Mke wa Makalla anusurika kifo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke wa Makalla anusurika kifo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pengo, Aug 25, 2010.

 1. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Na Mwandishi Wa Risasi
  Wakati Katibu wa NEC ya CCM, Uchumi na Fedha, Amos Gabriel Makalla akitarajiwa kuzindua kampeni zake kwa kishindo Agosti 29, 2010 (Jumapili ijayo), Mzumbe, Mvomero, mke wake, Grace Makalla amenusurika kifo.

  Grace, alipata ajali ya gari iliyonusa roho yake juzi (Agosti 22, 2010), katika eneo la Misungusungu, Kibaha, Pwani alipokuwa safarini kuelekea Morogoro kwenye msiba wa Katibu wa CCM Mvomero, Richard Kaseja.

  Chanzo chetu cha habari kilitupasha na baadaye Makalla kutoa uthibitisho kuwa Grace au Mama Gabriel alipata majeraha makubwa na kuvunjika mkono.  Mtoa habari wetu wa awali alisema, Mama Gabriel alikuwa kwenye tukio muhimu la chama na Mvomero kwasababu alikuwa anakwenda kwenye msiba wa katibu huyo.

  “Ana hali mbaya, hatujui itakuwaje lakini heshima ni kwamba amepata ajali hiyo wakati anafanya jambo kwa maslahi ya CCM na wananchi wa Mvomero kwa jumla.

  “Anasikitisha lakini tunamuombea Mungu ampe nafuu ya haraka. Ni mtu mwema kwa sababu alikuwa amejitolea kwenda Musoma kushiriki mazishi ya Kaseja na kwenye gari lake alibeba ndugu wawili wa marehemu pamoja na Katibu wa UWT, Mvomero (Tuhuma Lihepa),” kilisema chanzo chetu.

  Gazeti hili lilipowasiliana na Makalla Jumatatu wiki hii, majira ya saa moja jioni, alisema kuwa anamshukuru Mungu kwasababu mke wake ndiyo kwanza alikuwa amerejewa na fahamu na kuanza kuzungumza.

  “Amelazwa Tumbi, amevunjika mkono na ana majeraha makubwa. Namshukuru Mungu amepata nafuu na ameanza kuongea,” alisema Makalla.

  Uchunguzi wa baadaye wa gazeti hili ulibaini kuwa gari alilokuwa amepanda mama Gabriel ni Toyota Land Cruiser Hardtop ambalo lilichomekewa na Tipper la mchanga.
  Hata hivyo,gazeti hili lilibaini kuwa Tipper hilo ndilo lililopinduka na Land Cruiser liliharibika kwa kiasi kikubwa.


  Adha, Risasi lina majibu kuwa watu wote waliokuwa wameambatana na mama Gabriel kwenye gari hilo, walitibiwa na kuruhusiwa muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya Tumbi na kubaki yeye amelazwa kwa sababu alipata majeraha makubwa.

  Gazeti hili nakala ya Jumamosi iliyopita, liliandika kwamba Makalla ambaye ni mgombea ubunge Jimbo la Mvomero, anatarajiwa kuanza kampeni zake Jumapili inayokuja, Kata ya Mzumbe.

  Habari tulizozipata zinasema kuwa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’ itafanya onesho ‘babkubwa’ la kumsindikiza Makalla siku ya uzinduzi wa kampeni zake, Mzumbe.
   
 2. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,033
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Mmmh!! Hata kabla hajawa mbunge, akipiga chafya nayo mtaandika.Huyo Makala akiwa waziri mkuu je?

  Mbona ajali ya mtoto wa jana haikua covered kwenye magazeti ya leo na tbc kiivyo.
   
 3. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,185
  Likes Received: 233
  Trophy Points: 160
  Mpaka ifike 31 Oct, 2010, tutaona na kusikia mengi kutoka ccm.
  Wana maombi mpo? Nitasugua magoti mpaka Mungu atajibu kuhusu nchi yetu. Yaani makapi kama hayaachii uongozi, yatafia majukwaani il watu wapone na umaskini.
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  nawatakia majeruhi wapate nafuu ya haraka
   
 5. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  AMEN
  mix with yours
   
Loading...