Mke wa mtu

Red Scorpion

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2012
Posts
5,736
Reaction score
4,254
Kuna kisa kimoja:

Jamaa alienda na mke wa mtu Disko, wakati ameondoka, majirani wakamtonya mume kwamba mke wake ameondoka na hawara kwenda Disko. Mume akachukua panga na kuelekea penye Disko, akamkuta mlinzi mlangoni, akamwambia kiluchomleta, kwamba lazima amtende vibaya aliyemchukulia mke.

Kwa busara mlinzi akambembeleza na kumtuliza yule mume. Akafanya mpango ili amtoroshe yule mhusika. Alipoingia ndani akatangaza kwamba kama kuna mtu amekuja na mke wa mtu, mume wake yupo nje na panga, hivyo aje apitie huku asije akaumizwa.

Kwa kuwa hakutaja jina, alishangaa kuona ukumbi karibia wote wanakimbilia alipo Mlinzi.
 
ha ha haa ha. haaa..

mi mwenyewe nilikuwepo nikatimua mbio kuelekea mlango alioonyesha baunsa na kumwacha mwanamke niliyekuwa naye ndani
 
ha ha haa ha. haaa..

mi mwenyewe nilikuwepo nikatimua mbio kuelekea mlango alioonyesha baunsa na kumwacha mwanamke niliyekuwa naye ndani


πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚
 
Duh, ni balaa, yaani ukumbi mzima wamekuja na michepuko sumu!!
 
ee safi Acheni michepuko mtakuja mkatwe vikojo.LeoπŸ™
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…