huo msemo sina uhakika nao,kwa mifano yangu mimi,wapo waliooa mke wa 2,maisha yakawaendea vyema kuliko mwanzo,na wapo waliooa mke wa 2,maisha yakawaendea vibaya.kwa hiyo ni mchanganyiko.na huku niliko,talaka kila kukicha na kama sio talaka basi watu wanaongeza wake wa 2,na wengi waliofanya hivyo,kimaisha sijawaona kutatareka,wengi ni hard work na maisha yao ni mazuri tu.ila kwa mfano wangu wa karibu,my father aliongeza mke na akatutelekeza kabisa,mama yetu alikuwa single mum kwa miaka yake karibu yote.kwa sasa baba yupoyupo tu,na huyo mke wake,yeye ana kipato kizuri kabisa,hataki kumuona baba tena.na kwa upande wa mama yetu,mambo yake sio mabaya.

In most cases ndoa halali si vema kuivunja kwa sababu zozote zile mkingali hai, kweli ni kualika laana maishani mwenu, na laana hiyo haikawii,just a few years unaanza kujuta
Yah unachosema naweza kukubaliana na wewe bt kuna matatizo mengine hayavumiliki ndani. Mimi nina mfano hai kabisa, dadangu aliachana na mumewe kisheria kbsa (mahakamani) na dadangu huyu hakuchukua kitu chochote( kwenye mgawanyo wa mali) walichochuma na mumewe vyote alimuachia, its 4yrs tangu tukio hili limetokea, shemeji yetu akaoa mwanamke mwingine, hivi ninavyoandika hapa, mke 2 keshamuacha, mali zote hata moja hana, amebakiza kumbembeleza dada yetu warudiane na dada yetu huyo mambo yake sasa hivi ni supa.
wala sio kweli,mie baba na mama yangu waliachana na mama akamnyang'anya baba nyumba zote allikuwa hana mahali pa kuishi ila sasa ana nyumba nzuri tu kushinda hizi zetu,ana magari mawili na kamfungulia mkewe miradi ya bar na saloon nayo inafanya vizuri tu
Kwa kifupi Mama yako "ameharibikiwa"? siyo?
Kweli kabisa, jinsi unavyozidi kuongeza mke ndivyo majukumu unayazidisha. Mimi napendelea kuwa na mke mmoja tu. Sema inabidi mtu uwe makini kumchagua maana one mistake, one goal.
ee mwenyezi mungu nisaidie nisiolewe mke wa pili wala kuwa mama wa kambo nijalie nyumba yangu mwenyewe amina
husninyo achana na huyo mume wa mtunimepita tu.
Topic ni nyeti lakini ameileta kwa uchambuzi wa kitoto na wajuujuu, na haishawishi kuwa ameifanyia kazi, bali anapiga gumzo tu! lete data mzee na scope ya utafiti wako siyo ku-generalise issue kwani mtu mmoja akiumwa na nyoka wkt anapita njia fulani si lazima watakaopita baadaye huko ama kabla pia yaliwasibu vivyo hivyo!Hapa naongelea wanaume wanaofanya maamuzi ya kuachana na wake zao na kuoa mke mwingine au wake wengine - kutokana na sababu wanazozijua wao. Kwa waliofiwa na wake zao - poleni sana - hii mada haiwahusu au kama itawagusa - samahani sana...
Baada ya kufatilia kwa takribani miaka 40 - ndiyo arobaini na ushee - nimeonelea kuwa wanaume wengi ambao wameoa mara ya pili au zaidi wamekubwa na misukasuko mingi ya kimaisha kuliko wale ambao wamekuwa kwenye mahusiano ya ndoa na mke mmoja tu. Wanaume wengi ambao wameo mara ya pili au zaidi "wameharibikiwa" sana katika maisha katika njia nyingi mbalimbali....
Ninayo mifano zaidi ya 50 ya wanaume ambao "wameoa tena" na uzee wao umeishia pabaya sana ... Wengi wamegeuka kuwa ombaomba na masikini wa kutupwa pamoja na kwamba kabla ya "kuoa tena" walikuwa na maisha mazuri ya wastani au ya juu...
Ninapenda kuuliza, "kuoa tena" ni kujongezea mabalaa au ni changamoto za maisha...
Note: Wale ambao wanweza kuoa zaidi ya mwanamke mmoja kuishi nao hamuhusiki hapa...
Yah unachosema naweza kukubaliana na wewe bt kuna matatizo mengine hayavumiliki ndani. Mimi nina mfano hai kabisa, dadangu aliachana na mumewe kisheria kbsa (mahakamani) na dadangu huyu hakuchukua kitu chochote( kwenye mgawanyo wa mali) walichochuma na mumewe vyote alimuachia, its 4yrs tangu tukio hili limetokea, shemeji yetu akaoa mwanamke mwingine, hivi ninavyoandika hapa, mke 2 keshamuacha, mali zote hata moja hana, amebakiza kumbembeleza dada yetu warudiane na dada yetu huyo mambo yake sasa hivi ni supa.
@Ashadii: Kuoa mke wa pili mambo yakanyooka siyo sustainable - onaweza ikawa miaka mitano lakini haitazidi kumi - unakuta mwanaume amerudi mpaka kuwa mdoeaji wa Bia. Ukifuatilia sana unaambiwa huyu aliachana na mke akaoa mke wa pili akajenga maghorofa, akanunua magari, lakini baada ya muda mambo yakaanza kuharibika...
Mke wa pili anaweza akakunyanyua lakini utabakia hapo lazima utarudi chini kwa kasi ya ajabu... Kaa chini piga hesabu ya "matajiri" unaowafahamu ambao wanaweza kuwa kwenye miaka ya sitini au zaidi kidogo - waliosimama mpaka sasa ukifuatilia sana lazima utakuta ni wale wenye ndoa ambazo "hawakuoa tena"!
Huu utafiti wa wapi, will smith na donald triump vipi hawa, mengi je?