Mke wa Mbunge Babu Owino aiomba Serikali kumuachumia huru mumewe

Kenyan

JF-Expert Member
Jun 7, 2012
414
313
Mbunge wa Embakasi Mashariki Mheshimiwa Babu Owino angali bado anashikiliwa na polisi katika kituo cha Polisi cha Wanguru kilichoko kaunti ya Kirinyanga, Mke wake Fridah Ongili amethibitisha.

Owino ambaye ni mwandani wa karibu wa Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga alikamatwa Jumanne jioni katika Uwanja wa ndege wa JKIA jijini Nairobi. Hatahivyo haijabainika wazi sababu ya maafisa wa polisi kumsafirisha mpaka kaunti ya Kirinyaga.

Mke wake sasa ameiomba serikali kumuachua huru mumewe akisema kuwa anaugua.

"Nachotaka Mimi ni kumuona mume wangu nimpe chakula na dawa kwani hajiskiaa vizuri." Alisema Fridah baada ya maafisa wa polisi kumzuia kuona mumewe Mheshimiwa Babu Owino.

Mbunge huyo ni moja kati ya waandani wa Odinga waliokamatwa na polisi siku ya Jumanne na Jumatano kwa lengo la kuzuia uchochezi.

Mpaka kufikia sasa Raila Odinga hajulikani aliko japokuwa anawasiliana na wafuasi wake kupitia mtandao wa twitter.

Juhudi za Wanahabari kumfuata nyumbani kwake Karen pamoja na ofisi yake iliyoko mtaa wa Capitol Hill bado hazijafua dafu.
 
Back
Top Bottom