Mke wangu ananishangaza sana matendo yake...

Submita

Member
Jan 22, 2021
5
7
Tuna mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 3 , Tulibahatika kupata mtoto kabla ya kuoana yaani kipindi cha upenzi ndio kipindi ambacho alipata mimba na baadae akajifungua ndipo nikaamua nimsogeze tuwe familia moja....

Jambo linalo nishangaza sana ni kauli zake tata...kama mmnavyo jua kuwa mama diamond amesema ukweli kuwa diamond sio mtoto wa mzee abdul ..

Sisi tumekuwa na stori za kawaida zinazo husiana na tukio kubwa lililo fanywa na mama diamond
Kwenye stori tunazoziongelea mke wangu anasema kumpakazia mtoto mwanaume ni jambo la kawaida ....hili jambo amekuwa akilirudia mala kwa mala pia kuna wakati akasema mtoto anapewa Baba mwenye uwezo wa kulea haijalishi kama sio wakwake kikubwa ni mtoto aende mahali salama

Nikamuuliza kama utani vile "kama shida ni malezi ya mtoto kwanini mwanaume asiambiwe ukweli kwamba uyo mtoto sio wako ila nataka umlee " akanijibu hakuna mwanaume atakae kubali kabisa kwaiyo ni lazima ukweli ufichwe ili maisha yaendelee..

Sijamuonesha kuwa naanza kumuhisi vibaya ila kwakifupi anaonekana kuwatetea sana wanawake wanao wapakazia mwanaume watoto wasio wao ...

Ananifanya niache kujiamini juu ya huyu mtoto tulie nae na ananifanya nipunguze mapenzi kwa mtoto huyu....

Msaada wenu je ? Kuna uwezekano wa kupima DNA kwa siri bila yeye kutambua ..
 
Back
Top Bottom