Mke wangu hajui kupika wali

Mke wangu hajui kupika wali

screpa

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2015
Posts
10,902
Reaction score
15,931
Wali ni chakula ninachokipenda kuliko vyakula vyote duniani, kwa bahati mbaya naelekea kukichukia kwa sababu ya huyu mke.

Mwanzoni nilipomuoa alimleta msichana wa kazi kwa maana yeye anaenda kazini, huyo msichana wa kazi alikuwa ni mpishi mzuri na tuliishi naye karibu mwaka mzima.

Mimi sikuwa najua chakula wali siku zote ulikuwa unapikwa na msichana wa kazi ila nimejua hilo baada ya huyo msichana kuondoka na kuja mwingine ambaye ametoka kijijini mambo ya mapochopocho ya mjini hayajui sawasawa.

Hii imelazimu muda mwingi mke wangu ndio apike, sasa nilichogundua mke wangu naye kupika hajui hasa ubweche(wali)

Leo atapika bokoboko, kesho atapika mbichi, akipika msichana wa kazi naye ni yaleyale, yapata miezi mitatu sasa sijala wali wa maana.

Sasa mnanishaurije nduguzanguni, nimtafute yule msichana wa kazi aliyeondoka nimuweke ndani ili mke wangu akae bench au mnaonaje? Nakonda mwenzenu.
 
Hapo inaonyesha kuna expansion joint zimejitokeza na usipozifanyia marekebisho ya haraka watakuja kupiga picha siku moja waandishi(wageni) uje kuumbuka na kusababisha frustration(ugomvi na mkeo) zi/usiokua na msingi.

Mfundishe usimkalie kimya
 
Mwambie aingie instagram aangalie na kujifunza jinsi ya kupika kwenye akaunti hii
" TELANDE WORLD "
 
Back
Top Bottom