Mke kazidi mizaha

foreigner

Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
57
Reaction score
60
Nawasalimu.

Mnisamehe kwa kutokuwa mwandishi mzuri.

Moja kwa moja kwenye hoja ya msingi.

Nimeishi kwenye ndoa na huyu mke wangu kwa miaka 10 na kujaliwa watoto wawili.

Kilichonifanya nije hapa kuomba msaada wa mawazo ni hili tatizo la mizaha ya huyu mke wangu, amekuwa mtu wa kujibu au kuongea bila ya kuweka mipaka (kutenganisha kipi Cha kuongea na mpenzi na kipi Cha kuzungumza na mume ambaye ni mkuu wa kaya).

Nikiri ya kuwa katika maisha yetu yote nilishawahi mchapa makofi mara 3 kitu ambacho sitaki kukikumbuka na sitaki kitokee tena, ila nilifanya vile Ili tuu aweze kutambua kuwa sipendezwi na tabia zake.

Tabia hiyo ya kutokuwa na mipaka hasa ya kuzungumza haijawahi kwisha zaidi ya kupungua kwa muda na baadae kuanza tena.

Nimewahi kutumia kanuni ya kumtoa out na kwenda naye sehemu ya faragha na kumuambia kuhusu kutopendezwa na tabia zake huwa anaomba msamaha lakini baada ya muda hurudia tena.

Kiukweli ninampenda sana mke wangu, na mahusiano yetu yalianza tangu tukiwa secondary na baadae kuja kuoana.

Nje ya kumkanya mara kwa mara, niliona ni busara kufikisha jambo hili kwao, Ili waweze kumkanya binti yao, ila sikuona mabadaliko yoyote yale.

Yote yaliyotendeka niliweza kuvumilia ila hili nililolipata wiki hii, limenizidi uwezo. Baada ya chakula Cha jioni tukaingia chumbani, alikuwa anapanga nguo Mimi nikatangulia kuoga, baada ya muda nikatoka yeye akiwa Bado busy, kama kawaida kabla ya kulala ni kumshukuru Mungu kwa ulinzi wake wa siku, nikasikia akiseme acha kusali uongo.

Niliumia sana, nikamaaliza sala na kumuuliza ulikuwa unamaana gani, nikaona anacheka, nikamuuliza hii midhaha yako itaisha lini lakini akawa anaendelea kucheka, kwa kweri nilipatwa na hasira sana ila niliishia kutoka kwenda barazani ningeendelea kuwa pale ningeweza kumpiga kitu ambacho sitaki kitokee tena.

Mimi nimemzidi miaka 4 huyu mke wangu, hata kielimu nimemzidi, kisalary nimemzidi zaidi ya mara 4.

Nimeandika hivi Ili kutoa Ile dhana ya kuwa huenda nalelewa, nafanya majukumu yangu kama baba vizuri kabisa(ada, matibu, mavazi, afya, makazi) kwake na kwa watoto wetu.

Kutokana na hili huwa nakuwa na mawazo sana, kitu ambacho natamani kufanya maamuzi magumu ya kumwacha ila moyo unasita.

Ushauri wenu utaniponya.
 
Kwenye mapenzi Amani na furaha viwepo. Utani na mizaha iwepo, tatizo lako unatumika elimu Yako mpaka nyumbani kwako kwahiyo mwenzako akiongea kitu unakipima kutokana na elimu yake ya makaratasi.

Happy mwenyeshida ni wewe mke Hana tatizo Tena anaonekana mtu peace Sana na anapenda kufanya uwe na furaha ila wewe Kila akifanya vituko ufurahi wewe unamuona kituko tu kisa diploma.

Kunaujinga jinga unafanya mtaani au nyumbani ambao mkeo hapendi na anaona kabisa kufumba macho kwako na kusali Kila ulalapo na uamkapo ni unafiki tu, badili mienendo Yako na jitahidi kuwa flexible.

Akizidi mtandike makofi kadhaa Ili kurestore memory na atambue nafasi Yako Kama mume na si mkuu wa kaya Kama ulivojitanabaisha, maana mkuu wa kaya anaweza kuwa mwanamke au hata mtoto.
 
Miaka kumi hujamwelewa tu mwenzio, au labda kama neno mzaha limetumika vibaya!! Labda kama ana majibu mabaya mrekebishane 😀😀 au pia mkuu huenda uko serious sana !! Kila muda unawaza pesa na kazi !! Wakati mwenzako hiyo ndo njia ya kukusemesha ! Pengine pia akikutania ukanuna kidogo ndo anapenda. Na vipi yeye ukimfanyia mzaha anachukuliaje ?

Mimi pia napenda za utani (usio na madhara) , hata ikitokea sijamtania mwenzangu anaona kama siko sawa !! Atauliza mara mbili mbili kuna shida gani ?
 
Acha kumpiga mkeo kwanza, ila pia mbona ni jambo la kawaida??? kwani Dini mnatofautiana au ni moja?? pale alipokuambia unasali uongo ungemuuliza kwanini kiutaratibu angekujuza inawezekana kuna jambo umefanya ila wewe umetoka umeenda kukaa barazani ndio tatizo kwa madai umesusa, ila waswahili husema ukisusa wenzio wala

Acha kumnunia mkeo kwa mambo madogo sana, kwanza miaka 10 kwenye ndoa hujakubali kumzoea mtu kweli??? jaribu kukubali kua hilo ndio dhaifu lake hivyo mbebee kama mkeo songa mbele..........
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…