Mke wangu hajui mapishi na nikimkosoa anakuja juu

Mwanamke asiejua kupika ni mzigo tu!!! Yaani kinamshinda nini mtu kuchanganya tu viungo jamani!?
Ila mkuu, wewe ndo unateseka, mtolee uvivu na umpeleke akajifunze mapishi... Kuna vyuo kibaooo.
Au kama una mama muelewa mwambie akae na mkeo kwa mda fulani ili amfundishe... Ila msimwambue mke nia ya kwenda kukaa huko.

Nilikua namuuliza mama kuhusu kumpeleka kwa mama mkwe... Yaani mama yangu ni muelewa saana ila kwa hili kakataa eti hawezi mfundisha na ni aibu sana mume kumuomba mama ake amfundishe mkewe kupika.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkeo inaonekana ni yuko smart sana ee ,zile dizain za kufuga makucha,anaenda kazini akirud ni kusubir msosi,atajuaje kupika hali ya kua hajaaamua yy mwenyew kutaka kujua.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
kama hajui kupika wewe ndiye hujui kupika! she is your wife, yupo mikononi mwako badala ya kuja kulalamika huku tafuta namna ya kumfanya ajue kupika, kwa approach nzuri hakuna mwanamke au mwanamme mbishi duniani
 
Poleni kwa majukumu wana MMU

Ndugu zangu kama kichwa cha habari kinavyoeleza, mke wangu hajui kupika na nikimkosoa ni mbishi.

Kwa kawaida nikiwa kazini kuna Mama Ntilie anapika mpaka nachanganyikiwa hadi natamani nimpeleke akajifunze ila hatakubali na ataona nimemdharau.

Nifanyeje?
Msaada tafadhali.
Mnunulie vitabu vya mapishi
 
Back
Top Bottom