Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,561
- 21,536
Habari,
Husika na kichwa cha habari,
Kama kuna kitu cha kuangalia wakati wa kuoa na kuolewa ni hili suala la mume au mke ambaye kila linalotokea kwenye ndoa yenu yeye anaripoti kwao.
Katika uchumba wenu kuwa makini kuangalia unataka kuoa mke wa aina Gani, maana unaweza oa mwandishi wa familia.
Kila anachofanya na wewe bila kujali usiri wa mambo yenu yeye anaweka wàzi kwa familia na ndugu zao.
Ninasema hivi sababu Siri katika ndoa ni jambo ambalo lina umuhimu sana hasa katika kuleta maendeleo.
Pia amani yenu ipo kwenu nyie wawili na mambo yenu ila sio kwa mtu wa tatu ambaye hajui makubaliano yenu.
Sasa ukute mnakitu fulani mnataka kufanya Cha maendeleo yeye anaripoti kwao na kutangaza bila kujua adui wa mtu ni wa nyumbani mwake.
Ndugu wengi wao hawapendi kuona wenzao wanafanikiwa na kuwapita kunakuwa na kawivu Fulani.
Hapo utapigwa kipapai na ndugu utakuta hata hako kakiwanja hukajengi.
Achana na hayo ya maendeleo, njoo kwenye yale maijibishano ambayo yanatokea ndani, yeye huyo mbio anaripoti kwao kama muandishi wa kujitegemea wa online.
Umeoa au kuolewa na ndugu au familia nzima yaani Kila jambo linajulikana Kila mahali, ukienda Ukweni wanakuchora kama katuni Fulani.
Haya yote ni kwakuwa umeolewa au kuoa mke na mume ambaye friji lake haliwezi kugandisha.
Namaliza kwa kusema, kuoa mke au mume ambaye anatoa mambo ya ndani na kupeleka kwao ni zaidi ya Mchawi.