Mke wangu amenunua viwanja viwili bila kunishirikisha

ICDLTZ

Member
Sep 18, 2015
41
17
Dear JF,

Mke wangu tumeoana naye miaka kumi iliyopita, siku moja niliona SMS katumiwa na x-boy friend wake siku ya Jumapili ametumiwa tsh 100,000/- nikamuuliza akasema kuwa alikosea kutuma hiyo SMS kwa hiyo tuendelee na maisha.

Sasa juzi nimeona ana risiti amelipia viwanja viwili Mkuranga bila kunishirikisha mimi. Pesa alitumiwa 22/10/2015 na hivyo viwanja vimelipiwa 22/10/2015 tumezaa watoto wawili wa kiume.

Naombeni mawazo yenu please
 
Dear JF
Mke wangu tumeoana naye miaka kumi iliyopita siku moja niliona sms katumiwa na x-boy friend wake siku ya jumapili ametumiwa tsh 100,000/- nikamuuliza akasema kuwa alikosea kutuma hiyo sms kwa hiyo tuendelee na maisha.. sasa juzi nimeona anarisiti amelipia viwanja viwili mkuranga bila kunishirikisha mimi.. pesa alitumiwa 22/10/2015 na hivyo viwanja vimelipiwa 22/10/2015 ... tumezaa watoto wawili wa kiume... naombeni mawazo yenu.... pls
Pole sana mkuu. Kununue cha kwako nawe ukae kimya. Ukitaka kuleta mzozo kwa alofanya mkeo utapoteza familia.
 
Dear JF
Mke wangu tumeoana naye miaka kumi iliyopita siku moja niliona sms katumiwa na x-boy friend wake siku ya jumapili ametumiwa tsh 100,000/- nikamuuliza akasema kuwa alikosea kutuma hiyo sms kwa hiyo tuendelee na maisha.. sasa juzi nimeona anarisiti amelipia viwanja viwili mkuranga bila kunishirikisha mimi.. pesa alitumiwa 22/10/2015 na hivyo viwanja vimelipiwa 22/10/2015 ... tumezaa watoto wawili wa kiume... naombeni mawazo yenu.... pls

Toka mwezi wa 10 mpaka leo kuna mabadiliko yoyote umemwona naye.

Miaka 10 mpaka leo bado ana mawasiliano na x-boy friend wake?

Chukua hizo risit zitoe copy, rudisha mahali ulikozitoa. Tafuta documents au nenda Serikali ya kijiji husika na hizo document, ongea na muhusika yeyote serikali za mitaa mtoa hata 40,000 ili akupe information za nani walikuwa mashahidi kwenye huo ununuzi. Mweleze ukweli kwa nini unafatilia.

Ukikuta tu mmoja wa mashahidi ni huyo x, kimenuka.

Na kama una uhakika unampenda, achana na hizo habari za kumchunguza kwa sababu itakuumiza zaidi kujua ukweli wakati hauko tayari kumwacha, badala yake muulize ni kwa nini, majibu atakayokupa jifanye kuyakubali ili mwambie awe mwangalifu. Kama yuko powa atajirudi.
 
Mkuu....
Ebu kwanza rudi jando ukafundishwe tofauti HUBA na MAHABA.
Kwanza minilitarajia ungesha chukua hatua na kufanya maamuzi, kisha baada ya kuchukua hatua ndipo ungekuja hapa jf kutuambia nini kilijiri na kisha unaanza kutiririka kwa mrejesho.
Bada ya hapo ndipo wanaume wenzio tungekushauri aiseeee
 
Dear JF
Mke wangu tumeoana naye miaka kumi iliyopita siku moja niliona sms katumiwa na x-boy friend wake siku ya jumapili ametumiwa tsh 100,000/- nikamuuliza akasema kuwa alikosea kutuma hiyo sms kwa hiyo tuendelee na maisha.. sasa juzi nimeona anarisiti amelipia viwanja viwili mkuranga bila kunishirikisha mimi.. pesa alitumiwa 22/10/2015 na hivyo viwanja vimelipiwa 22/10/2015 ... tumezaa watoto wawili wa kiume... naombeni mawazo yenu.... pls

Hivi kwa nini watu hutafuta habari za x - boyfriend wa wake zao?
Nadhani hili linahitaji thread yake ila binafsi naona ni kujitafutia ugonjwa wa moyo.

Huyo ni mkeo na mmezaa watoto wawili, hivyo viwanja hata akiviandika jina lake na akija kukuacha
naamini watoto hatawatosa kwenye umiliki wa hivyo viwanja. Hivyo hilo lisikusumbue wala lisiharibu
ndoa yako.
 
Toka mwezi wa 10 mpaka leo kuna mabadiliko yoyote umemwona naye.

Miaka 10 mpaka leo bado ana mawasiliano na x-boy friend wake?

Chukua hizo risit zitoe copy, rudisha mahali ulikozitoa. Tafuta documents au nenda Serikali ya kijiji husika na hizo document, ongea na muhusika yeyote serikali za mitaa mtoa hata 40,000 ili akupe information za nani walikuwa mashahidi kwenye huo ununuzi. Mweleze ukweli kwa nini unafatilia.

Ukikuta tu mmoja wa mashahidi ni huyo x, kimenuka.

Na kama una uhakika unampenda, achana na hizo habari za kumchunguza kwa sababu itakuumiza zaidi kujua ukweli wakati hauko tayari kumwacha, badala yake muulize ni kwa nini, majibu atakayokupa jifanye kuyakubali ili mwambie awe mwangalifu. Kama yuko powa atajirudi.

nimependa ushauri wako ndygu
 
Hivi kwa nini watu hutafuta habari za x - boyfriend wa wake zao?
Nadhani hili linahitaji thread yake ila binafsi naona ni kujitafutia ugonjwa wa moyo.

Huyo ni mkeo na mmezaa watoto wawili, hivyo viwanja hata akiviandika jina lake na akija kukuacha
naamini watoto hatawatosa kwenye umiliki wa hivyo viwanja. Hivyo hilo lisikusumbue wala lisiharibu
ndoa yako.
Maswala ya ndoa sio rahisi kama unavyochukulia.
 
nimependa ushauri wako ndygu

Poa mkuu, matatizo ya ndoa wakati mwingine yanakuwa makubwa kwa sababu wana ndoa hawayazungumzi baina yao. Unaweza ukakaa na kitu rohoni kumbe kina sababu za msingi kabisa kuwa vile, ila kwa sababu hujauliza kinakuumiza bure.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom