwa katika ofisi za waizara ya usalama nchini Lebanon.

Mnamo mwezi Juni, Baghdadi alitajwa kama kiongozi wa kundi hilo katika maeneo ya Syria na Iraq ambayo yanadhibitiwa na IS.

Mwezi jana kundi hilo lilikannusha madai kuwa kiongozi huyo aliuawa au kujeruhiwa, katika shambulizi la angani lililofanywa na majeshi ya Marekani, mjini Mosul.

Kundi lenyewe lilitoa kanda ambapo lilisema utawala wao unapanuka na kutoa wito kwa wapiganaji wa jihad kujitolea mhanga.

Jarida lililoripoti kukamatwa kwa mkewe Baghdadi, limesema kuwa maafisa wa usalama walikuwa wameiweka operesheni yao kama siri kubwa kiasi kwamba hakuna aliyekuwa na taarifa kuhusu operesheni yenyewe.

Mwandishi wa BBC Jim Muir, ambaye yuko, anasema kuwa kukamatwa kwa mkewe Baghdadi na mwanawe kutawaweka katika hali tatanishi ambayo inaendelea kuibuka Lebanon.

Kundi la IS pamoja na kundi lengine la jihad al-Nusra linawazuilia wanajeshi 20 wa Lebabon kama mateka.Source
:Mkewe kiongozi wa IS akamatwa - BBC Swahili
 
Back
Top Bottom