nyumba kubwa
JF-Expert Member
- Oct 8, 2010
- 10,309
- 8,398
Achana na Facebook.
Facebook imekuwa chanzo cha mitafaruku mingi sana kwenye mahusiano. Mimi kama mimi sipo huko Facebook. Nipo ila nipo ki JF zaidi. Natumia jina la Nyani Ngabu na hata hivyo sijaingia huko tokea sijui lini..hata sikumbuki.
Watu huko huuza sura tu. Kila leo wanabandika mapicha yao halafu wanasubiri kumwagiwa misifa...ooh sijui you are beautiful...sijui I miss you...mara you look gorgeous...sasa kaka hebu fikiria kidogo. Yaani kama una mwenzako yuko huko halafu minjemba inamwagia misifa hivyo utapata amani kweli moyoni na akilini mwako? Vivyo hivyo kwako. Kama wachuchu wanakumwagia misifa kem kem mkeo au mpenzio unadhani atakuwa na amani kweli? Mimi sidhani hata kidogo.
Uamuzi wa mwisho ni wako. Ukiamua kubaki..poa tu...ukiamua kuachana nayo...na yenyewe haina ubaya. Mwisho wa siku pima uone jambo lipi ni la muhimu zaidi na fanya uamuzi kulingana na majibu utakayopata.
Kuna siku mme wangu alipropose tujitoe FB nikamuhoji kwa nini; hakuwa na strong arguments. Mimi nikaisifu kuwa inasaidia ku connect na marafiki zetu wa siku nyingi wengine wa primary school ambao hatukutarajia kucommunicate nao tena.
Ila sasa naanza kushawishika. Kwanza mimi sifungui FB mpaka nikute e mail alert kuwa nina message; hence am not addicted to it at all. Ngoja nimwambie tujitoe ila sijuhi kama atakubali maana naona sasa amekuwa engaged sana na hiyo kitu kuliko mimi niliepinga.
Kweli unajua hii yaweze kufanya ma ex kurudiana. Hasara ni kubwa kuliko faida ya kuwa FB.
Jamani waungwana naomba msaada wenu huyu mke wangu mie simuelewi kabisa.
mwanzoni mwa mahusiano yetu alikuwa na tabia sana ya kuchunguza simu yangu na hakuwahi kugundua message yoyote mbaya ingawa hata msg isiyo ya kimapenzi ikiingia kwenye simu yangu so long as inatoka kwa mwanamke basi siku hiyo ni vurugu kupita kiasi akidai huyo mwanamke atakuwa bibi yangu ama mpenzi wangu tu. siku mie niliposhika simu yake siku moja, nikagundua msg nyingi za kimapenzi toka kwa wanaume wawili tofauti, anaomba radhi nikamsamehe.
Baada ya muda alikuwa akinisumbua kwa kudai kuwa mimi nina uhusiano na wanawake chungu tele kuanzia wale ninaofanya nao kazi hadi mtaani. Baada ya kuchunguza nikagundua kumbe yeye ndio ana mahusiano ya kimapenzi na rafiki yangu. mini ni mvumilivu nilimsamehe ingawa ni baada ua kukana sana na mwisho wa siku akakubali. hayo yakaisha mwaka jana.
Sasa hivi amekuja na mpya. Anasema kila mwanamke ambaye ni rafiki yangu facebook kwamba ni bibi yangu na anakomaa kwelikweli. mie nashindwa hata nimwambie nini ili aamini kuwa mawazo yake sio kweli maana kuna wasichana zaidi ya 1000 kwenye orodha ya marafiki zangu fb na wavulana kama 1000 wengine. kila comment yangu kwa mwanamke yoyote inakuwa ugomvi hauna mfano, kisa eti na comment kwa bibi yangu. kwakweli sina amani kabisa na hali hii inanikosesha raha.
Naomba waungwana mnisaidie nifanye nini maana nahisi kama anaanza tena kuficha uovu wake kwa kunipakazia mie, nahisi tu hilo sijafanya uchunguzi tena.

huyu jamaa kaingia leoleo humu jf na katuletea homework ya demu wake....mambo mengine hata tukiongea mpaka tukaukiwe koo au tuandike mpaka vidole vivimbe, mwisho wake mwenye uamuzi ni wewe kwa sababu ndiye uliyeoa na ukaahidi kuwa mtapendana katika shida na raha. hivo vumilia hata kama jamaa wanamega. pole lkn hayo ndiyo madhara ya kuvamia utandawazi bila kujiandaa kukabilianan na changamoto zake.

No inawezekana jamaa yupo JF muda mwingi.ila kaamua kubadili ID ili aweke uzi wake.

yote yanawezekana...kaamua kubadili id.

No inawezekana jamaa yupo JF muda mwingi.ila kaamua kubadili ID ili aweke uzi wake.
Mkeo mlikutana fb?
Mzee mzima hii yako kali, yaani umeoa au umeolewa maana kwa maelezo yako mwenyewe huna mke hapo maana waswahili wanasema, Mtenda akitendewa hujihisi kaonewa au mkuki kwa Nguruwe kwa Binadamu mchungu.
huyu jamaa kaingia leoleo humu jf na katuletea homework ya demu wake....mambo mengine hata tukiongea mpaka tukaukiwe koo au tuandike mpaka vidole vivimbe, mwisho wake mwenye uamuzi ni wewe kwa sababu ndiye uliyeoa na ukaahidi kuwa mtapendana katika shida na raha. hivo vumilia hata kama jamaa wanamega. pole lkn hayo ndiyo madhara ya kuvamia utandawazi bila kujiandaa kukabilianan na changamoto zake.
Kwani unadhani Nelson Mandela na Winnie Mandela hawakuwa na ndoa? au unadhani Al Goren hakuwa na ndowa? acheni kuwa wajinga na mazezeta kwa visingizio vya ndoa, na ndio maana kuna neno Divorce. Ebo!IGWE jua kwamba huyu sio demu wangu, ni MKE wa ndoa na hapo ndipo nashindwa nifanye nini na kuamua kuwaomba ushauri
Achana na facebook ujinga tu huko mie hata kutumia sijui