Paul Alex
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 4,342
- 9,824
Dar es Salaam. Mjane wa aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba, Salome Komba amesema kuna kipindi mumewe alijisahau kusaidia watoto wake ada na badala yake alijikita kusaidia wananchi wa jimbo lake.
Kwa mantiki hiyo, amesema hafikirii kujihusisha na siasa kwa kuwa hakuona mafanikio aliyopata mume wake katika kipindi chote cha uhai wake.
Akizungumzia maandalizi ya uzinduzi wa kitabu cha historia ya maisha ya mumewe jijini Dar es Salaam leo, Salome amesema:
“Sitaki kujihusisha na masuala ya siasa kutokana na changamoto kubwa niliyoiona kupitia kwa mume wangu wakati akiwa mbunge.
“Licha ya kuwapenda watoto wake 11 na kuwataka wawe kitu kimoja, marehemu mume wangu aliwapenda zaidi wananchi wake wa jimbo la Mbinga Magharibi kuliko watoto wake wa kuzaa ambao wakati mwingine walikuwa wanaomba wapewe ada lakini hawapewi.”
Mke wa mwanasiasa huyo maarufu wakati wa uhai wake amesema kuna wakati Komba alijisahau kusaidia watoto mahitaji yao ya shule ikiwemo ada na badala yake alijikita kusaidia wananchi wake, alikuwa radhi kusaidia wananchi wake kuliko watoto wake.
Salome ambaye kwa taaluma ni mwalimu wa Hisabati na Kiingereza amesema anajipanga kufufua shule zake zilizotaifishwa na benki ya CRDB baada ya kushindwa kulipa mkopo.
“Tangu afariki mume wangu sijaona kiongozi hata mmoja wa chama au wa serikali amekuja kunitembelea zaidi ya mke wa Rais wa awamu ya nne, Mama Salma Kikwete ndio aliniita Ikulu Septemba mwaka jana na kuniambia yupo pamoja na mimi,” amesema Salome na kuongeza:
“Mbali na mama Salma kuniita , pia walikuja kunitembelea wake wa mawaziri ambao waliwakilishwa na mke wa Nyarandu na Maige lakini baada ya hapo sijawahi kuona kiongozi yoyote amekuja kunitembelea zaidi ya siku ile ya msiba,” amesema Salome mama wa watoto watano.
Salome ambaye alikuwa mwalimu wa shule ya msingi Lugalo kuanzia mwaka 1979 hadi 1997, anafafanua kuwa kifo cha mumwe anahisi kilitokana na mkopo wa CRDB licha ya ukweli kwamba alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu na kisukari.
“Kitu ambacho sitasahau ni kifo cha muwe wangu, kilikuwa ni kifo cha ghafla kwa sababu siku ile asubuhi aliamka salama tukaongea nae vizuri tukacheka nae vizuri lakini ilivyofika mchana hali ilibadilika na kuzidiwa na hivyo kukimbizwa hospitali,” ameongeza.