TANZANNIA
JF-Expert Member
- Sep 29, 2015
- 1,047
- 384
Kuna dada mmoja ambaye ni mke wa mtu naishi naye jirani umbali kama wa nyumba nne au tano kutoka kwangu ni mzuri sana kwa sura na umbo, sina mazoea naye sana na ananiheshimu sana na tukionana huwa ananiamkia.
Sasa cha ajabu juzi kati nikaona namba ya kigeni kwenye simu yangu ikiita, baada ya kuipokea akajitambulisha na kuniuliza kama niko wapi kwani ana maongezi na mimi, nikamwambia niko grocery, ndipo akaanza hadithi zake kuwa ananipenda tangu siku nyingi lakini anakwazwa na vitu viwili, kwanza yeye ni mke wa mtu nami ni mume wa mtu na pili ni heshima aliyonayo kwangu na amejitahidi kuvumilia kwa karibu miaka minne.
Sasa ameshindwa na ameamua kusema ukweli mimi ndio nitoe maamuzi niendelee kumumiza kwa kumkatalia ombi lake au nimsamehe kwa kunikosea adabu au niwe naye at least mara moja tu ili roho yake iridhike.
Nifanyeje wanajamvi?