Mke wangu uko wapi?

Mke wangu uko wapi?

Mremaaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2015
Posts
293
Reaction score
325
Nawasalimu sana wana jukwaa, itifaki imezingatiwa!

Ni mara kadhaa nimekuja hapa kuomba ushauri juu ya mahusiano yangu yalikuwa na utofauti mkubwa " Ikumbukwe utofauti unapokuwa mkubwa katika mahusiano, na panapokuwa na tofauti zisizorekebishika hakuna mahusiano na hatimaye ndoa pia hukosekana"

Mara ya mwisho niliomba ushauri hapa mwezi Nov 2017 (kama sikosei) na niliufanyia kazi, mwisho niliamua kuachana na Mahusiano ambayo hayakuwahi kunipa utulivu na amani kwa sababu tu ya tofauti na kutokuelewana panapostahili kurekebishana"

I have been alone for almost 4 months now!!, nafurahi kuwa single ila sasa kuna vitu nakosa especially Love, romantic care, na wakupanga naye maisha ya baadaye!!

Nahitaji mwanamke mwenye sifa zifuatazo!
1. Awe mkristo wa dini yeyote ila asiwe mlokole na kama ni Muslim awe tayari kunifuta (Mcha Mungu mwenye hofu ya Mungu), maana naamini ndoa ni ibada na msingi bora wa watoto wetu baadaye.

2. Awe na uwezo mkubwa wa kupambanua mambo (critical thinker)

3. Elimu yeyote kikubwa awe msikivu kwangu na awapende ndugu zangu na wazazi wangu (mwenye kutambua jukumu lake, mama katika familia na mwenye kutumia nafasi yake vizuri "anapokuwa kazini ni kazini anapokuwa nyumbani ni mama kwangu na kwa watoto wetu " sio kuwa akiwa na majukumu ya ofisi hawezi kuyamalizia akiwa nyumbani") (Asiwe mwenye kazi zenye shift (zamu) za usiku)

4. Age below 28 Mweusi au maji ya kunde kwa rangi, urefu (155-160 CM).

5. Awe na uwezo wa kustahimili vipindi mbalimbali vya maisha.

Kiufupi kuhusu mim:-
1.Mkristo (RC)
2.Ni mwajiriwa
3.Mweupe kwa rangi.
4.Urefu 166 CM
5 . Age Early 30's

Naomba kuwasilisha kwa wenye sifa karibuni PM. Tuanzee maisha life span inazidi kupungua kila uchwao!!

Asante sana poleni kwa kuwachosha!
 
Hautaki mwanamke atakayafanya kazi zako za nyumbani? Hivi hilo neno la mwanamke aliyeajiriwa huwa mnalitoa wapi?
 
MKE WANGU HAFANYI KAZI!

Maongezi kati ya mume na mwanasaikolojia.

Mwanasaikolojia: Unafanya kazi gani Bwana Mitomingi.
Mume: Nafanya kazi Benki ni Muhasibu.

Mwanasaikolojia: Mke wako anafanya kazi gani?
Mume: Hafanyi kazi, ni mama wa nyumbani tu naweza kusema ni goli kipa.

Mwanasaikolojia: Nani anaanda kifungua kinywa asubuhi?
Mume: Anaandaa mke wangu kwa kuwa hafanyi kazi.

Mwanasaikolojia: Ni muda gani mke wako huamka kuandaa kifungua kinywa?
Mume: Hua anadamka mida ya saa kumi na moja, kwa sababu hutakiwa kusafisha nyumba kabla ya kutengeneza kifungua kinywa.

Mwanasaikolojia: Watoto wako huwa wanaendaje shule?
Mume: Mke wangu huwapeleka kwa kuwa Hana kazi ya kufanya.

Mwanasaikolojia: Baada ya kuwapeleka watoto shule, mke wako hufanya nini?
Mume: Huenda sokoni, baada ya hapo hurudi nyumbani kwa ajili ya kupika na kufua nguo si unajua hafanyi kazi.

Mwanasaikolojia: Jioni baada ya wewe kurudi nyumbani kutoka ofisini, hua unafanya nini?
Mume: Napumzika baada ya kuchoka na kazi za ofisini za siku nzima.

Mwanasaikolojia: Mke wako hufanya nini muda huo wakati wewe umepumzika?
Mume: Huandaa chakula cha usiku, huawaogesha watoto, huniandalia chakula mimi, huosha vyombo, na kisha huwapeleka watoto chumbani kwao kulala.

***************
Katika hii story unafikiri nani anaefanya kazi nyingi?

Ratiba ya mke huanza mapema asubuhi mpaka usiku mwingi na hii ndiyo inayoitwa "HAFANYI KAZI"

Kuwa mke wa nyumbani haihitaji kuwa na cheti, stashahada, shahada ya uzamivu au uzamili bali majukumu kuhakikisha ustawi wa familia ni muhimu zaidi.

Waheshimuni wake zenu wanaofanya majukumu ya nyumbani kwa uaminifu kwa sababu sadaka wanayotoa haihesabiki. Hii ni kumbukumbu kwetu kwamba lazima tuheshimu majukumu ya kila mmoja wetu na panapo uwezekano tukasaidiana.
 
Hautaki mwanamke atakayafanya kazi zako za nyumbani? Hivi hilo neno la mwanamke aliyeajiriwa huwa mnalitoa wapi?
Kuna maneno mawili pale mwajiriwa au amejiajiri, kama hivyo hana awe critical thinker maana yake kuna mengine yanaweza yakafanyika sababu ya uwezo wake wa kufikiri na kupambanua mambo
 
Katika kutafuta mke bora, point yako namba 2 usiwe unaipa kipaumbele.
Huo ndiyo mwanzo wa kujitakia matatizo.
Yaani hapo utampata mwenye shida ya kuolewa na siyo mwenye upendo na hitaji la kuolewa.

Anyway, kila la kheri
 
mkuu toa hicho kigezo namba 2,mwanamke ndio anatakiwa aweke hicho kigezo sio mwanaume.kwanza haya mambo ya mwanamke kuajiriwa ni sababu ya utandawazi na ugumu ugumu wa maisha ila mwanamke ameumbwa kama chombo cha kumselehesha mwanaume sio wa kutafuta kipato
 
Tatizo lako ni no.3 na 4
Wanawake wengi wanapenda wanaume weusi afu warefu ...... sasa naona kaka una 166 bado ni mfupi , anyways wapo watakao fulika huko pm
 
Siku hizi hatuoi Mzee baba ni kutia mimba na kulea kuoa ilikuwa mfumo wa zamani. [emoji14] [emoji4] [emoji119]
 
Awe critical thinker= great thinker?? Well umepata jf wote ni ma great thinker
 
Back
Top Bottom