goldie ink
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 5,634
- 9,146
Niliamini mwanaume sio mtu lege lege, hivyo nilijikaza na kuamua kwenda kazini, kutokana na kufanya kazi juani na kwa muda mrefu nilijihisi kuchoka na nilijisikia vibaya,
Nilienda kuomba ruhusa na hatimaye niliruhusiwa kwenda hospitali na bosi wangu, nilikwenda moja kwa moja hadi kwenye hospitali ya wilaya, baada ya kupimwa juu ya ugonjwa nilionao nilienda kununua dawa katika duka kuu la kuuza dawa, nilinunua dawa zangu kisha nikarudi nyumbani kwa ajili ya kupumzika.
Nilifika getini na nikaona gari zuri aina ya land cruiser v8, ikiwa imepaki ndani nikajiuliza maswali mengi juu ya ile gari hasa ukizingatia nilishawahi kuliona mahali sikumbuki ni wapi, na nikazidi kupata kumbukumbu kuwa nile gari ndiye nililiomshusha mke wangu karibu na nyumbani akitokea kazini mida ya jioni,
Sikujali sana nilipita moja kwa moja hadi sebuleni nikaona pombe kali aina ya belaire ros'e na glasi mbili zikiwa mezani, napo sikujali kwa kuwa nilikuwa nimechoka mno na kujisikia vibaya niliamua kujipumzisha nikapita hadi chumbani na nikakugundua mlango wa chumbani kwangu umefungwa kwa ndani, ghafla nikasikia sauti ya mazungumzo ilikuwa ni sauti ya kike na sauti ya kiume, sauti ya kike ilikuwa ni ya mke wangu kwani nilimjua vizuri sana lakini ile sauti ya kiume sikujua ni nani.
Haraka nikatoka eneo lile na kwenda eneo la nje kuchungulia dirishani haki ya mungu niliyoyaona mule ndani nusura mapigo ya moyo wangu yasimame, kamwe sikutaka kuamini kile nilichokiona mule ndani,
nilimuona mke wangu na huyu bwana wake ( mchepuko ) wakiwa uchi wa mnyama kama walivyozaliwa, la hasha inaonekana wametoka kufanya mapenzi muda sio mrefu,
kwa kweli miguu yangu iliishiwa nguvu ghafla na nikajiachia taratibu mithili mwendo wa kombe hadi chini nikajisikiza ukutani, nilihisi homa inazidi kupanda mara nne zaidi na jasho jingi likitoka mfano wa maji yanayomwagika bombani, kwa muda ule bado niko pale chini ukutani niliweza kusikia tena mazungumzo yao.
" sasa baby kwanini umekataa kunizalia mtoto wakati unajua nakupenda " hii ni sauti ya kiume ilisikika kwa ndani,
" hapana mpenzi wangu wa dhati sijakataa kukuzalia mtoto ila damu yako ni kali sana na hata hivyo italeta madhara na matatizo makubwa mno katika ndoa yangu " sauti ya mke wangu ilisikika vyema akimjibu mchepuko wake.
ITAENDELEA...............