Mke wangu kaniambia wana ndoa sio lazima waishi pamoja, kahamia Dar lakini sijui anaishi wapi!

Ndoa bado changa
Unataka kufa si bure... Hakuna ndoa hapo huyo atakuwa ama anakuona si level yake na huenda ana mtu au pia anaona aibu kukutambulisha kwa wenzake. NDoa gani mke anaamua kuhama tu yani wala huna neno katika maamuzi makubwa kama hayo.
 
Alipomaliza chuo, nilipomuambia mambo ya kumuoa, akaniambia hapana, subiri mpaka nipate kazi, kuna mambo namalizia, nikajitahidi kuhangaika, kuna mshikaji wangu akamuunganishia, akapata kazi benki. Mshahara laki 6, sijakaa miezi miwili, ananiambia kuwa ananunua gari, nikawaza kwamba maisha gani ananunua gari, akanambia nimechukua mkopo kazini.

Mimi nikatulia, akanunua hiyo gari, nakumbuka kipindi kile IST alinunua milioni 14, nikasema poa, haina shida. Naongelea mambo ya ndoa, ananiambia mimi sina shida kuhusu kunioa, lakini siwezi kuishi huko, nataka kuishi Dar au Morogoro. Nikamuambia mimi niko Dodoma, unafanya kazi Dodoma, kwanini utake kuhama?

Akanambia, ndiyo nimeamua, kama unataka kunioa basi ni kati ya mikoa hiyo. Nikasema isiwe shida, tutahamia huko, basi tukafunga ndoa, mara kanambia anaacha kazi, anahamia Dar kama alivyonambia kwani kapata kazi nyingine huko, nikamuambia mimi uhamisho kuja Dar mgumu, ananiambia kwani nani alikuambia nataka uhamie na mimi.

Mimi sitaki kuishi na wewe, baki Dodoma, mimi nataka kuishi Dar, siwezi kuishi na mwanaume 24/7. Tukagombana, nampigia mama yake, ananiambia kama mwanangu hataki kuishi na wewe kwanini unanilazimisha. Sijakaa sawa, akaacha kazi, nasikia yuko Dar kahamisha kila kitu chake, hivyo ananiambia nitakuwa nakuja kila weekend!

Ni mwaka wa pili sasa, mke wangu namuona kila anapotaka yeye, sijui hata anaishi wapi huko Dar, nikitaka kwenda ananiambia unakuja kwani wewe ndiyo unalipa kodi, hataki hata kunizalia kiasi mimba anatoa, nipo tu hata sijui nafanya nini, nguvu ya kumuacha sina, hata nguvu ya kuchepuka sina!
Hivi uambiwe mara ngapi kuwa umepigwa na kitu kizito kaka? Ulitakiwa usimame tokea mapema, aishi na wewe or no ndoa.
Nakusikitikia huna ndoa brother
 
20240315_174600.jpg
 
Alipomaliza chuo, nilipomuambia mambo ya kumuoa, akaniambia hapana, subiri mpaka nipate kazi, kuna mambo namalizia, nikajitahidi kuhangaika, kuna mshikaji wangu akamuunganishia, akapata kazi benki. Mshahara laki 6, sijakaa miezi miwili, ananiambia kuwa ananunua gari, nikawaza kwamba maisha gani ananunua gari, akanambia nimechukua mkopo kazini.

Mimi nikatulia, akanunua hiyo gari, nakumbuka kipindi kile IST alinunua milioni 14, nikasema poa, haina shida. Naongelea mambo ya ndoa, ananiambia mimi sina shida kuhusu kunioa, lakini siwezi kuishi huko, nataka kuishi Dar au Morogoro. Nikamuambia mimi niko Dodoma, unafanya kazi Dodoma, kwanini utake kuhama?

Akanambia, ndiyo nimeamua, kama unataka kunioa basi ni kati ya mikoa hiyo. Nikasema isiwe shida, tutahamia huko, basi tukafunga ndoa, mara kanambia anaacha kazi, anahamia Dar kama alivyonambia kwani kapata kazi nyingine huko, nikamuambia mimi uhamisho kuja Dar mgumu, ananiambia kwani nani alikuambia nataka uhamie na mimi.

Mimi sitaki kuishi na wewe, baki Dodoma, mimi nataka kuishi Dar, siwezi kuishi na mwanaume 24/7. Tukagombana, nampigia mama yake, ananiambia kama mwanangu hataki kuishi na wewe kwanini unanilazimisha. Sijakaa sawa, akaacha kazi, nasikia yuko Dar kahamisha kila kitu chake, hivyo ananiambia nitakuwa nakuja kila weekend!

Ni mwaka wa pili sasa, mke wangu namuona kila anapotaka yeye, sijui hata anaishi wapi huko Dar, nikitaka kwenda ananiambia unakuja kwani wewe ndiyo unalipa kodi, hataki hata kunizalia kiasi mimba anatoa, nipo tu hata sijui nafanya nini, nguvu ya kumuacha sina, hata nguvu ya kuchepuka sina!
😂😂😂😂😂😂😂😂😂We jamaa mwanaume wa kaskazini nini?
Mkeo kabila gani kwanza?
 
Mtoa mada acha usengenge unaaibisha chama. Kabla umuoe mbona alishakuomesha dalili zote za hovyohovyo ila ukalamisha. Sijui wanawapaga nyama gani hadi mnazuzuka nao kiasi hicho
 
Back
Top Bottom