Mkeo akikubambikia mtoto ambae si wako utachukua uamuzi gani?

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
1,945
5,849
Huyu mtoto ana miaka 10 hamjui baba mwingine zaidi yangu, na nilikuwa najua ni mwanangu na nikawa naringa naye sana ila mwisho wa siku mama yake alijiroposha siyo wangu, nikasema sitaki kuchezewa akili acha nikapime DNA nijue moja.

Je, utachukua uamuzi gani kama mwanaume yakikukuta majibu kama haya?

IMG_20231226_211320_788~6.jpg
 
huyu mtoto ana miaka 10 hamjui baba mwingine zaidi yangu nanilikua najua ni mwanangu na nikawa na ringa naye sana ila mwisho wa siku mama yake alijiroposha siyo wangu nikasema sitaki kuchezewa akili acha nikapime DNA nijue moja.

je utachukua uamuzi gani kama mwanaume yakikukuta majibu kama haya haya .



View attachment 2853947
Pole sana Mkuu sina cha kukushauri lakini kila mtoto ana hisani yake kama vipi endelea kumlea tu.
 
Sikiliza mkuu, toka enzi na enzi wazee wetu walikuwa wanalea watoto wasio wao, na walikuwa wanajua kabisa huyu damu yangu, huyu si damu yangu.

Kiutaratibu ni kwamba watoto wote watakaozaliwa ndani ya ndoa ni wako no matter what. Hata mke akikimbia kwako, akienda kuzaa huko aliko wazee wetu walikuwa wanaenda kuwabeba hao watoto. Yani as long as umemlipia mahari basi watoto wote atakaozaa ni wako..

Shida ya kizazi cha sasa hatujui wazee wetu waliishi vipi enzi hizo mpaka wakaweza ku maintain social order✅. Sisi tunahisi haya mambo ni mapya, lakini yapo enzi na enzi.

Huyo mtoto wako na ataendelea kuwa wako no matter what, mkeo kuropoka ni jambo moja na mtoto kutokuwa wako ni jambo jingine kabisaaa, tena ameshakuwa mkubwa 10yrs?

Wewe relax, endelea na maisha yako, mwanaume hupaswi kuwa na stress na vitu vidogo kama hivi, huo ndiyo uanaume mkuu..
 
Mpumbavu mkubwa wewe hiyo nakala sio ya leo ni ya zaidi ya miaka 5 ilizunguka sana katika social media.
Hivi mnatuchuliaje members wa jf mnatuletea habari za uongo uongo tu,ubambikiwe mtoto mwenye umri wa miaka 10 unatoa wapi nguvu ya kuleta thread humu???
 
Back
Top Bottom