mke kuomba hela/service kwa wazazi wake hadi leo hii!

kaka mtoa mada (realTz 77)..hili ni suala dogo sanaaaaaa...kama unatumia kitabu cha biblia kwa maana ya kuwa mfuasi wa kristo...naamini ulifunga ndoa ya kikristo na kiapo cha kikristo cha ndoa kinaelezea mambo yoooote kwa umakini...."mutawaacha baba na mama zenu (WAZAZI WENU) na kuambatana pamoja kama MME NA MKKE ...na kwenda kuanza familia yenu".....hapa maandiko yanakuwa wazi kabisa na hapa ndipo ile heshima tulopewa wanaume ya kuwa VICHWA vya familia inapotumika ipasavyo.

sasa huyu mwenzako naomba ukae naye chini na kisha umwambie kuwa KUENDELEA KUWATEGEMEA WAZAZI WAKE wakati wewe kichwa upo kunakunyima haki yako ya ki-dini na kiimani mloitumia kuapa juu ya ndoa yenu...MTAVUMILIANA KWA SHIDA NA RAHA, UGONJWA NA AFYA NJEMA ..MPAKA KIFO KIWATENGANISHE...

mkumbushe kuwa hata kama hamna kitu (mna shida)..ni kifo ndicho kinatakiwa kiwatenganishe...na sio pesa za wazazi wake....NAAMINI kama alilelewa katika maadili ya kumjua MUNGU hata kwa jumapili moja ya kila week atakuelewa na ataelewa nini maana ya kiapo cha ndoa mlichoapa...

kingine cha msingi zaidi ..MKUU MATUMIZI KATIKA FAMILIA LAZMA YAWE CHINI AU BASI SAWA NA MAPATO KATIKA FAMILIA....ikitokea mapato yakawa chini na matumizi juu matokeo yake ndio haya ya WIFE KWENDA KWAO KUOMBA MISAADA...(wengine wanaomba kwa wanaume zao wa nje na hata maboss wao kazini kwa makubaliano ya tendo la ndoa)...jaribu kujadili matumizi na mapato ya familia na mkeo ili mujue haya mapungufu yanatokana na nini...

usiseme mkeo analipwa mshahara mzuri ukadhani umemaliza kazi...mshahara mzuri kiasi gani? na kwa matumizi gani?..ana save kiasi gani?..kwann anakuwa ombaomba.?....check her lifestle...wanawake wengi waajiriwa ndio hao ma-model wa maofisini kila baada ya break wanabadili nguo, viatu mikoba na perfumes, wengine hata hawaumwi macho ila wana-pair 100 za miwani ya macho..fashion-galz, too material, sooo much westernized ...ili mradi mashindano kwa kwenda mbele

NI MAONI TUU WADAU SEMA YENYE MTAZAMO MKALI KIDOGO KUKEMEA UVUNJIKAJI WA MAADILI NDANI YA NDOA
 
ama la kupew service na pesa kutoka kwao sijaona tatizo hata kidogo......
nafikiri kuna akina dada wengi ambao hata kama wameolewa wanapenda kubakisha ule upendo uliokuwpo kwa wazazi wao, ambao ni kama hiyo kupewa service fulani fulani au kununuliwa zawadi kwao......sio kama huw na shida, lakini huwa anataka kumfurahisha mzee wke tu kwa kupokea service zake na pesa.

anapokea service na pesa kutok kwako pia kuonyesha mapenzi na ndo vile vile nvyotaka kufany kwa wazazi wake

hamna tatizo mkuu, sidhani kama ina lengo la kukuletea dharau in any way
 
Lady N
user_offline.gif


Angeliona wapi wakati mwenzako alikua ana wahi kuoa mtoto matawi? Haya ndio matatizo ya kuoa kwa malengo, unapo kua umechoka mlala hoi unawahi kukamata mtoto wa kishua, ukiamini kua mambo yata kua super. siku ukimuoa , maana baba mkwe ataawapa kila kitu hawezi kukubali mwanaye ateseke

Siku inafika unatumia cheo cha mkweo na kuweka mambo yako freshi , unatengeneza hela kibao na kwavile wewe ni a male gold digger unakua una ubahili wakumpa mkeo mahitaji yake ( pale unapo pata utajiri kwa kutumia mgongo wa wazazi wa mke sababu wana influence sehemu kibao au hata mtaji wamekupa ) , sababu una vicheche vingi na pia hukumuoa mkeo kwa mapenzi , ulioa cheo au uwezo wa wazazi wake so inakua ngumu kumridhisha ,kwani umesha mtumia vya kutosha kujineemesha , mbaka mkeo ana amua kuanza kuomba hela au mahitaji kwao, maana kama hupendi ungeipinga hiyo tabia toka mwamzo.

Acha binti ya watu asaidiwe kwao kwani ndio kwnye mapenzi na malezi mema, kwao wana upendo wewe na kwa hizo inecurities zako zisichangie kuondoa upendo uliopo kati ya mkeo na familia yao , Kama baba yake anampenda bintiye mwache kwani haibadilishi kitu , huyo demu ndio kalelewa hivyo na ndio misingi yao ya maisha bora na kusaidiana , uiingilie kutaka kubadili maisha yao au labda usinge muoa.

Mh!Nilikua nataka kumuambia amshauri mkewe kua ni vizuri to grow out of the NEST, yaani ni wakati muafaka wa kuwaonyesha wazazi kuwa tunawajibika kwa kiasi chetu. Hata kama ni wa matawi kuzidi nyie, mnaenda hata na ka-wine hivi. Lakini basi, shemeji hangaika nalo. Na wewe peleka maombi yako, si wazazi wako pia... Mphhh(pumzi hiyo, naishushaaaa). Taratibu tu msije mkahamia kwao kuepuka shida za mtaani kwenu eeh!
 
btw, kwani shida nim nini, as long as wewe kama mumewe unatoa matumizi yote, na roho yako iko nyeupe , acha achukue pesa kwao, may be zipo nyingi na hazina kazi je? that is between yeye na parents wake, live your life. labda ana tamaa no matter how much you give her is not enough, wacha achukue kwao bana, si kwa wazazi wake?
 
Pole sana mkuu, cha kufanya ni kujaribu yafuatayo;

1. Uwe serious na umuoneshe kuwa wewe ndio kichwa cha familia yenu.

2. Mkalishe chini umweleze facts, kama hayupo tayari basi uwaeleze wazazi wake tena sio kwa kuwabembeleza, bali kwa kuwafikishia ujumbe kuwa hujisikii vema kwa hilo.

3. Mpunguzie uhuru wa kufanya mambo yake mwenyewe, na kila atakachotaka kukifanya akushirikishe tena kwa ukaribu sana.

4. Mpunguzie access za kuwatembelea hata ndugu zake bila sababu ya msingi, tena bila ukaribu wako.

5. Anza kumpangia majukumu ya kifamilia ambazo zitahitaji matumizi ya mshahara wake.

Kwa kufanya haya, utapata ukweli juu ya mazoea yake na mipango yake........!
 
.........Inawezekana wewe sio mtoaji wa pesa kwa mkeo, labda unasubiri hadi akuombe. Kuna baadhi ya wanawake huwa hatupendi kuomba pesa kwa waume zetu........hivyo anaona bora kuomba kwa wazazi wake na sio kwako, mtoto kwa mzazi hakui.

Hivyo inabidi ujifunze kumpa pesa mkeo hata kama haombi, usipompa atakwenda tu kwa wazazi wake. Hata kama mkeo ni mfanyakazi lakini inabidi tu umpe pesa.

Hizo ndizo tamaa za fisi. Hivi anamwombaga nani? baba au mama?
 
ReaTz77;

Hili tatizo naliangalia kwa sura mbili:
sura ya kwanza ni naivety yako na ya mkeo kupelekea kushindwa kutambua maana halisi ya ninyi kuwa mwili mmoja... inaonekana bado mliegemea kwa wazazi (hata kama ni wa mke pekee) na kuendeleza utoto au ujana ndani ya ndoa. tabia hiyo sasa imekua part of you family life na kuiondoa ni kazi sana na in most cases huondoka only kama kutakua na mtafaruku au faceoff kati yako na wazazi wa mkeo, tena uombe wawe waelewa, la sivyo umekwisha

sura ya pili, ambayo ni kwamba ulion na ukafumbia macho maksudi - fikra tegemezi kwamba misaada wakileta mafaidi kwahiyo haukuona ugumu sema sasa imezidi na ujue mwenye pesa ndiye mwenye sauti sasa umezidiwa

mengine yaweza kuwa kwamba mkeo bado anapenda kwao kuliko wewe, she has a fall back position na siajabu anavuta mda tu...

Iwapo wazazi wa demu ni waelewa hawatakudharau, lakini mara nyingi hii hali huendana na dharau ya kiaisi fulani na utaiona siku mkigombana, watakua wa kwanza kumwambia kwamba arudi tu nyumbani; hawajashindwa kumlea

as a way forward mimi naomba uongee na baba mkwe na mkeo mkiwa pamoja na pia muandane namna ya fu-finance nyumba yenu sustainably. ongeza msaada kwake lakini pia kuwa very firm kwenye haya mambo ya kuombomba hela

suala la kusema mambo ya ndoa yake kwao, hilo huwa halizuliki na wengi wanafanya hivyo ingawa ni kwa siri... jaribu kumshauri apunguze na achuje ya kusema nyumbani!!! ndoa nyingi huyumba kutokana na ndugu kujua siri nyingi za ndani
 
kama anatabia ya kueleza kila kinahotokea nyumbani kwenu basi huenda hata pale unapoishiwa anawaambia wazazi nao kama kumpenda mtoto wao wamemruhusa anaohisi kuwa na shida yoyote basi awaeleze wao ili waweze kusaidia
 
Waswahili wanasema samaki mkunje angali mbichi...akishakauka hakunjiki.
 
Hii inaenda na tabia ya mwanamke kukopa dukani; unashtukia unaambiwa duakani tunadaiwa hiki na kile; au nilichukua hiki na nikachukua kile; nadhani ni kudhibiti matumizi ndio dawa; lakini usizuie ama kupunguza access ya ndugu zake by the way how do you do that?
 
Pole sana mkuu. Kama ana sababu ya kuomba ningeona haina shida. Ila kama anaomba tu for the sake of doing it, siyo kitu kizuri hata kidogo. Ndani ya mji wako wewe ndio head of the family. Lakini kama bado wazazi wake ndio wanaotoa hela, ipo hatari kubwa mbele ya safari ya kuwa na influence kubwa katika mambo ya msingi kabisa ambayo wewe binafsi yanaweza kukukwaza sana. Ukikua ukaanza mji wako, bora pia uachane na baba na mama kwa utaratibu muafaka.
Hapo mzee ni lazima utumie busara kumuweka sawa mama watoto. Maana kuna siku zinaweza kuja ukiendelea kuacha hiyo free style ya kuwa na pesa kuendelea litakuja jambo halafu wewe utawekwa kwenye kona.
 
Back
Top Bottom