Tumeongelea sana elimu, pia kuna vyeo au madaraka hata kama wote ni wasomi. Mke akiwa na madaraka makubwa kumpita mume inaweza kuleta shida fulani aidha kwa mke kujiona yuko juu au mume akawa na complex inferiority!!
Michango mingi imenivutia.Napenda kuongezea kuwa ili ndoa isimame au ifanikiwe kuna bare minimums zinazotakikana bila kujali pesa au usomi ambao nao una nafasi/athari zake:
1. Mmekutana wapi - wengi hupuuza sana hii lakini ina nafasi yake maana itaamua huko mbele ya safari kutakuwa vipi. Mmekutana kwenye mazingira yenye kutoonyesha uhalisia kisha mkaamua kuoana basi ni tabu na shida tupu kwa vile mtakuja kugundua mengi ambayo hamkuyatarajia na ugomvi utakuwa hauishi
2. Mna interests za kufanana? k.m mmoja anapenda kujiendeleza mwingine hapendi anapenda starehe zaidi.Hata kama usomi upo ni tatizo maana matumizi ya rasilimali yatahitaji maamuzi magumu na assuming kuwa mama ndio ana pesa zaidi au msomi zaidi baba hatapenda kusikiliza ushauri au maamuzi ya mkewe maana anajiona yeye ndio kichwa lazima asikilizwe.
3. Heshima- Kama wanandoa hawaheshimiani au dharau imetawala, basi usomi unakuwa kama mwiba kwenye uhusiano.Haijalishi ni mwanamke au mwanaume.
4. Uelewa wa pamoja kuhusu kuingia katika ndoa - wengi husukumwa kuingia kwenye ndoa bila hata kujua wanajiingiza kwenye majukumu makubwa yenye kutaka commitment kubwa pia.Wengi ndoa ni fashion au ni tamaa zaidi ya kutaka kuwa pamoja bila kujua mapenzi kama mapenzi yana maisha mafupi kabla uhalisia haujaingia.Usomi huweza kujenga kiburi cha kukimbia majukumu au kutokutaka kusahihishwa pale mtu anapokosea. Ingetarajiwa usomi usaidie watu kupima kama kweli wanaingia kwenye ndoa wakiwa well informed au wanaingia tu kama fashion.Bahati mbaya sana wasomi wengi ndio wa kwanza kuingia kwenye ndoa wakiwa ignorant kuliko wasiosoma.Wasiosoma utakuta wanaingia kwenye ndoa wakijua hasa nini wanakifuata, heshima inakuwepo, nk. Usomi + pesa = jeuri, dharau, kujiamini kwa kipumbavu, kutokujali nk.
Cha msingi ili ndoa isimame wanandoa wanatakiwa wawe na yafuatayo:
Uvumilivu, unyenyekevu, staha, Heshima, kumcha Mungu,na kujua kuwa ndoa si lele mama - ni msalaba na siyo fungate!
Ndoa ni maelewano, na mnapokutana regardless of your background kinachowakutanisha ni penzi, baada ya muda ndio mnaanza kujuana tabia,ndugu na kisomo
Kwa upande wangu mimi na mume wangu kielimu tuko sawa ila tunafanya kazi tofauti, mwaka huu Mungu akipenda tutatimiza miaka 7 bila kokoro wala kelele I thank God daily for meeting and calling this man my husband,
Mambo tunayobishania hapa home mara nyingi sana ni future plans kama kubadili kazi,ujasiriamali etc maana kila mtu ana maono yake but we compromise,
Hatujawahi kuhitlafiana kuhusu elimu kwa watoto or matumizi ya pesa zetu za mshahara, kila mmoja anakatwa kiasi sawa kwa mwezi kuingia ktk account za watoto
Couples za wasiosoma kabisa huwa zimetulia sana! Refer enzi za ujima na zama za mawe ndoa zilikuwa zinadumu sana.
Mifano ipo hata Marekani wanawake waliosoma ni likely to become feminist ama Lesbian. .
Cha msingi ili ndoa isimame wanandoa wanatakiwa wawe na yafuatayo:
Uvumilivu, unyenyekevu, staha, Heshima, kumcha Mungu,na kujua kuwa ndoa si lele mama - ni msalaba na siyo fungate!
Usomi ni muhimu lakini dimension za mapenzi hazipimwi kwa usomi wa mtu. Ndio maana kuna prof wangu anafanya research Nasa alioa ba maid wa pale vatican sinza.
Couples za wasiosoma kabisa huwa zimetulia sana! Refer enzi za ujima na zama za mawe ndoa zilikuwa zinadumu sana.
Hapo kwenye kubishana mara kwa mara ndipo sie wanaume tunakereka, tunapenda tubishiwe lakini isizidi, ukweli unabaki palepale, kwa sasa mwanamke msomi au mwenye mafanikio zaidi ya mme wake huwa wanakuwa na kauendawazimu fulani hivi, nadhani ni ulimbukeni kwani sababu hali haikuzoeleka miaka ya nyuma, baadaye wataona ni hali ya kawaida. Nilialikwa kwenda dinner kwa Proffessor wa kike(sheria) na mme wake polisi constable mstaafu ( hawa wote ni wazungu kwenye nchi iliyoendelea), nilichokiona pamoja na usomi wake nyumbani ni mke mwema kama walivyokuwa wake wa miaka ya 1850s. Huko kwa wenzetu kuna ambao ulimbukeni wa mafanikio umeshaanza kuwatoka wengine bado wehu na kuamua kuishi kwa upweke wanishia kupendana na mbwa wao maana wameshindwa kuenzi hisia za mwanume. Cha muhimu wanaume tuwapende wake zetu ili nao watuheshimu kama inavyosema Bibia- kwa wakristo.