Mke anapokuwa ana elimu, fedha zaidi ya mume

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
645
Jambo hilo huwasumbua wengi sana, Ukweli ni kwamba ndoa nzuri au mbaya inategemea na malezi au tabia ya mtu kwa ujumla. Ndoa nyingi ambazo mmoja yuko juu sana na mwingine yuko chini sana, mara nyingi huwa ni ya maigizo.

Nje wanaonekana wana ndoa, ndani ni shida. Binafsi sijaweza kufanikiwa kushuhudia ndoa nyingi za wanawake matajiri sana au wenye majina makubwa ambazo ndani zina amani sana, labda kama watakuwa imara katika dini.
 
Narudia kwa mara ya mwisho: Ndoa inategemea na nyinyi wawili mmeiwekaje, huwezi kukopi au kuiga kila mtu na maisha yake. Kuna mwingine unaweza ukaona ananyanyasika kumbe mwenzio ni burudanii kabisa. hivyo zipo za wenye pesa ni za furaha na zipo za masikini ni za huzuni kila kikicha na kinyume chake pia. hivyo wewe jiangalie wewe na mwenzi wako mnataka nini ukiona haelekei chapa lapa.
 
Kwa hiyo kama unafikiria kuoana na mwanamke imara sana kiuchumi, au kielimu, sikushauri uache au uendelee, maamuzi ni yako, ila jitahidi kuhoji ni kwa nini hajaolewa�hasa kama ana umri wa miaka 35 na kuendelea.

Najua atakueleza sababu nyingi za kuachana na wapenzi wake wa zamani, nyingi zitaonyesha alioachana nao ndiyo walikuwa na matatizo.

Tafakari kwa makini zaidi, hasa kama alishawahi kuwa na mtoto au watoto au kuwepo kwenye ndoa. Kuwa kwenye ndoa ni raha lakini ni hatari kama unakuwa kwenye ndoa na mtu ambaye hakupi amani.
 
Back
Top Bottom