Access Denied
JF-Expert Member
- Aug 10, 2012
- 655
- 211
Tayari binti kampata amfurahishaye, jifunze mbinu mpya, acha kuishi kwa mazoea.Hali zenu wana JF, imenibidi nitumie jukwaa hili ili kuweza kupata ushauri wa busara na hekima. Mimi nimekua na mahusiano na msichana mmoja hivi kwa takribani miaka 6 hivi na hatimaye mwanzoni mwa mwaka tukakubaliana kuingia ktk ndoa. Kimsingi tumeishi vizuri sana kipindi chote cha uchumba wetu potelea mbali matatizo madogo madogo ambayo ni ya kawaida ktk mapenzi, lakini kilichonifanya kuanzisha huu uzi ni kwamba toka nianze kukaa nae mwezi wa 7 amekua na tabia ya kunichagulia marafiki wa kuwasiliana nao kwny simu kitendo ambacho kinanikera sana na tabia hii hakua nayo mwanzo, sms ikiingia anataka awe wa kwanza kusoma hata simu yng ikiita anataka aone nani anapiga na jana nilipigiwa simu na rafiki tu wa kike na yeye alikua nje akifua nguo baada ya kusikia nikiongea kwny simu alikuja dirishani ili kusikiliza mazungumzo yetu na kiukweli yalikua ni mazungumzo ya kawaida ya kutakiana hali cha ajabu yeye akakasirika na kudai kwanini nawasiliana na wasichana nikamwelesha lakini bado, na ikaingia sms ya gd9t tu ya hy hy msichana basi ndo ikawa tabu akaninunia mpaka mda huu hatujaongea nae hata chakula nimekula hotelini. Sijawahi kumcheat hy mwanamke lkn kwake naonekana namcheat daily, nimeongea nae kuhusu hili suala hadi nimechoka. Naomba mnishauri nifanye nini maana nimeishavunja urafiki na watu wengi na nimebadili laini hadi watu wananishangaa lakini kwake hy haitoshi. Nampenda sana lakini huu mwenendo wake umenichosha.
kaka hilo ni kosa kubwa sana. Mimi nimejifunza siwezi kuwa na msichana mwingize ama kuzoeana na demu mwingine zaidi ya msichana wangu tu. thats all. So nakushauri uachane kabisa na wasichana wengine ukiwazoea ama wanakupigia ama nini utaipoteza ndoa. Hapo mke wako hana kosa na yupo so right wewe omba msamaha na focus kwa mke wako tu .
Mpige Mimba ata kuifata simu ataona uvivu..
aaaah Lara1 umetishaa...ila shughuli utapokutana na shankupe wa m/nyamala au tandale kwa tumbo,nakwambia shilingi itakugeuka utajuta kumchokonoa..
Inawezekana comment yako ni nzuri sana, ila una mwandiko mbaya sana, sisomagi miye miandiko mibovu kama hii.Mimi USHAURI WANGU NAUTOA FRM EXPERIANCE!!!!!! My Broo nae kabla ya kuoa alikua SWEETIE wa mademu kibao, na hata kuchangia harusi walichanga kinomaaa! Sasa baada ya kuoa si ndio IKAWA KASHESHE!!! Bi dada kila simu ikiita ANAVIMBA KAMA KOBRAAAA! Tukamshauri awe Dk 3 Mbele!!!! Sasa wale SWEETIE umewaambia unaoa nao hawana tabu na mtu, na wamekuchangia, huwezi KUKATA MAWASILIANO GHAFLA!!! Na wengine ni wateja wazuri coz anafanya BUSINESS TOKA CHINA!!!! SULUHISHO TULILOFIKIA NI KUWA NA SIMU MBILI, TENA KAMUONESHA MKEWE, MOJA YA BUSINESS, INALALA KWENYE GARI, NYINGINE YA PERSONAL NDO ANAINGIA NAYO MATRIMONIAL ROOM! LOLEST! Tena Bi Dada alipigwa biti kuwa ASIIZOEE ZOEE ILE SIMU YA BUSINESS KABISA, HIYO PERSONAL AKITAKA ASHINDE NAYO, AKAAMBIWA KAMA ANATAKA WALE MAWE HUMO NDANI ACHEZEE BUSINESS CONECTIONS AND NETWORKS!!! Hahahaaaaaa! Simu anaitaka kuikagua, Kula mawe haweziii, ALISONYAJE KIMYA KIMYA!!! Sasa na wewe UMEWEKEE MKEO MIPAKA!!!! LOL! (Mimi sikuombi kukagua, NAKULIA TIMING TU! IKIINGIA KWENYE 18 ZANGU, NAMBA TATA ZOTE NAZIKOPI, WALA SIKUULIZI, NAZITAFUTIA LINE YA MAGUMASHI!!! UTAISOMA KIMYA! KIMYA! KILA NAYEMSHUKU ATALIJUA JIJI KUWASILIANA NA WEWE! LOLEST!!!)