Mke wangu ananikera na hii tabia ya kutokupenda kuvaa nguo

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,661
Habarini,

Naombeni mnisaidie, kuhusu hii tabia ya mke wangu! Sijui kama mimi ndo nina tatizo au yeye anatatizo lakini nimekuwa nikichukizwa sana na tabia yake mbali na tabia yake hiyo lakini tunapendana sana na mke wangu.

Tukiwa nyumbani mara nyingi tunakuwa wawili, mke wangu huwa hapendi kabisa kuvaa nguo, mara nyingi anapenda kujiachia bila nguo hata akijifunga basi huishia kujifungua khanga bila ya kuwa na nguo ya ndani yoyote ile na mara nyingi hukaa vibaya kitu kinacho nifanya nione mwili wake mara nyingi akiwa hana nguo kuliko akiwa ana nguo.

Hii tabia mimi siipendi na nimejaribu kuongea nae lakini habadiriki, siipendi kwa sababu naogopa itakuja kunifanya nisiwe na hamu naye kimapenzi kupitia muonekano wake kwasababu mara nyingi na kuwa na muona bila nguo, hata akiwa anapika mara nyingi huvaa nguo ya ndani moja bila 'Bra' akijisitiri sana basi atajifunga khanga vinginevyo atabaki hivyo hivyo.

Nimejaribu kuongea nae mara kwa mara anasema hiyo tabia kakua nayo ni toka anasoma alikuwa ana tabia hiyo, kuwa akiwa peke yake au na roomates wake alikuwa anajiachia hivyo hivyo, hadi nyumbani anadai mama ake kaongea nae kuhusu hiyo tabia lakini ameshindwa kubadirika kwasababu kwao analikuwa anaishi na mdogo wake wa kike mpka baba akirudi ndo atajisitiri kidogo na ameomba nimvumilie lakini kwangu mimi naona nimechoka kumvumilia na hiyo tabia yake nisiyopendezwa nayo.

Hata mgeni akija basi atajifunga khanga na nguo ya ndani na Tshirt basi anakuwa amemaliza tena khanga nyepesi atafanya kazi zake mgeni akiondoka anarudia tena kwenye hali yake ya kutopenda kuvaa nguo tukiwa ndani na mara nyingi utamkuta na khanga kama mtu anaye taka kwenda kuoga.

Kinacho nifanya niichukuie hiyo tabia ni kuwa mimi naona nakuwa namzoea sana kumuona akiwa 'naked' au na hizo nguo nyepesi nyepesi kitu kitakacho nifanya mimi nishindwe kuvutiwa naye na kuto kuwa na hamu naye kimapenzi kitu kinachoweza kupelekea ugomvi sitaki tufike huko ndo maana huwa namwambia sipendi lakini nimeshindwa.

Nadhani mnajua ya kuwa mke akiwa anajiachia sana anapoteza mvuto na atashindwa kufanya vitu vingine vitakavyo fanya nivutiwe na yeye tukiwa ndani.Japo hii tabia akina dada wengi wanayo wakiwa ndani lakini mimi kwa mke wangu nimekuwa sipendezwi nayo japo yeye anasema amejitahidi kujizuia lakini anashindwa.

Naombeni ushauri mimi nifanyaje nibadili mtazamo wangu au kuna njia nyingine.
 
Habarini...

Naombeni mnisaidie,kuhusu hii tabia ya mke wangu! Sijui kama mimi ndo nina tatizo au yeye anatatizo lakini nimekuwa nikichukizwa sana na Tabia yake!! Mbali na tabia yake hiyo lakini tunapendana sana na mke wangu!

Tukiwa nyumbani mara nyingi tunakuwa wawili,mke wangu huwa hapendi kabisa kuvaa nguo,mara nyingi anapenda kujiachia bila nguo hata akijifunga basi huishia kujifungua khanga bila ya kuwa na nguo ya ndani yoyote ile!,Na mara nyingi hukaa vibaya kitu kinacho nifanya nione mwili wake mara nyingi akiwa hana nguo kuliko akiwa ana nguo! Hii tabia mimi siipendi na nimejaribu kuongea nae lakini habadiriki,siipendi kwa sababu naogopa itakuja kunifanya nisiwe na Hamu naye kimapenzi kupitia muonekano wake kwa sababu mara nyingi na kuwa na muona bila nguo! Hata akiwa anapika mara nyingi huvaa Nguo ya ndani moja bila Bra akijisitiri sana basi atajifunga khanga vinginevyo atabaki hivyo hivyo!!

Nimejaribu kuongea nae mara kwa mara anasema hiyo tabia kakua nayo ni toka anasoma alikuwa ana tabia hiyo,kuwa akiwa peke yake au na roomates wake alikuwa anajiachia hivyo hivyo,hadi nyumbani anadai mama ake kaongea nae kuhusu hiyo tabia lakini ameshindwa kubadirika kwa sababu kwao analikuwa anaishi na mdogo wake wakike mpka baba akirudi ndo atajisitiri kidogo na ameomba nimvumilie lakini kwangu mimi naona nimechoka kumvumilia na hiyo tabia yake nisiyo pendezwa nayo!!

Hata mgeni akija basi atajifunga khanga na nguo ya ndani na Tshirt basi anakuwa amemaliza tena khanga nyepesi atafanya kazi zake mgeni akiondoka anarudia tena kwenye hali yake ya kutopenda kuvaa nguo tukiwa ndani na mara nyingi utamkuta na khanga kama mtu anaye taka kwenda kuoga!

Kinacho nifanya niichukuie hiyo tabia ni kuwa mimi naona nakuwa namzoea sana kumuona akiwa naked au na hizo nguo nyepesi nyepesi kitu kitakacho nifanya mimi nishindwe kuvutiwa naye na kuto kuwa na hamu naye kimapenzi!! Kitu kinachoweza kupelekea ugomvi sitaki tufike huko ndo maana huwa namwambia sipendi lakini nimeshindwa!!

Nadhani mnajua ya kuwa mke akiwa anajiachia sana anapoteza mvuto na atashindwa kufanya vitu vingine vitakavyo fanya nivutiwe na yeye tukiwa ndani!!

Japo hii tabia akina dada wengi wanayo wakiwa ndani lakini mimi kwa mke wangu nimekuwa sipendezwi nayo japo yeye anasema amejitahidi kujizuia lakini anashindwa! Naombeni ushauri mimi nifanyaje nibadiri mtazamo wangu au kuna njia nyingine!
wangu nae ana tabia hiyo,ila siichukii tabia yake,naifurahia coz ana CHURA wa mwendokasi...hakika sichoki kumtazama.
 
Sasa ulikuwa unataka akiwa na Wewe Ndani awe anavaa majeans...
Wanaume wengine bwana...
Wewe Mke wako a najiachia ili mda wote uwe unasikia hamu badala ufurahie unakuja kulalamika hapa..

Wanawake wenzio wakiwa wanafundwa wanaambiwa kabisa ukiwa Ndani na mumeo awe anajiachia..
Duh we wa wapi ndugu yangu
 
Ooh jitahidi kumwambia unapenda apendeze ndani ya nyumba, ajipodoe labda pia, sema mengine asiyofanya..labda utampa fikra za kujibadilisha na kuogopa kuwa hakufurahishi.

Inabidi umpe action ambayo kichwanibataamka na kuacha hizo, pole kweli kiaina anakutia aibu wageni wakija.

Ongea nae, anza kumkimbia akivaa hivyo, atashtuka tu..usichepuke tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom